Nenda kwenye maudhui
Masharti na sera

Hakimiliki

Hakimiliki

Kanuni ya kwanza ya hakimiliki

Watayarishi wanapaswa tu kupakia video ambazo wamezibuni au wameidhinishwa kuzitumia. Hii inamaanisha kuwa hawapaswi kupakia video ambazo hawakubuni, au kutumia maudhui katika video zao ambayo mtu mwingine ana hakimiliki, kama vile nyimbo, vijisehemu vya programu zilizo na hakimiliki au video zilizobuniwa na wengine, bila idhini zinazohitajika.

Ni nini maana ya Hali Zisizofuata Kanuni za Hakimiliki?

Hali zisizofuata kanuni za hakimiliki ni sheria zinazokuruhusu kutumia tena nyenzo zinazolindwa kwa hakimiliki za mtu mwingine bila ruhusa yake, lakini katika hali fulani tu.

Nchini Marekani, hali isiyofuata kanuni za hakimiliki inayotambulika zaidi ni matumizi ya haki. Wakati wa kufanya maamuzi kuhusu iwapo matumizi ni ya haki, mahakama huangalia vigezo vinne: madhumuni na aina ya matumizi, hali ya kazi iliyo na hakimiliki, kiasi na umuhimu wa sehemu inayotumiwa ikilinganishwa na kazi iliyo na hakimiliki kwa ujumla; na athari ya matumizi kwenye soko tarajiwa au thamani ya kazi iliyo na hakimiliki. Baadhi ya shughuli ambazo zinaweza kutimiza masharti ya kuwa matumizi ya haki ni pamoja na kukosoa, kutoa maoni na kuripoti habari. Matumizi ya haki yanalenga kukuza uhuru wa kujieleza.

Katika baadhi ya nchi zenye sheria za kiraia, zikiwemo nchi nyingi katika Umoja wa Ulaya, hali zisizofuata sheria zinazodhibitiwa zaidi zinatambuliwa ambapo utumiaji tena wa maudhui lazima uwe katika aina mahususi, badala ya kuwa na vipengele vinavyopimwa. Aina zilizobainishwa katika Kifungu cha 17 cha agizo la hakimiliki la Soko Moja la Dijitali la Umoja wa Ulaya ni manukuu, kukosoa, kutoa maoni, ucheshi, kubeza na kuiga kazi ya wengine. Maneno haya yana maana yake ya kawaida katika lugha ya kila siku, lakini pia hupitishwa kuwa sheria na kila nchi mwanachama na kufasiriwa na mahakama za kitaifa na Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya (CJEU). Pia ni muhimu kuzingatia muktadha wa matumizi na madhumuni ya hali hizo zisizofuata kanuni za hakimiliki, mojawapo ikiwa ni kusawazisha uhuru wa watayarishi wa kujieleza na hakimiliki za wenye haki.

Katika baadhi ya nchi, kama vile Kanada, Uingereza na Australia, dhana ya mseto ya matumizi yasiyo ya biashara ipo. Mahakama hupima vigezo sawa na vilivyo katika matumizi ya haki, lakini utumiaji tena lazima uwekwe katika aina mahususi. Aina hizi ni pamoja na manukuu (manukuu ya jumla na manukuu kwa madhumuni ya kukosoa, kutoa maoni, au kuripoti habari), ucheshi, kubeza na kuiga kazi ya wengine.

Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa kimataifa unaojulikana kama Mkataba wa Berne, ambao unaruhusu utumiaji tena katika aina mahususi, ikiwa ni pamoja na manukuu na kuripoti habari.

Ingawa kuna ulinganifu katika hali zisizofuata kanuni za hakimiliki kote ulimwenguni, bado kuna tofauti kubwa kati ya sheria za kila nchi. Hakuna jibu moja mwafaka kuhusu ikiwa utumiaji tena unajumuishwa katika hali zisizofuata kanuni za hakimiliki na mahakama hufanya maamuzi ya utekelezaji wa hali hizo zisizofuata kanuni kwa njia mahususi.

Katika YouTube, dhamira yetu ni kumpa kila mtu fursa ya kujieleza na kuonyesha wote matukio ya ulimwengu. Hali zisizofuata kanuni za hakimiliki huwa na jukumu muhimu katika kuendeleza dhamira hii kwa kuhimiza mtiririko huru wa mawazo na ubunifu. Kwa hivyo, tunawaomba wenye haki kuzingatia utekelezaji wa hali zisizofuata kanuni za hakimiliki kabla ya kuwasilisha maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Tunaamini kuwa hii italeta usawa kati ya kuheshimu hakimiliki ya wenye haki na uhuru wa watayarishi wa kujieleza ambao unaweza kulindwa na hali zisizofuata kanuni za hakimiliki.

Pia, tunabuni bidhaa zinazowawezesha watayarishi kufikia, kutunga na kushiriki maelezo kwa njia ya kipekee. Tumebuni Maktaba ya Sauti ili ugundue muziki wa ubora wa juu na athari za sauti bila malipo, ambazo unaweza kutumia tena kwa usalama. Sasa kwa kutumia Video Fupi za YouTube, unaweza kubuni video fupi kwa kuiga maudhui ya mtu mwingine, mradi akupe ruhusa ya kufanya hivyo. Pia, tunaendelea kubuni na kupanua Muziki wa Watayarishi, ambao huwaruhusu watayarishi katika mpango wa Washirika wa YouTube kutumia kwa usalama muziki wa biashara kwa kutoa leseni za nyimbo au kushiriki mapato yao ya video na wenye hakimiliki za muziki.

Walio na haki wanaweza kutuma vipi madai ya hakimiliki?

Kila mtu anaweza kufikia Zana za Kudhibiti Hakimiliki kwenye YouTube, zinazowapa wenye hakimiliki udhibiti wa maudhui yao yaliyo na hakimiliki kwenye YouTube. Tunafanya kazi na wenye hakimiliki ili kuwawezesha kutambua vipengele vinavyowafaa kulingana na kiwango cha maudhui yao yenye hakimiliki kwenye YouTube na nyenzo ambazo wameweka kudhibiti maudhui yao mtandaoni kwa kuwajibika. Kifurushi chetu cha Kudhibiti Hakimiliki kinatoa njia kadhaa ambazo wenye hakimiliki wanaweza kutuma madai ya hakimiliki.

Fomu ya wavuti

Njia rahisi zaidi ya kuondoa nakala ambazo hazijaidhinishwa za maudhui yaliyo na hakimiliki ni kwa kutuma mwenyewe arifa ya hakimiliki kupitia fomu ya wavuti ya DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali). Zana hii ni bora zaidi kwa watumiaji wengi - inaweza kutumiwa na kila mtu na inapatikana katika kila lugha.

Copyright Match Tool

Copyright Match Tool hutumia uwezo wa teknolojia ya Ulinganishaji wa Content ID ili kupata video zilizopakiwa upya kwenye YouTube. Inapatikana kwa zaidi ya vituo 1,500,000, inatambua karibu nakala kamili za video halisi za Mtayarishi zinapopakiwa kwenye vituo vingine vya YouTube na huruhusu Mtayarishi kuchagua hatua ya kuchukua: anaweza kuomba kuondolewa kwa video, kutuma ujumbe kwa mpakiaji wa video au kuweka tu video inayolingana kwenye kumbukumbu iwapo hangependa kuchukua hatua yoyote. Mtumiaji yeyote aliye na historia ya kuondoa video kwa mujibu ya DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali) kupitia fomu yetu ya wavuti anaweza kutuma ombi la ufikiaji kwa kutumia fomu yetu ya umma.

Content ID

Content ID ni suluhisho letu kwa walio na mahitaji magumu ya udhibiti wa haki. Ni mfumo wetu dijitali wa alama bainifu unaoruhusu wenye hakimiliki kupakia maudhui ambayo wana haki zake za kipekee kama vile faili za marejeleo, kisha huchanganua video zilizopakiwa kwenye YouTube ili kutafuta nakala ya maudhui hayo. Mtumiaji anapopakia maudhui, Content ID huchanganua kwa kulinganisha na hifadhidata ya video zinazolingana. Iwapo nakala ya video inapatikana, basi hatua huchukuliwa kulingana na sheria au sera zilizobainishwa mapema ambazo mmiliki wa maudhui anaweka mwenyewe:

  • Kuzuia video yote isitazamwe. Watayarishi huwa hawapokei onyo la hakimiliki iwapo mmiliki wa maudhui anazuia video.
  • Kuchuma mapato kwenye video kwa kuonyesha matangazo; katika hali nyingine, kugawana mapato na aliyepakia.
  • Kufuatilia takwimu za watazamaji wa video.

Katika hali nyingi, hii inamaanisha kuwa wenye hakimiliki hawahitaji kutuma ombi la kuondoa video hizi kutokana na ukiukaji wa hakimiliki na badala yake wana fursa ya kuchuma mapato na kuonyesha matangazo ili kuendelea kuonyesha video.

YouTube huchukua hatua gani kutokana na ukiukaji wa hakimiliki?

Iwapo mwenye hakimiliki anatuma malalamiko halali ya DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali) kupitia fomu yetu ya wavuti, tunaondoa video hiyo na kuweka onyo la hakimiliki. Mtumiaji akipata maonyo matatu ya hakimiliki ndani ya siku 90, tutafunga akaunti yake pamoja na vituo vyovyote vilivyounganishwa. Pia, tuna zana za kusaidia Watayarishi kusuluhisha maonyo yao ya hakimiliki - ikiwa ni pamoja na kusubiri muda wake uishe baada ya siku 90, kuomba dai la hakimiliki liondolewe au kutuma arifa ya kukanusha.

Content ID hufanya kazi kwa njia tofauti. Iwapo video mpya inayopakiwa italingana na nakala ya faili ya marejeleo, "dai" hutumwa. Kulingana na mapendeleo yaliyochaguliwa na mmiliki wa Content ID, tutatekeleza sera ili kufuatilia, kuchuma mapato au kuzuia, lakini hatutatoa onyo la hakimiliki.