Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube husaidia vipi nidhamu dijitali ya watumiaji?

Tunaamini kuwa teknolojia inapaswa kuboresha maisha, wala si kuyaathiri vibaya, kwa hivyo tumejitolea kukupa nyenzo unazohitaji ili kuendeleza uhusiano mzuri na teknolojia. Tumebuni zana kadhaa za kukupa ufahamu mzuri wa jinsi unavyotumia muda kwenye YouTube, kwa hivyo unaweza kufanya uamuzi mzuri kuhusu jinsi ungependa YouTube ifae maisha yako.

Kuendeleza nidhamu dijitali

Je, una mifano michache ya zana za nidhamu dijitali?

Mifano michache inajumuisha “muda uliotazama video”, “kikumbusho cha kupumzika kidogo”, “kikumbusho cha wakati wa kulala" na uwezo wa “kupima muda”. Hubuniwa kusaidia kila mtu afahamu vyema matumizi yake kwenye YouTube, kuondoka panapohitajika na kudumisha desturi nzuri kwa ajili ya familia yote.

Kwa nini YouTube huendelea kucheza video kiotomatiki?

Ukishaanza kutazama video, tunatoa orodha ya video nyingine ili uzitazame baada ya hii kupitia kipengele cha "kucheza kiotomatiki". Ni wajibu wetu kukupa zana unazohitaji ili udhibiti hali yako ya utumiaji kwenye YouTube, kwa hivyo unaweza kuzima kipengele cha "kucheza kiotomatiki" wakati wowote kwa kutumia swichi ya kugeuza inayopatikana kwenye ukurasa wa kutazama.