Wakati tunategemea uwezo wa AI, tungependa kuhakikisha kuwa
tunatumia mbinu sahihi za ulinzi. Sera na bidhaa zetu
zinalenga kulinda na kuwezesha watayarishi wa maudhui katika
enzi ya AI na kudumisha usalama wa jumuiya ya YouTube.
Kama kawaida,
Mwongozo wetu wa Jumuiya
hufafanua kanuni za kufuatwa na maudhui yote — ikiwa ni pamoja
na maudhui yaliyotayarishwa kwa AI kwenye YouTube. Pia tuna
sera mahususi zinazoelekeza jinsi tunavyoshughulikia maudhui
yaliyotayarishwa kwa AI, ikiwa ni pamoja na masharti ya
ufumbuzi na ya uwekaji lebo.
Tunahitaji watayarishi wafumbue maudhui yanayofanana na
uhalisia yanapotayarishwa kwa kutumia maudhui sanisi au
yaliyobadilishwa, ikiwa ni pamoja na Lebo za AI Zalishi
zinazoweza kuonyeshwa kwenye maelezo ya video yako na iwapo
maudhui yanahusiana na mada nyeti kama vile afya, habari,
uchaguzi au fedha, tunaweza pia kuonyesha lebo katika video
hiyo.
Tumesasisha pia viwango vyetu vya faragha vinavyoruhusu kuomba
kuondolewa kwa maudhui yaliyotayarishwa kwa AI au maudhui
mengine sanisi au yaliyobadilishwa ambayo yanaiga mtu
anayeweza kutambulika, ikiwa ni pamoja na uso au sauti yake
kwa kutumia mchakato wetu wa ombi la faragha. Si maudhui yote
yatakayoondolewa kwenye YouTube na tunazingatia vigezo
mbalimbali tunapotathmini maombi haya. Hii inaweza kujumuisha
iwapo maudhui ni ya tashtiti au bezo, iwapo mtu anayetuma ombi
anaweza kutambuliwa kimahususi au iwapo yanamwangazia kiongozi
katika serikali au mtu maarufu, hali ambayo huenda ikahitaji
kutimiza vigezo madhubuti zaidi.