YouTube Inavyofanya Kazi
LENGO LETU
Kumpa kila mtu fursa ya kujieleza na kuonyesha wote matukio ya ulimwengu
Tunaamini kuwa kila mtu anapaswa kuwa na fursa ya kujieleza na kuwa ulimwengu huwa pahali pazuri tunaposikiliza, kueleza na kukuza jumuiya kupitia simulizi zetu.
Vinjari tovuti hii ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi YouTube inavyotimiza malengo haya.
VIUNGO VYA HARAKA
MAPYA
Kulinda vijana katika ulimwengu wa kidijitali, si dhidi ya ulimwengu wa kidijitali
Kuongezeka kwa umaarufu wa teknolojia mpya miongoni mwa vijana, iwe ni michezo ya video, simu mahiri au majukwaa ya utiririshaji, kumeibua maswali muhimu kuhusu si tu njia sahihi ya wazazi kuwasaidia watoto wao kufahamu mazingira ya teknolojia yanayobadilika; lakini pia jukumu ambalo udhibiti unapaswa kutekeleza katika kuwalinda na kuwawezesha vijana.
Njia 20 tunavyoadhimisha miongo miwili tangu kuzinduliwa kwa YouTube
Furahia kwa sababu YouTube inaadhimisha miaka 20 tangu kuzinduliwa! Tangu klipu ya kwanza ya sekunde 19 hadi zaidi ya video bilioni 20 zilizopakiwa,1 ikiwa ni pamoja na muziki, Video Fupi, podikasti na zaidi, tumekua sana katika miongo miwili tu. Tunaanza maadhimisho yetu kwa njia nyingi za kusherehekea. Angalia baadhi ya vipengele, takwimu na vitu vyetu vipya fiche hapa chini ili kukusaidia kuadhimisha:
YouTube na viongozi wa sekta wanatangaza Mpango wa Nidhamu Dijitali kwa Vijana
Ujumbe kutoka kwa Neal Mohan, Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa YouTube : Leo, YouTube ina furaha kuungana na zaidi ya wasambazaji na watayarishi kumi wa maudhui wanaowakilisha nchi kumi ili kushiriki katika Mpango wa Nidhamu Dijitali kwa Vijana, unaounga mkono maono jumuishi ya ukuaji wa maudhui ya ubora wa juu yanayoambatana na umri kwa vijana.