Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube hushughulikia vipi maelezo ya kupotosha?

Huku mabilioni ya watu wakitembelea huduma yetu kila siku - iwe wanatafuta maarifa, kupata habari mpya au maelezo zaidi kuhusu mada wanazozipenda, tuna wajibu wa kuwasaidia watu wapate maudhui ya ubora wa juu. Kwa hivyo, cha muhimu zaidi tunachoweza kufanya ni kuzidisha mazuri na kupunguza mabaya. Ndiyo maana tunakabiliana na maelezo ya kupotosha kwenye mfumo wetu kulingana na kanuni zetu za "K 4" (Kuondoa, Kupunguza, Kukuza na Kutuza): tunaondoa maudhui yanayokiuka sera zetu, tunapunguza mapendekezo ya maudhui yanayokaribia kukiuka sera, tunaangazia vyanzo vya kuaminika vya habari na taarifa na kuwatuza watayarishi wanaoaminika. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyoshughulikia maelezo ya kupotosha kwenye YouTube.

Kukabili maelezo ya kupotosha

Ni sera zipi zilizopo zinazokabili maelezo ya kupotosha kwenye YouTube?

Sera kadhaa katika Mwongozo wa Jumuiya yetu zinatumika moja kwa moja kwa maelezo ya kupotosha.

Sera ya Maelezo ya Kupotosha kuhusu Matibabu ya COVID-19 hairuhusu maudhui yanayoeneza maelezo ya kupotosha ya matibabu yanayokinzana na taarifa ya matibabu kutoka mamlaka za afya katika eneo au Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mwongozo wetu kuhusu matendo ya udanganyifu unajumuisha sera thabiti dhidi ya watumiaji wanaojiwakilisha kwa njia ya uongo au wanaohusika katika njia nyingine za udanganyifu. Hii inajumuisha matumizi ya udanganyifu ya maudhui ya hila (k.m. “wahusika bandia”) ambayo yanaweza kusababisha hatari kubwa. Tunajitahidi pia kulinda uchaguzi dhidi ya mashambulizi na kuathiriwa, ikiwa ni pamoja na kulenga kukabili shughuli za kuathiri siasa.

Pia, tuna sera dhidi ya uigaji. Akaunti zinazotaka kueneza maelezo ya kupotosha kwa kujiwakilisha kwa njia ya uongo kupitia uigaji zinakiuka sera zetu na zitaondolewa.

Na mwishowe, sera yetu ya matamshi ya chuki hairuhusu maudhui yanayopinga kuwepo kwa matukio makuu ya ukatili yaliyorekodiwa.

YouTube hushughulikia vipi maudhui yanayokaribia kukiuka sera na maelezo hatari ya kupotosha?

Maudhui yanayokaribia — lakini hayakiuki — Mwongozo wa Jumuiya yetu ni sehemu ya asilimia moja ya maudhui yanayotazamwa kwenye YouTube nchini Marekani. Mifumo yetu ya mapendekezo haipendekezi maudhui kama hayo kwenye YouTube, hali inayosaidia kupunguza kusambazwa kwa video au maudhui yanayokaribia kukiuka sera ambayo yanaweza kupotosha watumiaji kwa njia hatari.

YouTube hubaini vipi maudhui yanayochukuliwa kuwa maelezo hatari ya kupotosha?

Tumeweka mifumo kwa makini ili kutusaidia kubaini maelezo hatari ya kupotosha kwenye video nyingi katika YouTube. Kama sehemu ya mchakato huu, tunaomba wataalamu na wakaguzi kubaini iwapo maudhui yanahimiza matumizi ya njama au taarifa zisizo sahihi. Wataalamu hawa wamepewa mafunzo kwa kutumia mwongozo wa umma na hutoa mchango mkuu katika ubora wa video. Kutokana na mchango wa wakaguzi hawa, tunatumia mifumo ya mashine kujifunza iliyofanyiwa majaribio bora ili kubuni miundo inayotengeneza mapendekezo. Miundo hii husaidia kukagua mamia ya maelfu ya saa za video kila siku ili kupata na kupunguza kuenezwa kwa maelezo hatari ya kupotosha.

YouTube hutoa vipi maelezo bora zaidi kwa watumiaji?

Kwa maudhui ambapo usahihi na kuaminika ni muhimu, ikiwa ni pamoja na habari, siasa, matibabu na maelezo ya kisayansi, tunatumia mifumo ya mashine kujifunza inayoipa kipaumbele taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika katika mapendekezo na matokeo ya utafutaji.

Kwa aina fulani za maudhui ambayo huenda yana maelezo ya kupotosha mtandaoni, tuna vidirisha vya taarifa vinavyotoa taarifa ya ziada kutoka vyanzo vingine vya kuaminika pamoja na video hizo ili kukupa muktadha zaidi wa kufanya maamuzi ya busara.

YouTube hutathmini vipi chanzo cha kuaminika?

Tunatumia ishara kadhaa ili kubaini kuaminika, ikiwa ni pamoja na hoja kutoka huduma za Tafuta na Google na Google News kama vile ufaafu na upya wa maudhui, pia ubora wa chanzo, ili kubaini maudhui unayoona katika mifumo yetu rasmi ya habari. Pia, tunatumia wakadiriaji na wataalamu wa nje ili kutoa maoni na mwongozo muhimu kuhusu usahihi wa video.

Maelezo ya kupotosha yanatofautiana vipi na taarifa za kupotosha?

Ni muhimu kuzingatia mtayarishi wa maudhui, pamoja na nia yake, kuamua iwapo maudhui hayo ni taarifa ya kupotosha au maelezo ya kupotosha. Mtu akishiriki maelezo ya uongo, basi ni maelezo ya kupotosha. Iwapo mtu anajaribu kimakusudi kudanganya au kupotosha watu kwa kutumia kasi, kiwango na teknolojia za intaneti, basi tunabaini hali hii kuwa taarifa za kupotosha. Kwa kuwa taarifa za kupotosha ni sehemu ndogo ya maelezo ya kupotosha, tunatumia maelezo ya kupotosha kama hoja ya msingi kurejelea hali zote kwenye tovuti hii.