Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube hulinda vipi jumuiya dhidi ya chuki na unyanyasaji?

Tumebuni sera zetu za matamshi ya chuki na unyanyasaji kwa kushauriana na Watayarishi walioshiriki mitazamo yao, pia mashirika ya wataalamu wanaochunguza uchokozi wa mtandaoni na kuenea kwa mambo ya chuki mtandaoni. Tumekutana pia na mashirika ya sera kutoka mirengo yote ya sekta ya siasa. Jinsi tunavyokabili maudhui mengine yanayokiuka sera, tunajitahidi kwa haraka kuondoa maudhui yanayokiuka sera zetu za chuki na unyanyasaji.

Kukabili chuki

Nini tofauti kati ya matamshi ya chuki na unyanyasaji?

Sera yetu ya matamshi ya chuki hulinda vikundi mahususi na wanachama wa vikundi hivyo. Tunaondoa maudhui yanayokiuka sera. Tunachukulia maudhui kuwa matamshi ya chuki yanapochochea chuki au vurugu dhidi ya vikundi kulingana na sifa zinazolindwa kama vile umri, jinsia, mbari, tabaka, dini, mwelekeo wa kingono au hali ya kuwa mwanajeshi aliyestaafu. Sera hii pia inajumuisha aina za kawaida za chuki mtandaoni kama vile kushusha hadhi ya wanachama wa vikundi hivi; kuwataja kuwa duni au waovu kabisa; kutangaza mambo ya chuki kama vile Mfumo wa Kinazi; kutangaza nadharia za ujanja kuhusu vikundi hivi; au kupinga kuwepo kwa matukio makuu ya vurugu yaliyorekodiwa, kama vile ufyatuaji shuleni.

Wasimamizi wakuu wa YouTube kutoka Timu ya Uaminifu na Usalama hufafanua jinsi tunavyolinda jumuiya yetu dhidi ya matamshi ya chuki.

Sera yetu ya unyanyasaji hulinda watu wanaoweza kutambuliwa na tunaondoa maudhui yanayokiuka sera. Tunachukulia maudhui kuwa unyanyasaji yanapolenga mtu kupitia matusi makali kwa muda mrefu kulingana na sifa mahususi, ikiwa ni pamoja na hali yake ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolinda au hali ya maumbile. Sera hii pia inajumuisha tabia hatari kama vile kutusi au kufedhehesha watoto kimakusudi, vitisho, uchokozi, upekuzi na utangazaji wa taarifa binafsi au kuhimiza tabia mbaya ya mashabiki.

Wasimamizi wakuu kutoka Timu ya Uaminifu na Usalama wa YouTube wanafafanua jinsi tunavyolinda jumuiya yetu dhidi ya unyanyasaji.

YouTube hudhibiti vipi nadharia hatari za ujanja?

Kama sehemu ya sera zetu za chuki na unyanyasaji, haturuhusu maudhui yanayolenga mtu au kikundi kupitia nadharia za ujanja ambazo zimetumiwa kutetea vurugu kwenye mazingira halisi. Kwa mfano, maudhui yanayotisha au kunyanyasa mtu kwa kupendekeza kuwa wanahusika katika moja wapo ya nadharia hizi hatari, kama vile QAnon au Pizzagate. Kama kawaida, muktadha ni muhimu, ili habari kuhusu matatizo haya au maudhui yanayojadili bila kulenga mtu au kikundi cha watu wanaolindwa yasiondolewe. Kutokana na hali inayobadilika na kubadilisha mbinu kwa vikundi vinavyotangaza nadharia hizi za ujanja, tutaendelea kubadilisha sera zetu ili ziendelee kufaa na kuchukua hatua zinazohitajika ili kutimiza wajibu huu.

YouTube hutekeleza vipi sera za matamshi ya chuki na unyanyasaji?

Si rahisi kutekeleza sera za matamshi ya chuki na unyanyasaji, kwa kuwa uamuzi unahitaji ufahamu bora wa lugha na miktadha husika. Ili tuweze kuendelea kutekeleza sera zetu, tuna timu za ukaguzi zenye ujuzi wa lugha na mada husika. Pia tunatumia mfumo wa mashine kujifunza kutambua kwa haraka maudhui yanayoweza kuwa hatari ili kuyatuma kwa watu wanaokagua. Kila robo ya mwaka, tunaondoa makumi ya maelfu ya video na vituo vinavyokiuka sera hizo. Kwa vituo vinavyokiuka sera zetu mara kwa mara, tunachukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuviondoa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (hali inayozuia kituo kisichume mapato), kutoa maonyo (kuondoa maudhui), au kufunga kituo.

Je, sera hizi huathiri vyanzo vya siasa ambavyo YouTube haikubaliani navyo, kwa njia isiyo sawa?

Tunapobuni na kubadilisha sera zetu, tunahakikisha kuwa tunasikia kutoka vyanzo tofauti, ikiwa ni pamoja na Watayarishi, wataalamu katika eneo fulani, watetezi wa usemi na mashirika ya sera kutoka mirengo mbalimbali ya siasa. Baada ya sera kubuniwa, tunatumia muda wa kutosha kuhakikisha kuwa sera mpya zilizobuniwa zinatekelezwa wakati wote na timu yetu ya wakaguzi kote duniani kulingana na mwongozo huru, bila kujali anayechapisha maudhui. Tumebuni mfumo wa vyanzo vinavyoaminika, ambao huwezesha jumuiya yetu pana ya Watayarishi wabadilishane mawazo.

Je, kuna hali ambapo sera ya matamshi ya chuki haizingatiwi?

YouTube ni mfumo wa kujieleza kwa njia huru. Ingawa haturuhusu matamshi ya chuki, tunaruhusu video ambazo zina lengo la elimu, hali halisi, sayansi au sanaa. Hii inaweza kujumuisha, kwa mfano, video halisi kuhusu kikundi cha chuki; ingawa video hiyo ya hali halisi inaweza kuwa na matamshi ya chuki, tunaweza kuiruhusu iwapo lengo lake linaonekana kwenye maudhui, maudhui hayatangazi matamshi ya chuki, na watazamaji wanapewa muktadha wa kutosha ili kuelewa kinachorekodiwa na kwa nini. Hatua hii, hata hivyo, si njia rahisi ya kuhimiza matamshi ya chuki na unaweza kuripoti kwa timu zetu za ukaguzi iwapo unaamini kuwa umeona maudhui yanayokiuka sera zetu za matamshi ya chuki.

YouTube hushughulikia vipi unyanyasaji unaojirudia?

Tunaondoa video zinazokiuka sera yetu ya unyanyasaji. Pia tunatambua kuwa wakati mwingine unyanyasaji hufanyika kupitia msururu wa tabia inayorudiwa kwenye video au maoni mengi, hata wakati video mahususi haziwezi kukiuka sera yetu. Vituo vinavyokiuka mara kwa mara sera yetu ya unyanyasaji vitaondolewa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP), hali inayoondoa uwezo wa kuchuma pesa kwenye YouTube, ili kuhakikisha kuwa tunawatuza tu Watayarishi wanaoaminika. Vituo hivi pia vinaweza kupokea maonyo (hali inayoweza kusababisha kuondolewa kwa maudhui) au kufungwa kwa akaunti.

Ni zana zipi zinapatikana kwa Watayarishi ili wajilinde na kudhibiti mazungumzo kwenye kituo chao?

Ingawa lengo la sera na mifumo yetu ni kupunguza uzito uliowekwa kwa Watayarishi kujilinda dhidi ya chuki na unyanyasaji, tumebuni pia zana za kuwasaidia kudhibiti hali yao ya utumiaji, jinsi ilivyoelezewa hapa chini kwa muhtasari.

Tunawapa Watayarishi zana za kudhibiti maoni ili waweze kudhibiti mazungumzo kwenye vituo vyao. Tunazuia maoni ambayo huenda hayafai ili yakaguliwe. Kwa hivyo Watayarishi wanaweza kuamua vyema maudhui yanayofaa hadhira yao. Pia, tuna zana nyingine zinazowezesha Watayarishi kuzuia maneno fulani katika maoni, kuzuia watu fulani wasitoe maoni, au kukabidhi haki za kudhibiti kwa watu wengine ili waweze kufuatilia maoni vyema kwenye kituo chao.

Ili kuhimiza mazungumzo ya heshima kwenye YouTube, tuna kipengele ambacho kitaonya watumiaji iwapo maoni yao yataonekana kukera wengine, hali inayowapa chaguo la kupitia na kubadilisha kabla ya kuchapisha.

Mwisho, tuna orodha ya nyenzo za kusaidia Watayarishi kuhisi salama kwenye YouTube. Tunajua kuna kazi nyingi inayotakiwa kufanywa na tumejitolea kuendeleza kazi hii.