Nenda kwenye maudhui
Kanuni na sera

Sera za Uchumaji wa Mapato

Sera za uchumaji wa mapato

Kukubaliwa katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) ni mafanikio makuu katika harakati za Mtayarishi yoyote. Kama sehemu ya Mpango wa Washirika wa YouTube, Watayarishi wanaweza kuacha kuchuma mapato kwenye maudhui yao, kupokea usaidizi kupitia barua pepe na gumzo na kufikia Copyright Match Tool ili kusaidia kulinda maudhui yao.

Masharti muhimu ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube ni kufuata Sera za uchumaji wa mapato kwenye YouTube, zinazojumuisha Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube, Sheria na Masharti na Sera za mpango wa Google AdSense. Sera hizi hutumika kwenye kituo cha Mtayarishi kikamilifu, wala si tu video mahususi.

Kuweka kiwango cha juu cha uchumaji wa mapato

Kwa miaka michache iliyopita, YouTube imechukua hatua kuboresha masharti ya uchumaji wa mapato ili wanaotuma taka, waigaji na watendaji wengine wabaya wasiweze kudhuru mfumo au kunyanyasa Watayarishi wazuri wanaotoa maudhui yenye ubora wa juu.

Ili kutuma ombi la kuwa katika Mpango wa Washirika wa YouTube, lazima vituo vitimize masharti ya kujiunga yanayohusiana na muda wa kutazama na kufuatilia vituo. Kutokana na kutekelezwa, timu ya ukaguzi ya YouTube huhakikisha kituo hakijakiuka sera za uchumaji wa mapato, za maudhui na za hakimiliki kwenye YouTube. Tutaruhusu tu vituo vinavyotimiza masharti haya ya kujiunga na kufuata mwongozo wetu wote kwenye mpango, hali inayovipa uwezo wa kuonyesha matangazo na kupata bidhaa nyingine za uchumaji wa mapato.

Mwongozo wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji

Mtayarishi akiwa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, haimaanishi kuwa video zote zilizo kwenye kituo chake zitatimiza masharti ya kuonyesha matangazo. Lazima kila video itii Mwongozo wetu wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji. Huu ni utaratibu wetu, kwa vile tunaelewa kuwa kuna mazungumzo muhimu ambayo yana nafasi kwenye YouTube, kama vile mjadala wa afya ya akili au matukio nyeti ya dunia, ambayo huenda yasifae chapa kulingana na watangazaji. Mifano mingine ya maudhui ambayo hayafai matangazo ni pamoja na aina fulani za lugha isiyofaa, vurugu, maudhui ya watu wazima au vitendo hatari.

Ili kuwasaidia Watayarishi waelewe video kwenye vituo vyao ambazo zinafaa matangazo, tumeshirikiana kwa karibu na watangazaji ili kubuni Mwongozo wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji, mwongozo huo ni dhahiri na wa kina. Watayarishi wanaotimiza masharti pia wana uwezo wa kutathmini wenyewe maudhui yao kulingana na mwongozo huu na kuwasha uchumaji wa mapato kupitia matangazo kwenye video mahususi katika kituo chao.

YouTube huchukua hatua gani dhidi ya video ambazo hazitii Mwongozo wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji?

Iwapo Mtayarishi amewasha uchumaji wa mapato kupitia matangazo katika video lakini wakaguzi na mifumo yetu ya kiotomatiki itambue kuwa video haitii Mwongozo wetu wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji, video hiyo itakuwa na matangazo machache au ikose matangazo yanayoonyeshwa. Hata hivyo, iwapo Watayarishi wanaamini kuwa bado video yao inafaa chapa zote, wanaweza [kuomba ikaguliwe na mtu](https://support.google.com/youtube/answer/7083671.