Kwa kuwa mfumo wetu unatumiwa duniani kote, mifumo na sera
zetu za uchaguzi hubuniwa na kutekelezwa kwa kuzingatia
mtazamo wa jumla -
Mwongozo wetu wa Jumuiya
hutekelezwa kwenye lugha na mifumo yetu huunganisha wapiga
kura katika nchi zote tunakohudumu na habari na taarifa za
ubora wa juu kuhusu uchaguzi, ambayo yanawafaa zaidi.
Watumiaji wanapotazama au kutafuta maudhui ya uchaguzi
katika YouTube, mfumo wetu wa mapendekezo huonyesha maudhui
ya ubora wa juu kwenye matokeo ya utafutaji, ukurasa wa
kwanza na kidirisha cha “Tazama Inayofuata”. Kwa hivyo,
wapiga kura hupata maudhui ya ubora wa juu kutoka vyanzo
mbalimbali vya habari. Pia, ili kupanua ufikiaji wa maudhui
mubashara yanayohusiana na uchaguzi, mitiririko mubashara ya
matukio makuu yanayohusiana na uchaguzi – kama vile mijadala
na maonyesho ya matukio ya uchaguzi – yanaweza kuonyeshwa
katika sehemu ya juu ya ukurasa wa kwanza au ya matokeo ya
utafutaji wako unapotafuta video zinazohusiana na matukio
mubashara mahususi ya uchaguzi wa kitaifa.