Nenda kwenye maudhui
Mipangilio ya mtumiaji

Vidhibiti vya faragha

Vidhibiti vya faragha

Kudumisha usalama wako mtandaoni ni muhimu zaidi kwa kila kitu tunachofanya -- ni wajibu wetu kuwa wazi kuhusu data tunayokusanya huku tukikupa chaguo na udhibiti wa data yako. Data unayotoa kwenye Google na YouTube hukupa huduma muhimu. YouTube ni sehemu ya Google na inatii kanuni na sera za faragha za Google. Unaweza kudhibiti mipangilio ya faragha kila wakati kwa kutembelea Data Yako kwenye YouTube au Akaunti yako ya Google.

Data yako kwenye YouTube

Data yako kwenye YouTube ni kipengele kinachorahisisha kuelewa na kudhibiti data inayohifadhiwa na jinsi inavyotumiwa kwenye YouTube na Google. Kinakupa uwezo wa kufikia haraka vidhibiti vya faragha vya YouTube, pamoja na taarifa kuhusu YouTube inavyofanya Kazi na data yako kama vile kwa mambo uliyotafuta na historia ya video ulizotazama. Shughuli kwenye Historia yako ni za faragha na hutumiwa kuboresha hali yako ya utumiaji, kama vile kukukumbusha video ambazo umetazama, kukupa mapendekezo na matokeo ya utafutaji yanayokufaa zaidi. Unaweza kuondoa video mahususi kwenye historia ya video ulizotazama na hoja kwenye historia ya mambo uliyotafuta, kusimamisha historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta, au kuanza upya kwa kufuta historia yote ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta. Video zozote zinazoondolewa kwenye Historia yako hazitaathiri tena mapendekezo yako na hoja unazoondoa hazitaonekana kwenye upau wa kutafutia kama mapendekezo.

Data yako kwenye YouTube: Dhibiti mipangilio yako ya faragha kwenye YouTube na Google

Hali Fiche kwenye YouTube

Hali Fiche kwenye YouTube hukuruhusu uvinjari kwa faragha katika kipindi fulani, kwa hivyo historia ya mambo uliyotafuta na video ulizotazama kwenye akaunti yako haitaonyesha unachotazama na haitahifadhiwa kwenye akaunti ambako umeingia.

Hali fiche: Vinjari kwa faragha ili historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta isiathiri au kuonyesha unachotazama