Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

Jinsi YouTube Huwezesha Shughuli za Uchaguzi na Michakato ya Kiraia kwa Kuwajibika

Katika historia, 2024 ndio mwaka wenye shughuli nyingi zaidi za uchaguzi, huku zaidi ya nusu ya watu duniani wakiwa katika nchi zitakazoandaa upigaji kura katika nchi nzima. Huku kukiwa na watumiaji kote duniani wanaokuja kwenye YouTube kupata habari na taarifa kuhusu majukumu yao ya kiraia, iwe ni usajili wa wapiga kura au mahali pa karibu kwao pa kupigia kura, tuna wajibu wa kusaidia kuwepo kwa raia wanaofahamu mambo na kuendeleza majadiliano mazuri ya kisiasa. Ili tutekeleze wajibu huu, huwa tunaondoa maudhui yanayokiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu, ikiwa ni pamoja na maudhui ya uchaguzi, kuweka habari na taarifa zenye ubora wa juu kuhusu uchaguzi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika katika matokeo ya utafutaji na mapendekezo, kupunguza kuenea kwa maelezo hatari ya kupotosha kuhusu uchaguzi na kuwatuza watayarishi wanaoaminika kupitia Mpango wa Washirika wa YouTube. Sera zetu zinatumika kwa kila mtu na zinatekelezwa kwa njia sawa, bila kujali mitazamo ya kisiasa iliyotolewa, lugha ya maudhui au jinsi maudhui hayo yalivyozalishwa.

Kusaidia uadilifu wa kisiasa

YouTube huondoa vipi maudhui yanayohusiana na uchaguzi ambayo yanakiuka sera?

Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube una maelekezo ya wazi kuhusu maudhui yasiyoruhusiwa kwenye mfumo wetu na huwa tunaondoa maudhui yanayokiuka sera hizi.

Sera mahususi dhidi ya maelezo ya kupotosha kuhusu uchaguzi inajumuisha:

  • Kuzuia au Kuwakatisha Tamaa Wapiga Kura - Hairuhusu maudhui yanayolenga kuwapotosha wapigaji kura kuhusu muda, mahali na namna au masharti ya kutimiza ili kuweza kupiga kura au madai ya uongo yanayoweza kuwakatisha tamaa zaidi watu kupiga kura. k.m. video inayowafahamisha watazamaji kuwa wanaweza kupiga kura kupitia mbinu bandia kama vile kutuma ujumbe wa maandishi ulio na chaguo lao kwenye namba fulani.

  • Mgombeaji Kutimiza Masharti - Hairuhusu maudhui yanayoendeleza madai ya uongo yanayohusiana na masharti wanayofaa kutimiza wagombeaji wa sasa wa siasa na wafanyakazi wa serikali wa sasa waliochaguliwa. Masharti ya kugombea yanayozingatiwa yanalingana na sheria inayotumika ya kitaifa na yanajumuisha umri, uraia, au hali muhimu.

  • Uchochezi ili kukatiza michakato ya demokrasia - Hairuhusu maudhui yanayohimiza wengine kukatiza michakato ya demokrasia. Hii inajumuisha kuzuia au kuingilia utaratibu wa kupiga kura.

Mwongozo wa Jumuiya unaotumika kwa maudhui ya aina zote, ikiwa ni pamoja na uchaguzi, unajumuisha:

  • Sera Dhidi ya Unyanyasaji - Kwa mujibu wa sera zetu dhidi ya Unyanyasaji na uchokozi wa mtandaoni, haturuhusu maudhui yanayotishia watu kama vile wasimamizi wa uchaguzi, wagombeaji au wapiga kura.

  • Sera Dhidi ya Matamshi ya Chuki - Kwa mujibu wa sera yetu dhidi ya Matamshi ya chuki, haturuhusu maudhui yanayohimiza vurugu au chuki dhidi ya watu au vikundi kwa misingi ya sifa fulani. Hii inajumuisha, kwa mfano, maudhui yanayoonyesha mtu aliyehudhuria mkutano wa kisiasa akidhalilisha kikundi fulani kwa misingi ya sifa inayolindwa, kama vile mbari, dini au mwelekeo wa kingono.

  • Maudhui Yaliyobadilishwa kwa Hila - Sera hii hairuhusu maudhui yaliyobadilishwa au yaliyochezewa kwa kutumia teknolojia kwa namna ambayo yanapotosha watumiaji (kwa kawaida mbali na klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha) na yanaweza kusababisha madhara mabaya sana. Kwa mfano, video iliyohaririwa kwa kutumia teknolojia ili kumfanya mgombeaji wa ofisi ya umma atoe madai ya uongo kuwa anajiondoa kwenye kinyang'anyiro.

  • Maudhui Yasiyo Halisi - Kwa mujibu wa [Sera za maelezo ya kupotosha], haturuhusu maudhui yanayoweza kusababisha madhara mabaya sana kwa kudai kwa njia ya uongo kwamba video ya zamani kutoka kwenye tukio la zamani imetokana na tukio la sasa(https://support.google.com/youtube/answer/10834785?hl=en). Kwa mfano, video inayoonyesha mkuu wa nchi akiunga mkono mzozo wa vurugu ambao kamwe hakuunga mkono.

  • Sera dhidi ya Maudhui ya Vurugu au ya Kuogofya - Kwa mujibu wa Sera zetu dhidi ya maudhui ya vurugu au ya kuogofya, haturuhusu maudhui yanayowahimiza wengine kutenda vitendo vya vurugu, ikiwa ni pamoja na vitendo vinavyowalenga wasimamizi wa uchaguzi, wagombeaji au wapiga kura.

  • Sera dhidi ya Uigaji - Kwa mujibu wa sera yetu dhidi ya Uigaji, haturuhusu maudhui yanayolenga kuiga mtu au chaneli, kama vile mgombeaji wa kisiasa au chama chake cha siasa.

  • Sera dhidi ya Taka, Tabia za Udanganyifu na Ulaghai - Sera hii hairuhusu maudhui ya kupotosha yanayolenga kuwatumia vibaya watumiaji wa YouTube.

  • Sera dhidi ya Viungo vya Nje - Maudhui yaliyo na viungo vya nje vinavyoelekeza kwenye nyenzo zinazoweza kukiuka sera zetu na zinaweza kusababisha madhara mabaya sana, kama vile maudhui ya kupotosha au ya udanganyifu yanayohusiana na uchaguzi, matamshi ya chuki yanayolenga vikundi vya watu wanaolindwa au unyanyasaji unaolenga wasimamizi wa uchaguzi, wagombeaji au wapiga kura. Hii inaweza kujumuisha URL za kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyinginezo katika video kwa kutamka, pamoja na njia nyinginezo za kutuma viungo.

Wakati mwingine, video ambazo huenda zikakiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu zinaweza kuruhusiwa kwenye YouTube ikiwa maudhui hayo yana muktadha wa Elimu, Makala Hali Halisi, Kisayansi au Kisanaa (EDSA).

Ili kubaini iwapo video inaweza kuruhusiwa kwa mujibu wa EDSA, tunazingatia vigezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na mada na maelezo ya video pamoja na muktadha unaotolewa kwenye sauti au picha ya video hiyo. Kwa mfano, jambo linaloweza kuruhusiwa kwa mujibu wa EDSA ni maudhui ambapo mtu anatoa madai ya uongo kwamba watu wenye umri mkubwa kuliko umri fulani hawaruhusiwi kupiga kura katika uchaguzi wa kidemokrasia na pia kuweka wazi kwenye video, sauti, mada au maelezo kuwa madai haya si kweli.

Kushughulikia maelezo ya kupotosha ya uchaguzi yanayotayarishwa kwa AI

Changamoto zinazoletwa na AI zalishi zimekuwa jambo ambalo YouTube inafuatilia kwa makini, lakini tunafahamu kuwa AI inaleta hatari mpya ambazo watendaji wabaya wanaweza kujaribu kutumia wakati wa uchaguzi. AI pia inaweza kutumiwa kuzalisha maudhui yanayoweza kuwapotosha watazamaji—hasa ikiwa hawafahamu kuwa video hiyo imebadilishwa au imebuniwa kwa njia sanisi. Ili kushughulikia suala hili ipasavyo na kuwafahamisha watazamaji wakati maudhui wanayotazama yamebadilishwa au ni sanisi, tutaanza kuleta masasisho yafuatayo:

  • Ufumbuzi wa Mtayarishi: Watayarishi watatakiwa kufumbua wanapotayarisha maudhui sanisi au yaliyobadilishwa, ikiwa ni pamoja na kutumia zana za AI. Hii itajumuisha maudhui ya uchaguzi.

  • Kuweka lebo: Tutawekea lebo maudhui halisi ya uchaguzi ambayo ni sanisi au yaliyobadilishwa ambayo hayakiuki sera zetu, ili kuwaonyesha wazi watazamaji kuwa baadhi ya maudhui ni sanisi au yalibadilishwa. Katika maudhui ya uchaguzi, lebo hii itaonyeshwa kwenye kicheza video pamoja na maelezo ya video na itaonekana bila kujali mtayarishi, mitazamo ya kisiasa au lugha.

Jaribio linaloonyesha lebo iliyowekwa kwenye kicheza video na kidirisha cha maelezo.

Kutatua mapema matatizo yanayoibuka

Tunapaswa kuwa na ufahamu kuhusu vitisho vinavyoibuka ili tuweze kuondoa haraka iwezekanavyo maudhui yanayokiuka sera kando na maudhui ambayo tayari tumeyapiga marufuku. Ili tuweze kushughulikia mapema masuala yanayoibuka kabla yafike au yasambae kwenye mfumo wetu, tumeweka michakato ya kina ili kuzipatia timu zetu uwezo wa kushughulikia masuala haya vizuri.

Mnamo 2018, tulianzisha Kituo cha Ufuatiliaji, timu ya ndani inayofuatilia na kutambua mambo mapya yanayohusu tabia mbaya na maudhui yasiyofaa ili kusaidia kuyashughulikia mapema.

Vilevile, tunashirikiana kwa karibu na Kikundi cha Google cha Uchanganuzi wa Tishio (TAG) ili kutambua shughuli za ushawishi ulioratibiwa kwenye YouTube na kufunga chaneli na akaunti za wanaoendeleza shughuli hizo. Hii ni pamoja shughuli ya udukuzi inayoungwa mkono na serikali kwa lengo la kukatiza michakato ya uchaguzi. Kupitia TAG, tunazitumia asasi za kutekeleza sheria na washirika wa sekta taarifa za uchunguzi, mbinu bora na taarifa kuhusu tishio. TAG hufumbua kwenye taarifa zao za kila mwezi za Bulletin kuhusu kampeni za shughuli za ushawishi ulioratibiwa ambazo zimesimamishwa kwenye mifumo ya Google, ikiwa ni pamoja na YouTube.

Je, YouTube hupataje taarifa za uchaguzi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika?

Kwa habari na mada za taarifa kama vile za uchaguzi na shughuli za kiraia, usahihi na kuaminika ni muhimu. Hii ndiyo sababu tulijumuisha dhana ya “kuaminika” katika mfumo wetu wa mapendekezo. Watumiaji wanapotazama au kutafuta maudhui ya uchaguzi kwenye YouTube, mfumo wetu wa mapendekezo huonyesha dhahiri maudhui yanayoaminika kwenye matokeo ya utafutaji, ukurasa wa kwanza na kidirisha cha “Tazama Inayofuata”.

Tunatumia ishara kadhaa ili kubaini kuaminika, ikiwa ni pamoja na ufaafu na upya wa maudhui, pia ubora wa chanzo, ili kubaini maudhui unatakayoyaona kwenye mifumo yetu rasmi yenye lebo ya habari. Pia, tunatumia wakadiriaji na wataalamu wa nje ili kutoa mchango na mwongozo muhimu kuhusu usahihi wa video. Wakadiriaji hawa wanatoka kote duniani na wamepata mafunzo kupitia mkusanyiko wa kina wa, mwongozo wa ukadiriaji unaopatikana kwa umma .

Vipengele vya habari husaidia kupata habari zinazohusiana na uchaguzi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika

Upatikanaji unategemea eneo la kijiografia

Vipengele vya bidhaa vinavyosaidia kupata habari kutoka kwenye vyanzo vinavyoaminika kwenye YouTube ni pamoja na:

Ukurasa wa kutazama wa habari kwenye YouTube

*Skrini ya Majaribio. Ni kwa Madhumuni ya Mfano Pekee

Ili kuwasaidia watazamaji kugundua pande tofauti za habari na kupata taswira zao wenyewe kuhusu ulimwengu, tulizindua ukurasa wa kutazama unaoleta pamoja mkusanyiko wa maudhui ya habari kutoka kwenye vyanzo anuwai na vinavyominika kwenye YouTube.

Habari zinazojiri kwenye ukurasa wa kwanza

Tukio kuu la habari zinazojiri linapofanyika, tunataka kuhakikisha kuwa watazamaji wetu wanafahamu na wanaweza kufikia taarifa za kuaminika kwa urahisi. Katika hali hizo rafu ya Habari Zinazojiri huonekana moja kwa moja kwenye ukurasa wa kwanza. Rafu hii huangazia video zinazofaa kutoka vyanzo vya habari vinavyoaminika kuhusu matukio ya habari ya umuhimu wa kitaifa.

*Skrini ya majaribio. Ni kwa madhumuni ya kutoa mifano pekee.

Habari kuu kwenye Matokeo ya Utafutaji

Watazamaji wanapotafuta mada zinazohusiana na habari, wataona sehemu ya Habari Kuu kila wakati karibu na sehemu ya juu ya matokeo ya utafutaji, inayoonyesha matokeo yanayofaa kutoka vyanzo vinavyoaminika.

*Skrini ya majaribio. Ni kwa madhumuni ya kutoa mifano pekee.

Habari kuu kwenye ukurasa wa kwanza

Watazamaji wanapotafuta mada zinazohusiana na habari, wataona sehemu ya Habari Kuu kila wakati karibu na sehemu ya juu ya matokeo ya utafutaji, inayoonyesha matokeo yanayofaa kutoka vyanzo vinavyoaminika.

*Skrini ya majaribio. Ni kwa madhumuni ya kutoa mifano pekee.

Vidirisha vya taarifa huwapatia watumiaji muktadha zaidi ili kuwasaidia kufanya uamuzi bora kuhusu maudhui kwenye mfumo wetu

Dirisha la habari zinazoendelea

Katika hali za habari zinazoendelea, viungo vinavyoelekeza kwenye makala za habari za maandishi kutoka vyanzo vinavyoaminika vinaweza kuonyeshwa sehemu ya juu ya matokeo husika ya utafutaji, kwa kuwa huenda video yenye ubora wa juu isipatikane papo hapo.

*Skrini ya majaribio. Ni kwa madhumuni ya kutoa mifano pekee.

Kidirisha cha taarifa za ufadhili wa wachapishaji

Ili kutoa muktadha zaidi kuhusu vyanzo vya habari, taarifa kuhusu ufadhili zinaweza kuonyeshwa kwa wachapishaji wa serikali au wanaofadhiliwa na umma.

*Picha, vichwa vya habari na vyanzo vimeigwa ili kutolea mifano kipengele hiki.

Kidirisha cha taarifa kuhusu muktadha wa mada

Ili kutoa muktadha zaidi kuhusu mada zilizo katika hatari ya kutolewa maelezo ya kupotosha, kama vile upigaji kura kupitia barua, kidirisha cha taarifa kinaweza kuonyeshwa katika sehemu ya juu ya matokeo ya utafutaji au chini ya video ili kuonyesha taarifa msingi ya usuli iliyotoka kwenye vyanzo vinavyoaminika

*Picha, vichwa vya habari na vyanzo vimeigwa ili kutolea mifano kipengele hiki.

Nyakati za matukio muhimu ya kiraia na uchaguzi, tunafanya juhudi zaidi ili kupata taarifa kutoka vyanzo vinavyoaminika

Kando na vipengele vyetu visivyozimwa kamwe vinavyoweka taarifa kutoka vyanzo vinavyoaminika kwenye mfumo wetu, tunaweza kuzindua vipengele zaidi nyakati za matukio muhimu ya kiraia na uchaguzi.

Vidirisha vya taarifa kuhusu mgombeaji

Kwa baadhi ya chaguzi, taarifa za ziada kama vile chama cha mgombeaji zinaweza kutolewa kwa wagombeaji wote wa taifa. Kando na hayo, kwa wagombeaji walio na chaneli rasmi za YouTube, chaneli zao zinaweza kubandikwa kwa chaguzi hizo mahususi.

Wawaniaji wetu wa wadhifa wa mkuu wa serikali wametimiza masharti ya kupokea kadi kubwa inayoonyeshwa upande wa kulia.

*Picha, vichwa vya habari na vyanzo vimeigwa ili kutolea mifano kipengele hiki.

Vidirisha vya taarifa kuhusu upigaji kura

Watazamaji wanaotafuta mada zinazohusiana na upigaji kura, viungo vinavyoelekeza kwenye taarifa zinazoaminika kuhusu "jinsi ya kujisajili ili kupiga kura" na "jinsi ya kupiga kura" vinaweza kuonyeshwa, vikiwa vinaelekeza kwenye vyanzo vinavyoaminika vya washirika wengine wa data wasioegemea upande wowote kama vile Democracy Works.

*Picha, vichwa vya habari na vyanzo vimeigwa ili kutolea mifano kipengele hiki.

Vidirisha vya taarifa kuhusu matokeo ya uchaguzi

Watazamaji wanapotafuta matokeo ya uchaguzi au kutazama video zozote zinazohusiana na uchaguzi, kiungo kinachoelekeza kwenye kipengele cha Google cha “Matokeo ya Uchaguzi”, kwa hisani ya wahusika wengine wanaoaminika, kama vile Associated Press, kinaweza kuonyeshwa.

*Picha, vichwa vya habari na vyanzo vimeigwa ili kutolea mifano kipengele hiki.

Vikumbusho kwa wapiga kura

Katika muda wote wa uchaguzi, tunaweza kuwapa watazamaji viungo vya taarifa zinaoaminika zinazotolewa wakati ufaao kuhusu mchakato wa upigaji kura moja kwa moja kwenye ukurasa wa kwanza, kama vile “jinsi ya kujisajili ili kupiga kura”, “jinsi ya kupiga kura”, na “jinsi ya kujitolea kuwa mfanyakazi wa shughuli za kura”.

*Skrini ya majaribio. Ni kwa madhumuni ya kutoa mifano pekee.

Je, YouTube huwatuza na kuwasaidia vipi watayarishi – ikiwa ni pamoja na watayarishi wa maudhui ya habari na ya siasa pamoja na wagombeaji katika nyanja zote za kisiasa?

Biashara yetu ni ya kipekee ikilinganishwa na mifumo mingine kwa sababu kwa zaidi ya miaka 15, tumekuwa na mfumo wa ugavi wa mapato ambao ni Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) na huwa tunawatumia hundi watayarishi waliotimiza masharti kila mwezi.

Tunazingatia uchumaji wa mapato kwenye mfumo wetu kuwa ni fursa maalum. Ni lazima watayarishi wakubaliwe kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) ili waweze kuchuma mapato kutokana na maudhui yao.

Masharti muhimu ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube ni kufuata Sera za uchumaji wa mapato kwenye YouTube, zinazojumuisha [Mwongozo wa Jumuiya] yetu(https://support.google.com/youtube/answer/9288567), Sheria na Masharti na Sera za mpango wa Google AdSense. Sera hizi hutumika kwenye chaneli ya mtayarishi kwa jumla, si tu video mahususi. Na huwa tunakagua chaneli ya kila anayetuma ombi kabla ya kuidhinisha.

Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, tumechukua hatua za kuimarisha masharti ya uchumaji wa mapato ili watumaji wa taka, waigaji na watendaji wengine wabaya wasiweze kuharibu mfumo au kutumia vibaya watayarishi ambao wametimiza masharti yetu ya kujiunga.

Kwa sababu ya mfumo huu wa kipekee, tunatoa marupurupu ya muda mrefu kwa njia ya asili ili kutimiza wajibu wetu. Watangazaji, watazamaji, watayarishi na washirika wa maudhui hawataki kuhusishwa na maudhui hatari.

Mpango wa Washirika wa YouTube unawawezesha wagombeaji na watayarishi wa maudhui ya siasa

Kupitia Mpango wa Washirika wa YouTube, watayarishi — ikiwa ni pamoja na watayarishi wa maudhui ya habari na ya siasa pamoja na wagombeaji kwenye nyanja zote za siasa — wanaweza kufikia kifurushi bora chenye vipengele na nyenzo za YouTube, zinazowasaidia kufikia watazamaji kwa ufanisi zaidi, kufanya mahusiano ya dhati zaidi na hadhira pamoja na kudumisha na kulinda biashara au mifumo yao. Kifurushi hiki kinajumuisha:

Timu Maalum za Ushirikiano - Wasimamizi Maalum wa Mikakati ya Washirika hufanya kazi kwenye nyaja mbalimbali za siasa ili kuboresha upatikanaji kwenye YouTube, kufikia watazamaji na kuwasiliana na jumuiya yao.

Fursa za Mapato - Vipengele mbadala vya uchumaji wa mapato huwasaidia wagombeaji kudumisha mifumo yao.

Utangazaji wa maudhui ya siasa kwenye YouTube

Tumeweka sera kadhaa tofauti kwa aina tofauti za maudhui kwenye Google na YouTube zinazoweza kuhusiana na utangazaji wa maudhui ya siasa. Tunatekeleza mwongozo huu wote kwa njia sawa bila kujali mtazamo wa siasa kwenye video. Unaweza kupata matangazo ya kisiasa yanayoonyeshwa kwenye Google kupitia Ripoti yetu ya Uwazi kuhusu Matangazo ya Siasa.

Sera za Google Ads na sera za YouTube zinafanya kazi pamoja ili kuhakikisha hali salama na nzuri ya utumiaji kwa watumiaji, watayarishi na watangazaji wanaotumia mifumo yetu

Google imeweka sera kadhaa za kuwezesha mazingira salama ya utangazaji dijitali, ikiwa ni pamoja na maudhui ya siasa. Sera hizi zinasimamia maudhui yanayoonyeshwa katika matangazo kwenye Google, ikiwa ni pamoja na YouTube. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu sera hizi hapa.

Kuchapisha tangazo au maudhui kwenye YouTube kutabaini sera zinazotumika

Kama sehemu ya Google, matangazo yote kwenye YouTube ni sharti yatii Sera za Google za utangazaji. Vilevile, YouTube imeweka sera za uchumaji wa mapato zinazosimamia maudhui ambayo watayarishi wanaweza kutumia kuchuma mapato. Kwa maneno mengine, sera hizi zinasimamia maudhui ambapo matangazo haya yanaweza kuonyeshwa. Mojawapo ya mifano ya maudhui yanayoweza kusababisha hali ya “matangazo machache au hamna matangazo” ni maudhui yanayolenga kuwadhalilisha watu binafsi au kikundi au mashambulizi au maneno ya kumkashifu mtu binafsi.

Sera za kipekee kutoka Google na YouTube zinafanya kazi pamoja ili kuhakikisha hali salama na nzuri kwa watumiaji, watayarishi na watangazaji wetu.

Matangazo kwenye YouTube Maudhui kwenye YouTube
Sera za Google Ads
Mwongozo wa Jumuiya ya YT
Sera za YT za Uchumaji wa Mapato

Zana na Nyenzo

Kutoka Blogu ya YT

Kuhusu uchaguzi wa 2024:

Kuhusu sasisho letu la hivi majuzi la sera ya uadilifu wa uchaguzi:

Kuhusu uchaguzi wa katikati ya muhula wa 2022:

Kuhusu uchaguzi wa 2020: