Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube hulinda vipi maudhui yaliyo na hakimiliki?

Tumewekeza mamilioni ya dola ili kubuni Zana ya Kudhibiti Hakimiliki iliyobuniwa kusawazisha mahitaji ya mfumo wote. Tunafanya kazi na wenye hakimiliki na Watayarishi wa aina zote ili tuwape vipengele vinavyofaa kulingana na wingi wa maudhui yao kwenye YouTube na njia ambazo wameweka ili kudhibiti kwa kuwajibika maudhui yao mtandaoni.

Kulinda hakimiliki

Zana yetu ya Kudhibiti Hakimiliki inawapa wenye hakimiliki udhibiti wa maudhui yao yaliyo na hakimiliki kwenye YouTube. Hutumia mchakato wa Ulinganishaji wa Content ID, ambao ni teknolojia bora zaidi inayotumiwa kutambua maudhui yanayoweza kukiuka sera. Inajumuisha fomu yetu ya wavuti ya umma ya DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali), inayopatikana kwa watumiaji wote bilioni 2 wanaotembelea YouTube; Copyright Match Tool, zana yetu iliyobuniwa kimahususi kwa ajili ya Watayarishi na inapatikana kwa zaidi ya watayarishi 1,500,000; na Content ID, suluhisho letu la biashara kwa walio na mahitaji ya kudhibiti hakimiliki kama vile studio za muziki, studio za filamu au jamii ya kukusanya mirabaha.

Baada ya kutupa faili za marejeleo, watumiaji wa Content ID na Copyright Match Tool huarifiwa kiotomatiki kuhusu video zinazopakiwa na mtumiaji ambazo huenda zina kazi zao za ubunifu. Pia, watumiaji wa Content ID wanaweza kuchagua mapema mambo ambayo wangependa yafanyike baada ya video hizo kutambuliwa. Kutokana na chaguo tofauti ambazo Content ID huwapa wenye hakimiliki, Content ID si tu suluhisho la kakabili matukio ya kughushi, lakini pia ni zana ya kuzalisha mapato. YouTube imelipa zaidi ya bilioni $5.5 kwa wenye hakimiliki kutokana na mapato ya matangazo pekee katika maudhui ambayo wamedai na kuchuma mapato kupitia Content ID.