Nenda kwenye maudhui
Mipangilio ya mtumiaji

Vidhibiti vya wazazi

Vidhibiti vya wazazi

Kila familia ina njia tofauti ya kutumia teknolojia, kuvinjari mtandaoni na kuweka kanuni za dijitali. Ndiyo maana tunatoa chaguo na vidhibiti kwa wazazi na walezi ili kuwasaidia kuamua hali ya utumiaji kwenye YouTube inayofaa familia yao.

YouTube Kids

YouTube Kids ni programu iliyobuniwa kwa ajili ya watoto. Ilizinduliwa mnamo 2015 ili kuwapa watoto mahali salama na rahisi pa kugundua mambo yanayowavutia kupitia video mtandaoni. Programu hii ya kando ni toleo lililochujwa la YouTube na ina vituo na video chache ikilinganishwa na tovuti na programu kuu ya YouTube. Hii ni kwa sababu tunajitahidi kubaini maudhui yanayoambatana na umri, yanayotii kanuni zetu za ubora na ambayo ni anuai kiasi cha kukidhi mahitaji ya watoto kote duniani, ambao huvutiwa na mambo tofauti tofauti.

Mamilioni ya watazamaji hutumia YouTube Kids kila wiki; na tunajitahidi kuwapa wazazi wa aina zote njia za kuweka hali ya utumiaji inayofaa zaidi kwa mahitaji mahususi ya watoto wao na familia zao. Wazazi wanaweza kuchagua kati ya viwango vitatu vya maudhui vinavyolingana na umri (Chekechea, Wenye umri mdogo, Wakubwa) au waamue kujichagulia tu video, vituo na mikusanyiko ya maudhui ambayo wangependa watoto wao watazame.

Vidhibiti vya wazazi: Dhibiti na ubaini maudhui ambayo watoto wanaweza kutazama kwenye YouTube Kids

Hali ya utumiaji inayosimamiwa kwenye YouTube

Mwaka 2021, tulizindua chaguo mpya kwa wazazi ambao wameamua kuwa vijana wadogo au vijana wao wako tayari kuvinjari maudhui kwenye YouTube wakitumia akaunti inayodhibitiwa. Wazazi huunganisha Akaunti ya Google ya mtoto wao na yao kabla ya kumpa idhini ya kufikia YouTube, kisha kuchagua kwenye mipangilio ya maudhui ambayo kwa ujumla hulingana na ukadiriaji wa maudhui kwa vijana wadogo na wakubwa.

Hali hii inaonekana kabisa kama programu na tovuti za YouTube za kuripoti, lakini kuna marekebisho kwenye maudhui ambayo mtoto anaweza kupata na kutazama, vipengele wanavyoweza kutumia, mipangilio chaguomsingi ya akaunti na ulinzi wa matangazo. Hali hii pia hufanya kazi kwenye Family Link, inayotoa vidhibiti zaidi vya wazazi ili kusaidia kuongoza watoto wanapojifunza, kucheza na kugundua mtandaoni.

Hali ya utumiaji inayosimamiwa kwenye YouTube: Wazazi wanaweza kuchagua kutoka mipangilio ya maudhui ambayo hulingana kwa jumla na madaraja ya maudhui kwa vijana wadogo na wakubwa