Ni nani anapaswa kuitumia?
Huku ikipatikana katika zaidi ya lugha 80, wenye
haki wote wanaweza kufikia fomu ya wavuti, ambayo
tumebuni kama njia rahisi na ya haraka ya kutuma
maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.
**Je, inafanya kazi gani? **
Wenye haki huweka maelezo machache ya ombi lao,
ambayo hukaguliwa na YouTube ili kubaini iwapo
yanatii masharti ya kisheria ya kuondoa maudhui
yaliyoripotiwa.
Wenye haki wanaweza kufikia vipengele thabiti,
ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuiomba YouTube izuie
kiotomatiki nakala za maudhui yaliyoondolewa ili
yasipakiwe upya.