Nenda kwenye maudhui
Vipengele vya bidhaa

Video zinazopendekezwa

Video zinazopendekezwa

Muhtasari

Mapendekezo hukusaidia ugundue video nyingi unazopenda, iwe ni mapishi mapya unayojaribu au wimbo mtamu unaofuata. Mafanikio ya mapendekezo ya YouTube yanategemea kutabiri kwa usahihi video ambazo ungependa kutazama. Wakati mapendekezo yetu ni bora zaidi, yanaunganisha mabilioni ya watu kote duniani na maudhui ambayo yanahamasisha, kufahamisha na kuburudisha kwa njia ya kipekee.

Unaweza kupata mapendekezo katika sehemu mbili kuu: ukurasa wako wa kwanza na kidirisha cha “Inayofuata”.

  • Ukurasa wa kwanza: Ukurasa wako wa kwanza ni sehemu unayoiona unapofungua YouTube mara ya kwanza, huonyesha mseto wa mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo, vituo unavyofuatilia, taarifa na habari mpya.

  • Inayofuata: Kidirisha cha 'Inayofuata' huonekana unapotazama video. Hupendekeza maudhui ya ziada kulingana na unachotazama sasa, pamoja na video nyingine ambazo tunafikiri huenda zikakuvutia.

Je, mfumo wa mapendekezo kwenye YouTube unafanyaje kazi?

Tunaanza kwa kufahamu kuwa kila mtu ana mazoea ya kipekee ya utazamaji. Kisha mfumo wetu hulinganisha mazoea yako ya utazamaji na yale yanayolingana nayo na hutumia maelezo hayo kupendekeza maudhui mengine ambayo huenda ungependa kutazama.

Mfumo wetu wa mapendekezo unaendelea kubadilika, kwa kujifunza kila siku kutokana na zaidi ya vipengee bilioni 80 vya maelezo tunavyoviita ishara:, vya msingi vikiwa:

  • Historia ya video ulizotazama: Mfumo wetu hutumia video za YouTube unazotazama ili kukupa mapendekezo bora zaidi, kukumbuka ulikoachia na mengine mengi.

  • Historia ya mambo uliyotafuta: Mfumo wetu hutumia mambo unayotafuta kwenye YouTube ili kuathiri mapendekezo ya siku zijazo.

  • Vituo unavyofuatilia: Mfumo wetu hutumia maelezo kuhusu vituo vya YouTube unavyofuatilia ili kupendekeza video zingine ambazo huenda ukazipenda.

  • Alama za imenipendeza: Mfumo wetu hutumia maelezo yako ya alama za imenipendeza kujaribu kutabiri uwezekano kwamba utavutiwa na video kama hizi katika siku zijazo.

  • Alama za haijanipendeza: Mfumo wetu hutumia video ulizowekea alama ya haijanipendeza ili kuamua ni maudhui gani ya kuzuia kupendekeza katika siku zijazo.

  • Chaguo za maoni za "Sijavutiwa": Mfumo wetu hutumia video unazotia alama ya "Sijavutiwa" ili kuamua ni maudhui gani ya kuzuia kupendekeza katika siku zijazo.

  • Chaguo za maoni za “Usipendekeze kituo”: Mfumo wetu unatumia chaguo zako za maoni za “Usipendekeze kituo” kama ishara kwamba huenda maudhui ya kituo si kitu ambacho ulifurahia kutazama.

  • Tafiti za kubainisha kiwango cha kuridhika cha watumiaji: Mfumo wetu hutumia tafiti za watumiaji ambazo zinakuomba ukadirie video ulizotazama, jambo ambalo husaidia mfumo kuelewa kiwango cha kuridhika, si tu muda wa kutazama.

Vipengele tofauti vya YouTube hutegemea ishara fulani za mapendekezo kuliko vingine. Kwa mfano, tunatumia video unayotazama kwa sasa kama ishara kuu tunapopendekeza video ya kucheza inayofuata. Ili kutoa mapendekezo ya video kwenye ukurasa wa kwanza, tunategemea historia yako ya video ulizotazama. Unaweza kuzima na kufuta historia yako ya video ulizotazama ikiwa hupendi tukikupa mapendekezo ya video kwenye ukurasa wa kwanza.

Kwa watu waliozima kipengele cha historia ya video ulizotazama kwenye YouTube na wasio na historia ya kutosha ya video ulizotazama hapo awali, ukurasa wa kwanza utaendelea kuonyesha upau wa kutafutia na menyu ya upande wa kushoto ya Mwongozo. Hii inaruhusu hali ya utumiaji iliyoboreshwa inayokupa uwezo wa kutafuta, kuvinjari vituo unavyofuatilia na kupata video zinazovuma katika menyu ya kipengele cha Gundua, ambayo inatoa kurasa lengwa kwa kategoria maarufu na watayarishi chipukizi na wasanii wanaochipuka.

Mapendekezo ya YouTube husaidia vipi kudumisha mfumo unaowajibika?

Mapendekezo huchangia pakubwa katika jinsi tunavyodumisha mfumo unaowajibika. Hukuunganisha kwenye maelezo muhimu, unaokufikia kwa wakati unaofaa na wenye ubora wa juu na wakati huo huo huchangia katika kazi inayofanywa na Mwongozo wetu wa Jumuiya, ambao hubainisha mambo yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

Tunachukua hatua ya ziada ya kupendekeza video za kuaminika kwa watazamaji kuhusu mada kama vile habari, siasa, matibabu na maelezo ya kisayansi.

Tunategemea wakaguzi, waliopewa mafunzo kwa kutumia mwongozo unaopatikana hadharani, ambao hukagua ubora wa maelezo katika kila kituo na video. Ili kuamua iwapo video ni ya kuaminika, wakaguzi huangalia vigezo kama vile utaalamu na sifa ya anayezungumza au kituo, mada kuu ya video, na iwapo maudhui yanatimiza ahadi yake au kutimiza lengo lake. Kadri video inavyoaminika, ndivyo itakavyotangazwa katika mapendekezo.

Vidhibiti vya kufanya mapendekezo yakufae zaidi

Mfumo wetu hupitia mabilioni ya video ili kupendekeza maudhui yanayofaa mambo yanayokuvutia. Hata hivyo, tunajua kuwa si kila mtu angependa kushiriki maelezo haya nasi kila wakati. Kwa hivyo tumebuni vidhibiti vya kukusaidia kuamua kiasi cha data ambacho ungependa kutoa.

Unaweza kusitisha, kubadilisha au kufuta historia yako ya mambo uliyotafuta na video ulizotazama kwenye YouTube wakati wowote. Pia tunakupa njia za kuwasiliana nasi tunapokupendekezea maudhui ambayo hayakuvutii. Kwa mfano, vitufe kwenye ukurasa wa kwanza na kwenye sehemu ya "Inayofuata" vinakuruhusu kuchuja na kuchagua mapendekezo kulingana na mada mahususi. Unaweza pia kubofya kitufe cha “sivutiwi” ili uipe YouTube ishara kuwa hungependa kutazama video au kituo fulani kwa wakati huo.

Na ikiwa hutaki kuona mapendekezo kwenye ukurasa wa kwanza, unaweza kuzima na kufuta historia yako ya video ulizotazama kwenye YouTube. Kwa watumiaji waliozima kipengele cha historia ya video ulizotazama kwenye YouTube na wasio na historia ya kutosha ya video ulizotazama, ukurasa wa kwanza utaonyesha upau wa utafutaji na menyu ya upande wa kushoto ya Mwongozo, bila mipasho ya video zinazopendekezwa.