Nenda kwenye maudhui
Vipengele vya bidhaa

Uchumaji wa Mapato kwa Watayarishi

Uchumaji wa Mapato kwa Watayarishi

Watayarishi wa YouTube ni watu wanaozalisha maudhui kwenye mfumo. Huu ni muundo mahususi unaowawezesha Watayarishi kupata pesa moja kwa moja kwenye mfumo wetu kwa njia nyingi tofauti, ikiwa ni pamoja na matangazo, mauzo ya bidhaa na ufuatiliaji wa vituo.

Matangazo

Matangazo ndiyo njia kuu ambayo Watayarishi wanaweza kutumia kupata pesa kwenye YouTube. Mapato ya matangazo huzalishwa wakati watu wanatazama matangazo yanayoonyeshwa kwenye video. Mapato haya yanayotokana na matangazo yanagawanywa kati ya YouTube na Mtayarishi - hali inayowezesha Watayarishi kunufaika moja kwa moja kwa kazi zao.

Lazima kwanza watayarishi watimize masharti ya kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) ili waweze kupata pesa kutokana na matangazo kwenye video zao na mitiririko ya moja kwa moja. Katika kutekeleza ahadi yetu ya uwajibikaji, tunachukulia uchumaji wa mapato kama fursa na kuwatuza tu Watayarishi wanaoaminika.

Vyanzo mbadala vya uchumaji wa mapato

Katika miaka michache iliyopita, tumezindua vyanzo kadhaa mbadala vya mapato mbali na matangazo ili kusaidia Watayarishi wanaotimiza masharti kuchuma mapato kutokana na maudhui yao wanapowasiliana na watazamaji. Kama ilivyo katika matangazo, Watayarishi na YouTube hugawana mapato yanayotokana na bidhaa hizi.

Uanachama katika kituo

Mashabiki wanaweza kujiunga kwenye kituo cha Watayarishi kupitia malipo yanayorudiwa kila mwezi na kupata uwezo wa kufikia manufaa ya wanachama pekee kama vile beji, emoji maalum na maudhui ya kipekee.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza katika nchi zaidi.

Uanachama katika Vituo

Super Chat na Super Stickers

Mashabiki wanaweza kununua na kutuma ujumbe wa vibandiko dijitali au SMS ili kuangazia ujumbe wao wa gumzo la moja kwa moja na kuwasiliana na Watayarishi wanaowapenda.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza katika nchi zaidi.

Super Chat na Super Stickers

Ununuzi kwenye YouTube

Uza bidhaa zako moja kwa moja kwa mashabiki wako. Unganisha duka lako na utaweza kuonyesha bidhaa zako kwenye rafu iliyo chini ya video na mitiririko yako mubashara. Pamoja na hayo, kichupo cha “Duka” kitafunguka kwenye kituo chako -- ambacho ni kama sehemu ya mbele ya duka lako mwenyewe kwenye YouTube.

*Inategemea masharti ya kujiunga.

Usajili

YouTube pia hupata pesa kutoka kwa biashara za usajili wa kulipiwa kila mwezi kama vile YouTube Premium. Kupitia YouTube Premium, wanachama wanaweza kufurahia video yoyote kwenye YouTube bila matangazo huku wakiendelea kuwasaidia watayarishi. Kwa sasa, mapato kutoka ada za uanachama wa YouTube Premium husambazwa kwa Watayarishi wa video katika Mpango wa Washirika wa YouTube kulingana na kiasi cha maudhui kinachotazamwa na wanachama.