Nenda kwenye maudhui
Vipengele vya bidhaa

Habari na taarifa za kuaminika

Habari na taarifa

Kuna nyakati ambazo unakuja kwenye YouTube ili kupata habari mpya au kupata tu maelezo zaidi kuhusu mada unazopenda. Kwa maudhui ambapo usahihi na kuaminika ni muhimu, ikiwa ni pamoja na habari, siasa, matibabu na maelezo ya kisayansi, tunatumia mifumo ya mashine kujifunza inayoyapa kipaumbele maelezo kutoka vyanzo vya kuaminika na kutoa muktadha ili kukusaidia kufanya maamuzi bora.

Kukuza sauti za kuaminika

Kuna ishara nyingi - kama vile ufaafu na umaarufu - ambazo kwa kawaida ni muhimu wakati mifumo yetu inabaini video za kuonyesha unapotafuta maudhui. Hata hivyo, katika habari na taarifa, tunajua kuwa kuaminika ni muhimu. Ndiyo maana tumejitahidi kusaidia watumiaji hawa kugundua vyanzo vya kuaminika katika habari na maelezo kwenye mfumo wetu.

Habari Zinazojiri

Wakati tukio kuu la habari zinazojiri linafanyika katika nchi uliko, tunataka kuhakikisha kuwa unafahamu na unaweza kufikia taarifa za kuaminika kwa urahisi. Katika hali hizo rafu ya Habari Zinazojiri huonekana moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa kwanza. Rafu hii huangazia video zinazofaa kutoka vyanzo vya habari vinavyoaminika kuhusu matukio ya habari ya umuhimu wa kitaifa.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwenye nchi zaidi.

Rafu ya Habari Zinazojiri kwenye ukurasa wa kwanza wakati wa matukio makuu ya habari zinazojiri

YouTube hubaini vipi habari zinazojiri?

Unaweza kuona video za Habari Zinazojiri kwenye ukurasa wa kwanza kwa matukio kama vile mikasa mikubwa, majanga ya kiasili na matukio ya muda katika siasa za kitaifa na za kimataifa. Ili kuangazia habari zinazojiri zinazofaa katika nchi uliko, tunategemea Google News kufahamu kinachoendelea duniani na wakati taarifa za habari zinatokea.

Habari Kuu

Unapotafuta mada zinazohusiana na habari, mara nyingi utaona sehemu ya Habari Kuu karibu na sehemu ya juu ya matokeo ya utafutaji, inayoibua matokeo yanayofaa kutoka vyanzo vya kuaminika kama vile CNN na Fox News. Rafu ya Habari Kuu kwenye ukurasa wa kwanza pia inaweza kuonekana ukitazama au kutafuta maudhui ya habari. Rafu ya Habari Kuu itaonekana bila kujali umri na itajumuisha maudhui yanayofaa kutoka vyanzo vya habari vinavyofuata sera za maudhui za Google News.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwenye nchi zaidi.

Rafu ya Habari Kuu: huonyesha matokeo yanayofaa kutoka vyanzo vya kuaminika katika matokeo ya utafutaji

Kukuza vyanzo vya kuaminika

Tunakuza vyanzo vya kuaminika vya matukio ya habari katika matokeo ya utafutaji na vidirisha vya "Inayofuata". Mbali na matukio ya sasa, kuaminika pia ni muhimu katika mada ambazo ni rahisi kuwa na maelezo ya kupotosha, kama vile chanjo. Katika hali hizi, tunalenga kuonyesha video kutoka kwa wataalamu, kama vile taasisi za afya ya umma, katika matokeo ya utafutaji.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwenye nchi zaidi.

Vyanzo vya kuaminika vya matukio ya habari hupewa kipaumbele katika matokeo ya utafutaji na vidirisha vya "Inayofuata”

Kukupa muktadha ili kukusaidia kufanya maamuzi ya busara

Muktadha ni muhimu wakati wa kutathmini taarifa, kwa hivyo tunakupa muktadha pamoja na matokeo fulani ya utafutaji na video ili kukusaidia kufanya maamuzi yako mwenyewe kuhusu maudhui unayopata kwenye YouTube. Ili kufanya hili, tunaangazia maelezo ya maandishi kuhusu mada, matukio na wachapishaji fulani kutoka vyanzo vingine kwa kutumia vidirisha vya taarifa kwenye YouTube.

Habari Zinazochipuka

Katika hali za habari zinazochipuka, wakati video za ubora wa juu hazipatikani mara moja, tunaonyesha viungo vya makala ya habari katika maandishi kutoka vyanzo vya kuaminika kwenye matokeo ya utafutaji ya YouTube. Pia tunatoa kikumbusho kuwa habari zinazochipuka zinaweza kubadilika kwa haraka. Tunategemea ishara za Google News ili kuonyesha hili.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwenye nchi zaidi.

Vidirisha vya taarifa za habari zinazojiri huunganisha kwenye makala ya habari pamoja na matokeo ya utafutaji wakati wa habari zinazojiri

Kuhakikisha ukweli

Vidirisha vyetu vya maelezo ya kuhakikisha ukweli hutoa muktadha wa ziada kwa kuangazia makala mengine yanayofaa yaliyohakikishwa ukweli, juu ya matokeo ya utafutaji kwa hoja zinazofaa, ili uweze kufanya uamuzi bora kuhusu madai katika habari.

Kuna vigezo vingi vya kubaini iwapo kidirisha cha taarifa ya kuhakikisha ukweli kitaonekana kwenye utafutaji wowote ule. Muhimu zaidi, lazima kuwe na makala ya kuhakikisha ukweli yanayopatikana kutoka kwa mchapishaji anayetimiza masharti. Na ili kulinganisha mahitaji yako na taarifa tunayotoa, makala ya kuhakikisha ukweli yataonekana unapotafuta dai mahususi. Kwa mfano, ukitafuta "je, kimbunga kilipiga jiji la Dar es Salaam," unaweza kuona makala yanayofaa ya kuhakikisha ukweli, lakini ukitafuta hoja ya jumla zaidi kama "kimbunga", huenda usiyaone.

Vidirisha vyetu vya taarifa ya kuhakikisha ukweli vinategemea mtandao wazi wa wachapishaji wengine na hutumia ClaimReview mfumo wa kuweka lebo. Wachapishaji wote wanaweza kushiriki mradi wafuate [mwongozo wa data] unaopatikana hadharani wa ClaimReview (https://developers.google.com/search/docs/guides/sd-policies), na wawe sehemu ya Mtandao wa Kimataifa wa Kuhakikisha Ukweli au wawe wameainishwa kama wachapishaji wanaoaminika.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwenye nchi zaidi.

Kuhakikisha ukweli: madai yaliyohakikishwa ukweli hivi majuzi huonekana pamoja na matokeo ya utafutaji

Mada zilizo rahisi kuwa na maelezo ya kupotosha

Kwa mada za historia na sayansi ambazo ni rahisi kuwa na maelezo ya kupotosha, kama vile “Apollo 11,” makala ya jumla ya marejeleo yanayounganisha kwenye vyanzo vingine huonekana pamoja na video na matokeo ya utafutaji yanayohusiana ili kutoa muktadha zaidi. Tunafanya hili kwa kuonyesha taarifa ya muktadha kutoka vyanzo vingine ikiwa ni pamoja na Encyclopedia Britannica na Wikipedia pamoja na video na matokeo ya utafutaji. Tumeanza na kundi dogo la mada kulingana na vyanzo vya wengine tunapofanyia majaribio na kuendelea kusambaza kipengele hiki.

Vidirisha vya taarifa kulingana na mada huangazia makala ya marejeleo ya jumla pamoja na matokeo ya utafutaji kwenye mada zinazoweza kuwa na maelezo ya kupotosha

Kwa utafutaji unaohusiana na COVID-19 au taarifa kuhusu chanjo ya COVID-19, unaweza kuona vidirisha vya taarifa kwenye YouTube vinavyoangazia viungo vya kukuongoza kwenye Shirika la Afya Duniani ili upate maelezo zaidi. Katika baadhi ya maeneo, utaona taarifa kuhusu COVID-19 katika lugha za eneo husika zikielekeza kwenye vyanzo vya eneo, kama vile wizara za afya na vituo vya kudhibiti magonjwa. Kidirisha kitaonekana kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube, katika matokeo ya utafutaji wa hoja zinazohusiana na COVID-19, pia kwenye ukurasa wa kutazama katika video zinazohusiana na COVID-19. Vidirisha hivi vinanuiwa kukusaidia upate taarifa za kuaminika kuhusu COVID-19 au chanjo ya COVID-19 kutoka kwenye vyanzo vingine na si uamuzi kuhusu usahihi wa video yoyote.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwenye nchi zaidi.

Kidirisha cha taarifa kuhusu COVID-19 huunganisha kwenye Shirika la Afya Duniani, au mamlaka za afya katika eneo ulimo ili upate maelezo zaidi kuhusu COVID-19 au taarifa kuhusu chanjo za COVID-19

Ufadhili wa wachapishaji

Kwa kuwa ufahamu kuhusu vyanzo vya ufadhili unaweza kutoa muktadha wakati wa kukagua historia ya shirika na kukusaidia kuelewa zaidi kama mtazamaji, tunaonyesha ufadhili wa serikali au wa umma unaotolewa kwa wachapishaji wa habari kupitia vidirisha vya taarifa pamoja na video zao. Tunatoa vidirisha vya taarifa kuhusu ufadhili wa mchapishaji kwenye zaidi ya vituo elfu moja.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwenye nchi zaidi.

Vidirisha vya taarifa za ufadhili wa wachapishaji huonyesha ufadhili wa Serikali au umma kwa mashirika ya kuchapisha habari

Afya

Unapotafuta kwenye YouTube kuhusu mada zinazohusiana na afya, kama vile COVID-19, unaweza kuona vidirisha vya taarifa kwenye YouTube vinavyoonyesha taarifa ya afya kutoka vyanzo vinavyoaminika, kama vile Shirika la Afya Duniani na wizara nyingine za afya. Vidirisha hivi vya taarifa vinajumuisha taarifa huru za wengine, kama vile dalili, matibabu na uzuiaji. Unaweza pia kwenda kwenye tovuti ya wengine ili upate maelezo zaidi. Katika baadhi ya nchi au maeneo, unaweza kuona viungo vinavyoelekeza kwenye njia za kimatibabu zilizothibitishwa za kujichunguza kutoka kwa mamlaka za afya katika eneo. Kulingana na majibu ya kujichunguza, utapata maelezo zaidi kuhusu aina za usaidizi au huduma za matibabu ambazo zinaweza kukufaa.

*Upatikanaji wa kipengele hutofautiana kulingana na nchi na tunajitahidi kusambaza kwenye nchi zaidi.

*Maelezo yanayohusiana na afya kwenye YouTube hayafai kutumiwa na kila mtu na si ushauri wa kimatibabu. Iwapo una tatizo la kimatibabu, hakikisha unawasiliana na mtoa huduma za matibabu. Iwapo una dharura ya kimatibabu, wasiliana na daktari wako au upige nambari ya dharura mahali uliko.

Vidirisha vya taarifa za afya huonyesha taarifa za kina kuhusu afya kutoka kwa vyanzo vya kuaminika, kama vile wizara za afya