Nenda kwenye maudhui
Mchango na hatua tulizopiga

Mchango wetu

Watu kote duniani wametumia YouTube kufuata mambo wanayopenda, kuwasiliana na wengine na kubuni fursa za uchumi kwa ajili yao na jumuiya zao. Gundua hadithi za wanabiashara kadhaa wabunifu kwenye YouTube hapa.

Mchango wetu

Brandon Reed

"Kutimiza Azma ya Uhuishaji"

Brandon alibadilisha azma yake ya kuchora kuwa ajira yake kwa kujifunza jinsi ya kuhuisha kupitia mafunzo kwenye YouTube. Mifululizo yake iliyohuishwa kwenye YouTube imepata hadhira kubwa, hali inayomruhusu apate riziki ya kukimu familia yake.

Chasity Sereal

"Mtindo Mpya wa Ufanisi"

Chasity alitamani kila siku kuwa msanifu, lakini hakuwa na uwezo wa kwenda kwenye shule ya usanifu. Kwenye YouTube, aliweza kupata masomo ya usanifu wa mitindo ambayo yamemsaidia kukuza biashara yake ya mitindo ya mavazi.

Easton LaChappelle

"Kurejesha Matumaini kwa Mamilioni ya Watu"

Easton alitembelea YouTube ili kujifunza kuhusu mambo ya msingi ya roboti. Sasa anatengeneza miguu na mikono ya bandia, ambayo anapanga isambazwe duniani kote kwa bei nafuu.

Eddie Adams

"Kuboresha Maisha kupitia Muziki"

Eddie alitumia YouTube kujifunza jinsi ya kucheza selo, jambo lililomwondoa kwenye maisha ya upweke na akaanza kujumuika na wengine. Baadaye alianza kusomea shahada ya muziki katika Chuo Kikuu cha George Mason.

Cheong Choon Ng

"Matumizi ya Pete za Mipira"

Cheong alipata njia ya kushirikiana na binti zake katika kutengeneza bangili za pete za mipira na uvumbuzi wake wa Rainbow Loom ® ukawa maarufu sana kimataifa. Hili liliwezekana kupitia mafunzo kwenye YouTube.

Vicky Bennison

"Hadithi ya Pasta Grannies"

Miaka mitano iliyopita, Vicky alianzisha kituo chake cha YouTube ili kuorodhesha na kuhifadhi ujuzi wa mabibi nchini Italia, wa kutengeneza tambi za kienyeji. Sasa, Pasta Grannies huhamasisha kizazi kijacho cha wapishi wa nyumbani.

Macinley Butson

"Kuvumbua Zana ya Kukabili Miale Hatari"

Mwanafunzi wa Australia, Macinley, alikuwa na umri wa miaka 16 pekee alipoamua kujitahidi ili kulinda wanawake dhidi ya miale hatari inayotolewa wakati wa matibabu ya saratani ya matiti. Kupitia video za YouTube na majarida ya sayansi, alipata maelezo aliyohitaji ili kuvumbua mbinu inayoweza kuokoa maisha.

Krystn Keller

"Matibabu ya Kujipatia"

Krystn alikuwa akitafuta mbinu ya kutibu mtoto wake dhidi ya ukurutu. Alitumia video za kutengeneza sabuni za kiasili kwenye YouTube. Kwa kubahatisha, alipata mbinu mwafaka ya kutengeneza - na sasa ana biashara yake inayovuma.

Chef May

"Kugundua Mapishi ya Nyumbani"

Baada ya kujifunza kupika vyakula vya kithai alivyofurahia akiwa mtoto kwa kutazama YouTube, May alikuwa mpishi hodari mjini Manchester, Uingereza.

Nate Boyer

"Kutoka Jeshi la Marekani na Kuwa Mchezaji Maarufu"

Nate akiwa kazini Iraki, alifuata ndoto yake ya kuwa mchezaji wa kulipwa kwa kuboresha ujuzi wake kupitia mafunzo kwenye YouTube - mwishowe akawa mchezaji wa kulipwa aliyeanza kucheza akiwa mzee zaidi katika historia ya NFL.

Charles Lomu

"Kuleta Mabadiliko kupitia Kinyozi"

Charles alijifunza ujuzi wa kunyoa kupitia YouTube. Sasa analeta mabadiliko polepole kupitia kunyoa na kuwashauri vijana ili kuwasaidia wanafunzi wanaopitia wakati mgumu shuleni.

Meredith Bell

"Kuondoka Jijini na kuwa Mkulima"

Meredith aliacha kazi ya kampuni ili afuate ndoto yake ya kuwa mkulima katika Kaunti ya Kern, CA. Alitumia YouTube kujifunza jinsi ya kulima na akatimiza ndoto yake ya kuwa mkulima.

Joshua Carroll

"Kulenga juu"

Kutana na Joshua - mwanajeshi mstaafu aliyetimiza ndoto yake ya kuwa mwanafizikia kwa kujifunza Hisabati ya kina kwenye YouTube.

Eddie Woo

"Kushiriki Ubabe wa Hisabati"

Eddie Woo, mwalimu mjini Sydney, anashiriki upendo wake wa hesabu na jumuiya, nchi na ulimwengu kwa kupakia mafunzo yake kwenye YouTube. Sasa wanafunzi na walimu hutegea ili kujifunza kwa kutumia mbinu za Eddie Woo.