Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube hudhibiti vipi maudhui hatari?

YouTube ni mfumo huru wa video ambapo mtu yeyote anaweza kupakia video na kuishiriki na watu duniani. Kutokana na uhuru huu, kuna fursa na changamoto nyingi – ndiyo maana tunajitahidi kila wakati kusawazisha ubunifu na wajibu wetu wa kulinda jumuiya dhidi ya maudhui hatari. Katika kiini cha utaratibu wetu, tuna mbinu nne: Kuondoa maudhui yanayokiuka sera zetu haraka iwezekanavyo; Kupunguza kuenea kwa maelezo hatari ya kupotosha na maudhui yanayokaribia kukiuka sera zetu, Kukuza vyanzo vya kuaminika wakati watu wanatafuta habari na taarifa; na Kuzawadi Watayarishi na wasanii wanaoaminika, ambao wanatimiza masharti.

Kudhibiti maudhui hatari

YouTube huondoa vipi maudhui hatari?

Jukumu letu la uwajibikaji huanza na Mwongozo wa Jumuiya yetu. Sera hizi zimebuniwa kuhakikisha kuwa jumuiya yetu imelindwa. Hubainisha kinachoruhusiwa na kisichoruhusiwa kwenye YouTube na hutumika katika aina zote za maudhui kwenye mfumo wetu, ikiwa ni pamoja na video, maoni, viungo na vijipicha. Sera zetu hushughulikia masuala kama vile matamshi ya chuki, unyanyasaji, usalama wa watoto na itikadi hatari, miongoni mwa mengine.

Kila mojawapo ya sera yetu hubuniwa kwa ushirikiano na wataalamu wengi wa sera na wa sekta kutoka nje ya kampuni, pamoja na Watayarishi wa YouTube na tunakagua sera zetu kwa utaratibu ili kuhakikisha kuwa zimesasishwa. Mifano ni pamoja na masasisho makuu kwenye sera zetu za matamshi ya chuki na unyanyasaji mnamo 2019; uchapishaji wa sera yetu ya 2020 ili kushughulikia maudhui ya nadharia hatari za ujanja; na sera yetu ya maelezo ya kupotosha kuhusu matibabu ya COVID-19, ambayo imebadilika katika kipindi chote cha janga.

Tunaondoa maudhui yanayokiuka sera zetu haraka iwezekanavyo, kwa kutumia mseto wa watu na mashine kujifunza ili kutambua kwa haraka maudhui yanayoweza kuwa na matatizo. Pia, tunategemea jumuiya ya YouTube na wataalamu kwenye mpango wetu wa Wapigaripoti wa Kuaminika ili kutusaidia kutambua maudhui ambayo huenda yana matatizo kwa kuyaripoti kwetu moja kwa moja. Tunajitahidi zaidi ili kuhakikisha kuwa maudhui yanayokiuka sera zetu hayatazamwi zaidi, au hata hayatazamwi hata kidogo, kabla yaondolewe. Mifumo yetu otomatiki ya kuripoti hutusaidia kutambua na kukagua maudhui kabla yatazamwe na jumuiya yetu.

Baada ya maudhui kama hayo kutambuliwa, watu wanaokagua maudhui hutathmini iwapo yanakiuka sera zetu. Iwapo yanakiuka, tutayaondoa na kuyatumia kufunza mashine zetu ili zitambue vizuri siku zijazo. Wakaguzi wetu wa maudhui pia hulinda maudhui ambayo yana lengo bayana la elimu, hali halisi, sayansi au sanaa [EDSA].

YouTube hupunguza vipi kuenea kwa maelezo hatari ya kupotosha na maudhui yanayokaribia kukiuka sera?

Ingawa Mwongozo wa Jumuiya yetu huweka kanuni za maudhui kwenye YouTube, bado kutakuwa na maudhui ambayo yanakaribia kukiuka sera zetu, lakini hayakiuki. Maudhui haya yanayokaribia kukiuka sera huwakilisha sehemu ya asilimia moja ya video zinazotazamwa kwenye YouTube. Hata hivyo, hata sehemu ya asilimia ni nyingi zaidi.

Kwa hivyo, mnamo 2019, tulitangaza mabadiliko kwenye mifumo yetu ya mapendekezo ili kupunguza kuenea kwa maudhui yanayokaribia kukiuka sera, hali iliyosababisha kupungua kwa asilimia 70 kwa muda wa kutazama wa maudhui ambayo yanapendekezwa kwa wasiofuatilia nchini Marekani mwaka huo. Pia tulishuhudia kupunguka kwa muda wa kutazamwa kwa maudhui yanayokaribia kukiuka sera kutoka kwenye mapendekezo katika masoko mengine. Na kuanzia Machi 2021, tulitekeleza mabadiliko kwenye mfumo wetu wa mapendekezo ili kupunguza maudhui yanayokaribia kukiuka sera katika kila soko tunakohudumu. Tunajitahidi kuendeleza shughuli za kupunguza mapendekezo ya maudhui yanayokaribia kukiuka sera. Ingawa mabadiliko ya algoriti huchukua muda kuonekana na unaweza kuona matumizi ya maudhui yanayokaribia kukiuka sera yakiongezeka na kupungua, lengo letu ni kuhakikisha kuwa kuonyeshwa kwa maudhui yanayokaribia kukiuka sera kwa wasiofuatilia, yanayopendekezwa yamepungua asilimia 0.5.

YouTube hukuza vipi maudhui yanayoaminika?

Kuna ishara nyingi - kama vile ufaafu na umaarufu - ambazo huzingatiwa katika kubainisha video ambazo kwa kawaida unaziona katika mapendekezo na utafutaji kwenye YouTube. Hata hivyo, katika mada kama vile habari, siasa, matibabu na maelezo ya sayansi, tunajua kuwa hakuna kibadala cha uaminifu. Ndiyo maana tumezindua vipengele vingi ili kukabili changamoto hii kikamilifu.

Kwa mfano, katika matokeo ya utafutaji na video zinazopendekezwa, tunakuza vyanzo vya kuaminika kwa matukio ya habari na mada zinazoweza kuwa na maelezo ya kupotosha. Tumeweka pia vipengele vya bidhaa kama vile rafu ya Habari Zinazojiri na rafu ya Habari Kuu, zinazoangazia video zinazofaa kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika.

Muktadha ni muhimu wakati wa kutathmini habari, kwa hivyo tunaweka vidirisha vya taarifa vinavyoangazia taarifa za maandishi pamoja na video na matokeo fulani ya utafutaji ili kukusaidia kufanya maamuzi yako kuhusu maudhui unayopata kwenye YouTube.

YouTube huzawadi vipi watayarishi na wasanii wanaoaminika?

Kukubaliwa katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) ni mafanikio makuu katika harakati za Mtayarishi yeyote. Kama sehemu ya Mpango wa Washirika wa YouTube, Watayarishi wanaweza kuchuma mapato kutokana na maudhui yao na pia kufikia manufaa na usaidizi.

Kwa miaka michache iliyopita, tumechukua hatua za kuboresha masharti ya uchumaji wa mapato ili wanaotuma taka, waigaji na wengine wasidhuru mfumo au kuwahasiri Watayarishi ambao wametumia muda, nguvu na ari yao kutoa maudhui yenye ubora wa juu.

Ili kutuma ombi la kuwa katika Mpango wa Washirika wa YouTube, lazima vituo vitimize masharti ya kujiunga yanayohusiana na muda wa kutazama na idadi ya wanaofuatilia vituo. Baada ya kutekelezwa, timu ya ukaguzi wa YouTube huhakikisha kuwa vituo vinavyotimiza masharti ya kujiunga na kufuata mwongozo wetu wote ndivyo tu vinavyosajiliwa kwenye mpango, hali inayofanya vituo hivyo vitimize masharti ya kupokea uwezo wa kufikia matangazo na bidhaa nyingine za uchumaji wa mapato.

Kwa kawaida watangazaji hawapendi kuhusishwa na maudhui yenye utata au nyeti kwenye YouTube - jinsi inavyobainishwa kwenye Mwongozo wetu wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji. Iwapo Mtayarishi amewasha uchumaji wa mapato kwenye matangazo katika video lakini wakaguzi na mifumo yetu ya kiotomatiki ibaini kuwa video haitii Mwongozo wetu wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji, video hiyo itaonyesha matangazo machache au isiyaonyeshe hata kidogo kumaanisha kuwa hatapata pesa kutokana na video hiyo. Tunaweza pia kufunga kituo cha mtayarishi kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube kwa kukiuka zaidi au mara kwa mara Sera za uchumaji wa mapato kwenye YouTube.

Lengo letu kuu ni uwajibikaji na kila kitu tunachofanya huzingatia kigezo hicho. Madhara kwa watumiaji na biashara huzidi manufaa yote.