Nenda kwenye maudhui
Vipengele vya bidhaa

Maonyesho ya Kwanza na Mitiririko ya Moja kwa Moja kwenye YouTube

YouTube Moja kwa Moja

Kila siku, watu kutoka duniani kote hutembelea YouTube ili kufurahia matukio makubwa zaidi ya utamaduni duniani. Iwe ni kuandaa tukio la moja kwa moja, mijadala ya kisiasa au mkutano wa wanahabari kuhusu habari zinazojiri, YouTube Moja kwa Moja na Maonyesho ya Kwanza, huruhusu Watayarishi kuleta watazamaji pamoja katika muda halisi ili kujifunza, kujadili na kubuni jumuiya mpya kwenye jamii.

YouTube Moja kwa Moja ni njia rahisi kwa Watayarishi kufikia jumuiya zao katika muda halisi. Iwe unatiririsha tukio, unafunza darasa au unaandaa warsha, YouTube ina zana zitakazosaidia udhibiti mitiririko ya moja kwa moja na uwasiliane na watazamaji katika muda halisi.

Watayarishi wanaweza kutiririsha moja kwa moja kwenye YouTube kupitia kamera ya wavuti, kifaa cha mkononi na kutiririsha kupitia programu ya kusimba. Kamera ya wavuti na kifaa cha mkononi huchukuliwa kuwa chaguo bora kwa wanaoanza na huruhusu Watayarishi kutiririsha moja kwa moja kwa haraka. Kutiririsha kupitia programu ya kusimba ni njia bora zaidi kwa mitiririko ya moja kwa moja ya kina kama vile: kushiriki skrini ya mtayarishi au kuonyesha uchezaji wako, kuunganisha kwenye vifaa vya nje vya sauti na video na kudhibiti utayarishaji wa mitiririko ya moja kwa moja ya kina (kama vile kamera na maikrofoni nyingi).

Ili upate mwongozo wa hatua kwa hatua, pakua Mwongozo wa Matukio Dijitali katika lugha yako.

Maonyesho ya kwanza huruhusu Watayarishi na hadhira yao kutazama na kufurahia video mpya pamoja, jinsi ilivyo kwenye filamu au onyesho la kwanza la kipindi cha televisheni. Maonyesho ya kwanza huruhusu Watayarishi kuratibu upakiaji wa video na kubuni ukurasa wa kutazama wa umma unaoweza kushirikiwa kabla ya onyesho la kwanza.

Maonyesho ya Kwanza: Baada ya onyesho la kwanza kuratibiwa, ukurasa wa umma wa kutazama na unaoweza kushirikiwa hubuniwa, jambo linalowaruhusu watayarishi, wasanii, wachapishaji na hadhira yao kutazama na kugundua video mpya pamoja.

Kudhibiti gumzo la moja kwa moja la kituo hufanya jumuiya yetu ya YouTube iridhishe na iwe bora zaidi. YouTube hutoa zana za kudhibiti gumzo la moja kwa moja ili kusaidia kuzuia unyanyasaji na kufanya kila mtu ahisi salama. Baadhi ya zana hizi zinajumuisha: kuweka wanaodhibiti, orodha ya maneno yanayozuiliwa, kuzuilia gumzo zisizofaa ili zikaguliwe, hali ya polepole na kuzima Gumzo la Moja kwa Moja. Kabla ya kuanza mtiririko wa moja kwa moja au kuonyesha Onyesho la Kwanza kwenye YouTube, tunahimiza kila mtu afahamu zana zetu za kudhibiti na Mwongozo wa Jumuiya ili kufanya gumzo la moja kwa moja liwe bora kwa watazamaji.

Kwa Watayarishi ambao huchuma mapato kwenye mitiririko ya moja kwa moja au Maonyesho ya Kwanza, kituo chao kinahitaji kusajiliwa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP). Watayarishi wana njia kadhaa za kupata pesa kutokana na mitiririko ya moja kwa moja na Maonyesho ya kwanza: Matangazo, Super Chat na Super Stickers na Uanachama katika Kituo.

*Upatikanaji wa vipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwa nchi zaidi.

Eneo letu la kuvinjari YouTube Moja kwa Moja ni mahali ambapo watazamaji wanaweza kupata matukio yanayosisimua zaidi ya moja kwa moja yanayofanyika kwenye YouTube wakati wowote. Watazamaji pia wanaweza kufuatilia vituo wanavyopenda vinavyotiririsha moja kwa moja kwenye YouTube ili waarifiwe kuhusu Maonyesho ya Kwanza na mitiririko ijayo ya moja kwa moja.

Gundua YouTube Moja kwa Moja: Eneo la Moja kwa Moja huwapa watumiaji uwezo wa kufikia mitiririko ya moja kwa moja kwa aina maarufu za maudhui kama vile Michezo, Muziki, Mitindo na Urembo, Mafunzo na zaidi – haya yote katika eneo moja.