Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube hufanya nini kuzuia mapendeleo?

Tunajitahidi ili kuhakikisha kuwa mifumo yetu haibuniwi kupendelea maudhui ya watu au makundi kulingana na mitazamo ya siasa au sifa nyingine kama vile jinsia, au mwelekeo wa kingono. Kila wakati, mfumo wetu umeendeleza hatua ya kushiriki taarifa kila mahali na kuwapa watu wengi fursa ya kujieleza.

Kuzuia mapendeleo

YouTube husaidia vipi kuhakikisha kuwa hamna mapendeleo hatari yasiyotarajiwa kwenye mifumo yake?

Tunatumia watu duniani kote kufunza mifumo yetu ya utafutaji na ugunduzi. Mwongozo wanaoutumia unapatikana hadharani. Mifumo yetu ya kutafuta na kupendekeza haijabuniwa kuchuja au kuondoa video au vituo kulingana na mitazamo mahususi ya siasa.

Pia, tunakagua mifumo yetu ya mashine kujifunza ili kusaidia kuhakikisha kuwa mapendeleo ya algoriti yasiyotarajiwa kama vile mapendeleo ya jinsia hayapo. Tunarekebisha makosa tunapoyapata na kufunza upya mifumo yetu kuwa sahihi zaidi baadaye.

Je, sera za YouTube hulenga makundi au mitazamo fulani ya siasa kwa njia isiyo ya haki?

Tunapobuni na kubadilisha sera zetu, tunahakikisha kuwa tunapata maoni kutoka vyanzo vingi, ikiwa ni pamoja na Watayarishi, wataalamu katika sekta fulani, watetezi wa uhuru wa kujieleza na mashirika ya sera kutoka mitazamo mbalimbali ya siasa.

Baada ya sera kubuniwa, tunatumia muda wa kutosha ili kuhakikisha kuwa sera mpya zilizobuniwa zinatekelezwa wakati wote na timu yetu ya wakaguzi kote duniani kulingana na mwongozo huru. Kabla sera yoyote izinduliwe, wakaguzi katika mazingira ya kujaribu (ambapo maamuzi ya sera hayatekelezwi) lazima wafanye maamuzi sawa katika kiwango cha juu zaidi. Wakishindwa kufanya hivyo, tunabadilisha mwongozo na mafunzo ya ndani ili kuhakikisha uwazi na kurudia mchakato. Lengo ni kupunguza mitazamo ya binafsi na mapendeleo ili kudumisha usawa na usahihi wa hali ya juu tunapotoa huduma kwa wingi. Tutazindua sera kwa umma pindi tutakapofikia kiwango kinachokubalika cha usahihi.