Tuna baadhi ya mbinu thabiti za kuwalinda watumiaji wetu
wachanga dhidi ya maudhui hatari. Mbinu hizi zinasimamiwa na
sera zinazopatikana
hapa.
YouTube hairuhusu maudhui yanayolenga watoto wadogo na
familia, yaliyo na mada za ngono, vurugu, lugha chafu au mada
nyingine za watu wazima ambazo hazifai hadhira za watoto.
Tunasasisha mara kwa mara hali ya matumizi ya bidhaa na sera
zetu za familia kwa kushauriana na wataalamu wa maudhui ya
watoto, ukuaji wa watoto, mafunzo ya kidijitali na uraia
kutoka katika nyanja mbalimbali za taaluma, mashirika yasiyo
ya faida na ya kitabibu.
Kamati hii ya Ushauri ya Vijana na Familia
ni mkusanyiko wa wataalamu wanaojitegemea wanaoshauri kuhusu
bidhaa, sera na huduma tunazotoa kwa vijana na familia.