Ungependa kujua
jinsi YouTube inavyofanya kazi?
Kila siku, mamilioni ya watu hutembelea YouTube kufahamishwa, kuhamasishwa au kuburudika tu. Kwa muda mrefu, maswali yameulizwa kuhusu jinsi YouTube hufanya kazi, kwa hivyo tumebuni tovuti hii ili kutoa baadhi ya majibu - na kufafanua tunachofanya ili kubuni mfumo unaowajibika ambao unaweza kutegemewa na watumiaji, watayarishi na wasanii katika jumuiya yetu.
Kufanya YouTube iwe salama zaidi
Katika kiini cha utaratibu wetu tuna mbinu nne - Kuondoa maudhui yanayokiuka sera zetu, Kupunguza kuenea kwa maelezo hatari ya kupotosha na maudhui yanayokaribia kukiuka sera zetu, Kukuza vyanzo vya kuaminika vya habari na taarifa na Kuzawadi Watayarishi wanaoaminika.
Kufanya YouTube iwe salama zaidi
Chochote unachotafuta kwenye YouTube, tungependa utulie kwa amani ukiwa hapo.
Tungependa uwe na hali bora zaidi ya utumiaji unapotumia YouTube. Kwa hivyo, bidhaa zetu hukusaidia upate unachotafuta na uwe na udhibiti wa unachoona. Kwa sasa, sera zetu hufafanua mambo unayoweza na usioweza kufanya ukiwa kwenye YouTube, kwa hivyo kila mtu anatumia kanuni sawa.
Endelea kusoma ili upate maelezo kuhusu jinsi kila mojawapo ya bidhaa na sera yetu hufanya kazi.
Pata maelezo zaidi kuhusu hatua tunazopiga katika juhudi zetu za uwajibikaji na athari ambayo YouTube imetoa kwenye utamaduni, jamii na uchumi wa maeneo mahususi.
Hatua tulizopiga katika kudhibiti maudhui hatari
Hoja muhimu za data za kukuonyesha jinsi tunavyotekeleza sera zetu kuhusu maudhui hatari.
Mchango wetu
Hadithi kuhusu jinsi baadhi ya wanabiashara wabunifu kwenye YouTube wanabadilisha maisha yao na jamii zao.
Mitindo na utamaduni
Data, mitindo ya sasa na rekodi zinazokusaidia ufahamu vyema kizazi kijacho cha Watayarishi na wasanii.