Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube husaidia vipi ushirikiano wa kiraia na kujilinda, kutoegemea upande wowote na kudumisha usawa wakati wa uchaguzi?

Kutokana na watumiaji wengi duniani kote wanaokuja kwenye YouTube kupata maelezo kuhusu viongozi wa siasa, kushiriki katika ushirikiano wa kiraia na kutoa maoni ya dhati kuhusu matukio ya sasa, tuna wajibu wa kusaidia kuwepo kwa raia wanaofahamu mambo na kuendeleza majadiliano mazuri ya kisiasa. Ili kutimiza wajibu huu, tunaondoa maudhui yanayokiuka sera, kukuza vyanzo vya kuaminika vya habari, kupunguza kuenea kwa maelezo ya kupotosha yanayohusiana na uchaguzi na kutoa nyenzo nyingi kwa washirika wa kiraia, kama vile wafanyakazi wa serikali, wagombeaji, mashirika ya kiraia na Watayarishi wa maudhui ya siasa ili kuhakikisha sauti nyingi zinasikika.

Kusaidia uadilifu wa kisiasa

YouTube huondoa vipi maudhui yanayohusiana na uchaguzi ambayo yanakiuka sera?

Mwongozo wa Jumuiya Yetu unatoa utaratibu wazi kuhusu maudhui ambayo hayaruhusiwi kwenye YouTube. Sera zetu zinajumuisha maudhui yanayohusiana na uchaguzi na tunatekeleza sera hizi kila wakati, bila kujali anayeyaweka. Tunatumia mseto wa watu na mashine ili kutambua kwa wingi maudhui ambayo huenda yana tatizo. Tunapotambua maudhui kama hayo, wakaguzi huthibitisha kama yanakiuka sera zetu. Kama yanakiuka sera, maudhui hayo huondolewa na hutumiwa kufunza mashine zetu ili zitambue vizuri baadaye.

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ambapo sera zetu thabiti za matendo ya udanganyifu hutumiwa kwenye maudhui yanayohusiana na uchaguzi:

  • Maudhui ambayo yamebadilishwa kwa ujanja kwa nia ya kupotosha watumiaji (mbali na klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha) na yanaweza kusababisha hatari kubwa; kwa mfano, video ambayo imebadilishwa kwa ujanja ili kufanya ionekane kuwa mfanyakazi wa serikali amekufa.

  • Maudhui yanayolenga kupotosha watu kuhusu michakato ya kupiga kura au kuhesabu watu, kama vile kuwafahamisha watazamaji tarehe isiyo sahihi ya kupiga kura.

  • Maudhui yanayoendeleza madai ya uongo yanayohusiana na masharti ya bandia ya kujiunga kwa wagombeaji wa sasa wa siasa na maafisa waliochaguliwa wa sasa ili kufanya kazi, kama vile madai ya uongo kuwa mgombeaji hajatimiza masharti ya kufanya kazi kulingana na maelezo ya uongo kuhusu hali ya uraia inayohitajika ili kufanya kazi katika nchi hiyo.

  • Maudhui yaliyo na maelezo yaliyodukuliwa, ambayo yakifumbuliwa yanaweza kuathiri michakato ya kidemokrasia, kama vile uchaguzi na kuhesabu watu. Kwa mfano, video zilizo na maelezo yaliyodukuliwa kuhusu mgombeaji wa kisiasa zinazoshirikiwa kwa lengo la kuathiri uchaguzi.

  • Maudhui yanayohimiza wengine kukatiza michakato ya demokrasia, kama vile kuzuia au kuingilia utaratibu wa kupiga kura. Kwa mfano, kuambia watazamaji watunge foleni ndefu za kupiga kura kwa lengo la kufanya iwe vigumu kwa wengine kupiga kura.

Pia, tunafunga vituo ambavyo:

  • Vinajaribu kuiga mtu au kituo kingine, kuwakilisha kwa njia ya uongo nchi yake, au kuficha ushirikiano wake na mhusika wa serikali.

  • Kuongeza kwa njia bandia idadi ya maoni, mara ambazo video imetazamwa, mara ambazo video imependwa au vipimo vingine kupitia matumizi ya mfumo wa kiotomatiki au kwa kuonyesha video kwa watazamaji wasiotarajia.

Kama kawaida, tunatekeleza sera zetu bila kujali mtazamo wa kisiasa wa video.

YouTube hukabili vipi matukio ya wageni ya kuingilia michakato ya kupiga kura?

Ili kukabili matukio ya wageni au wenyeji kuingilia michakato ya kupiga kura, tunashirikiana kwa karibu na Kikundi cha Kuchanganua Hatari kwenye Google (TAG) ili kubaini watendaji wabaya na kufunga akaunti na vituo vyao. Kupitia kikundi cha TAG, tunashirikiana na kampuni nyingine za teknolojia ili kusambaza uchunguzi na mbinu bora, na kushiriki taarifa za vitisho na wanaotekeleza sheria.

YouTube huwapa vipi watazamaji uwezo wa kufikia habari na taarifa za kuaminika zinazohusiana na uchaguzi?

Habari na matukio ya siasa yanaweza kuwa na maelezo ya kupotosha, kwa hivyo upatikanaji wa vyanzo bora vya habari ni muhimu. Ndiyo maana tunakuza vyanzo vya kuaminika, ikiwa ni pamoja na vyanzo vya habari kama vile CNN na Fox News, kwa habari na taarifa katika matokeo ya utafutaji na vidirisha vya "Inayofuata". Mbali na hayo, tuna vipengele vya bidhaa vinavyosaidia kuangazia maudhui kwenye mfumo wetu, ikiwa ni pamoja na rafu za Habari Kuu na Habari Zinazojiri ili kuangazia uanahabari bora, pia vidirisha vya taarifa vinavyoonyesha vyanzo vya pesa chini ya video kutoka kwa wachapishaji wanaopokea ufadhili wa umma au serikali. Tumepanua pia vidirisha vyetu vya taarifa za kuhakikisha uweli nchini Marekani. Kipengele hiki kinatoa muktadha kutoka kwenye makala mengine yaliyohakikishwa ukweli juu ya matokeo ya utafutaji wa hoja husika—ikiwa ni pamoja na madai mahususi kuhusu uchaguzi.

Pia, tunaonyesha vidirisha vya taarifa vinavyounganisha kwenye vyanzo vingine katika idadi ndogo ya mada ambazo zinaweza kuwa na maelezo ya kupotosha na ambazo sasa zinajumuisha kupiga kura kupitia barua za posta. Hii inamaanisha kuwa chini ya video zinazojadili kupiga kura kupitia barua za posta, utaona kidirisha cha taarifa kinachokuelekeza kwenye taarifa za kuaminika kutoka Bipartisan Policy Center, kituo kinachoshughulikia masuala ya vyama vingi.

Mbali na vipengele vyetu vilivyo kwenye bidhaa na ambavyo huwa vimewashwa saa zote, vinavyopata habari kutoka vyanzo vya kuaminika kwenye mfumo wetu, tunachukua hatua za ziada wakati wa matukio muhimu ya kiraia na uchaguzi. Kwa mfano, wakati kuna matukio makuu ya moja kwa moja -- kama vile Taarifa ya Rais kwenye Bunge, mijadala ya uchaguzi na kutawazwa kwa marais -- tunajitahidi kufanya mitiririko hii ipatikane kwa urahisi kwa hadhira pana kwenye mfumo wetu.

Katika uchaguzi wa Marekani 2020, unapotafuta mgombeaji wa urais au Ubunge kwenye YouTube, tutaonyesha kidirisha cha taarifa za mgombeaji na taarifa za ziada kuhusu mgombeaji huyo—kwa mfano, chama na ofisi yake—juu ya matokeo ya utafutaji. Tunaangazia pia vituo rasmi vya YouTube vya wagombeaji vinapopatikana.

Vidirisha vya taarifa za wagombeaji: huunganisha kwenye taarifa za wengine za kuaminika kuhusu wagombeaji

Pia, unapotafuta hoja mahususi zinazohusiana na usajili wa wapiga kura kwenye YouTube utaona kidirisha cha taarifa kuhusu kupiga kura katika sehemu ya juu ya ukurasa unaokuelekeza kwenye kipengele cha Google cha "Jinsi ya kujisajili kupiga kura" katika jimbo uliko. Taarifa zinazohusiana na jinsi ya kujisajili kupiga kura zinajumuisha maelezo kama vile tarehe za mwisho, chaguo za kujisajili na njia rahisi ya kukagua hali ya usajili wako.

Pia, utaona [kidirisha cha taarifa] kuhusu kupiga kura(https://support.google.com/youtube?p=election_information_panels) katika sehemu ya juu ya matokeo ukitafuta kwenye YouTube hoja mahususi zinazohusiana na jinsi ya kupiga kura, kinachoelekeza kwenye kipengele cha Google cha "Jinsi ya kupiga kura". Zana hii inajumuisha taarifa zinazoaminika kuhusu jinsi ya kupiga kura katika jimbo uliko, ikiwa ni pamoja na maelezo kama vile masharti ya kitambulisho, siku ya kumalizika kwa mchakato wa kujisajili na kupiga kura. Pia, mwongozo kuhusu njia tofauti za kupiga kura, kama vile ana kwa ana au kupitia barua za posta.

Google hufanya kazi na washirika wengine wa data wasioegemea upande wowote kama vile Democracy Works, ambao hujumlisha data rasmi moja kwa moja kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi katika jimbo na kaunti na huunganisha kwenye tovuti rasmi ya serikali ya jimbo uliko ili upate maelezo zaidi.

Kidirisha cha taarifa kuhusu kupiga kura: huunganisha kwenye maelezo ya wengine yanayoaminika kuhusu jinsi ya kupiga kura au kujisajili kupiga kura

Kwa uchaguzi wa Marekani 2020, tulizindua kidirisha kipya cha taarifa za matokeo ya uchaguzi katika sehemu ya juu ya matokeo ya utafutaji kwa hoja pana zinazohusiana na uchaguzi chini ya video zinazojadili uchaguzi. Kidirisha hiki cha taarifa kinadokeza kuwa huenda matokeo ya uchaguzi yasiwe ya mwisho na huunganisha kwenye kipengele cha Google cha matokeo ya uchaguzi, kinachokuwezesha kufuatilia matokeo ya uchaguzi katika muda halisi. Kama ilivyokuwa katika miaka ya awali na uchaguzi wa 2020, Google hufanya kazi na The Associated Press ili kutoa matokeo ya uchaguzi yanayoaminika.

Kidirisha cha taarifa za matokeo ya uchaguzi: huunganisha kwenye matokeo mpya ya uchaguzi katika Google

Kwa taarifa mpya, tafadhali angalia blogu ya YouTube.

Ni zana na nyenzo zipi za YouTube zinapatikana kwa washirika wa kiraia kama vile wafanyakazi wa serikali, wagombeaji, mashirika ya kiraia na Watayarishi wa maudhui ya siasa?

YouTube ina zana na nyenzo nyingi za kusaidia washirika wa kiraia kuendeleza chapa zao na kuwasiliana na wahusika. Tumebuni miongozo mingi ya kuwasaidia kuanza.

  • Mwongozo wa Jumla wa Kuanza Kutumia - Gundua mbinu bora na mifano inayolenga washirika wa kiraia ili wakuze vituo vyao, ikiwa ni pamoja na vitengo vya chapa, kupanga maudhui, kutunga maudhui na ugunduzi wa maudhui.

  • Mwongozo wa Kutiririsha Moja kwa Moja - Pata maelezo kuhusu jinsi washirika wa kiraia wanaweza kuwasiliana vizuri na jumuiya yao moja kwa moja kwenye YouTube, ikiwa ni pamoja na maelezo kuhusu kuandaa matukio ya moja kwa moja, mikutano na wanahabari na mawasiliano na hadhira katika muda halisi - na kugundua chaguo za maunzi na programu ili kuwafanya wanufaike zaidi katika mitiririko yao ya moja kwa moja.

YouTube huchukulia vipi utangazaji wa siasa?

Kwa sababu ya umuhimu wa uaminifu wa pamoja katika mchakato wa kidemokrasia, tungependa kuboresha imani ya wapigakura katika matangazo ya siasa wanayoweza kuona kwenye mifumo ya matangazo. Tunatekeleza mwongozo wetu wote bila kujali mtazamo wa siasa kwenye video.

Matangazo yanayoonyeshwa kwenye YouTube yanategemea sera za Google Ads, maudhui yanayowekwa kwenye mfumo wetu yanategemea Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube, na vituo ambavyo ni sehemu ya Mpango wa Washirika wa YouTube vinategemea Sera za Uchumaji wa Mapato kwenye YouTube. Kwa hivyo video inayopakiwa kwenye kituo cha YouTube na Mtayarishi inategemea Mwongozo wa Jumuiya yetu lakini iwapo video hiyo imeangaziwa kama tangazo, itategemea tena sera za Matangazo ya Google.

Sera za matangazo ya Google hudhibiti matangazo yanayoonyeshwa kwenye YouTube. Haturuhusu ulengaji wa moja kwa moja (yakiwemo matangazo yasiyo ya siasa). Watangazaji walioidhinishwa wa siasa nchini Marekani wanaweza tu kuonyesha matangazo ya uchaguzi kuhusu umri, jinsia, mahali (k.m. msimbo wa posta) na muktadha (k.m. mada). Ufumbuzi wazi unahitajika kwa matangazo yote ya uchaguzi ili kukusaidia uelewe vyema anayeyalipia - data inayopatikana hadharani kwenye Ripoti yetu ya Uwazi. Tunatumia teknolojia na wakaguzi kukagua iwapo sera zetu zinafuatwa.

Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube hubainisha maudhui yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa kwenye YouTube, na tuna sera ambazo zimebuniwa mahususi kwa ajili ya uchaguzi. Sera zinazohusiana moja kwa moja na uchaguzi ni pamoja na:

  • Kuzuia wapigakura
  • Kudhibiti kushiriki katika hesabu ya watu
  • Madai ya uongo kuhusu ustahiki wa mgombeaji
  • Uigaji
  • Chuki na unyanyasaji
  • Taka, matendo ya udanganyifu na ulaghai

Sera za uchumaji wa mapato za YouTube zinatumika kwa watayarishi ambao wako kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) ili kutumia bidhaa za uchumaji wa mapato kupata pesa kwenye vituo vyao. Lazima vituo vinavyoshiriki vitimize masharti ya kujiunga na pia vifuate sera zetu za uchumaji wa mapato na mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji. Kukosa kufanya hivyo kunamaanisha maudhui yatakuwa na matangazo machache au hayatakuwa na matangazo yoyote.

YouTube hushughulikiwa vipi matangazo yaliyo na maudhui ya siasa katika sehemu tofauti za dunia?

Watayarishi wa Maudhui ya Siasa ambao wangependa kuthibitishwa ili kuonyesha matangazo yaliyo na maudhui ya siasa watahitaji kupata maelezo zaidi kuhusu utangazaji wa maudhui ya siasa katika nchi uliko.