Bango kuu la kujifunza

Kujifunza

Kila siku, watu hutembelea YouTube ili kujifunza mambo mapya. Watu hutumia YouTube ili kuboresha maisha yao kupitia maelezo mapya, iwe ni kupata usaidizi kuhusu mazoezi ya shuleni, kujifunza lugha ya kigeni au kugundua kazi tofauti.

Lengo letu ni kuendelea kurahisisha mchakato wa kujifunza na kufundisha kwenye YouTube kwa mabilioni ya watayarishi, walimu, wanafunzi na wanaojifunza kila siku, duniani kote, ambao wanategemea mfumo huu ili kuendelea.

Jinsi Watumiaji Wanavyojifunza kwenye YouTube

YouTube huvutia watu mbalimbali wanaojifunza ambao wanatafuta njia tofauti za kujifunza.

Watu huchagua kujifunza kwenye YouTube kwa sababu ni maktaba kubwa zaidi duniani ya maudhui kuhusu mada za aina zote iwe ni usimbaji au kemia. Watumiaji hufurahia hali ya kujifunza kwenye YouTube kwa kuwa inatoa fursa ya kugundua watayarishi na jumuiya zinazowahamasisha, kufahamu zaidi maudhui wanayochagua na kuendelea kujifunza kadiri ya uwezo wao.

Katika zana na bidhaa zetu mbalimbali zinazolenga kujifunza, tunawezesha safari za kujifunza za watumiaji kwa kufanya hali za kujifunza ziwe shirikishi, kuimarisha hali za kujifunza kwenye mfumo, kutoa maoni kuhusu hatua walizopiga na zaidi.

صورة للاختبارات
صورة للدورات التعليمية

Jinsi YouTube Inavyosaidia Watumiaji wake Kujifunza

Watu wanapotembelea YouTube, hupata maudhui ya elimu yenye ubora wa juu kutoka kwa watayarishi wa kiwango cha kimataifa na zana zinazokuza mazingira salama, yenye manufaa na yanayoweza kufikiwa ya kujifunzia yanayolenga rika zote.

Kujifunza kwenye YouTube kunawezeshwa na maudhui ya elimu yenye ubora wa juu yanayotayarishwa na watayarishi bora kutoka kote duniani, wengi wao wakiwa walimu wa zamani wanaotumia maarifa yao ya elimu katika masomo mbalimbali ili kutayarisha maudhui yanayowasaidia watumiaji kujifunza.

YouTube ina maudhui mengine, si burudani pekee – ni mahali pa watu kujifunza ujuzi mpya, kufahamu zaidi ari zao, kujieleza kwa njia ya kipekee na kugundua watayarishi. Tunafahamu thamani ya YouTube katika maisha na michakato ya kujifunza ya watumiaji wetu na tumejitolea kuifanya iwe hali salama, nzuri na yenye manufaa.

1

Nchini Marekani, asilimia 92 ya watazamaji huripoti kutumia YouTube kupata maelezo na maarifa.

Kulingana na utafiti kutoka Oxford Economics

Jinsi YouTube inavyotumika kama Zana ya Walimu

Kwa walimu, YouTube ni zana ya elimu inayoaminika na yenye ufanisi ndani na nje ya darasa.

Walimu hutumia YouTube kuboresha mipangilio ya masomo ya kawaida kwa video za kujifunza zinazoshirikisha na zenye ufanisi na kuandaa mipangilio ya masomo iliyowekewa mapendeleo mahususi kwa wanafunzi wanaohitaji muda na umakini wa ziada ili kukuza uelewa.

Kichezaji cha Elimu

Kichezaji cha Elimu cha YouTube ni kichezaji cha YouTube kilichopachikwa kisichokatiza ambacho kinaboresha jinsi YouTube inavyoonyesha video ndani ya zana za elimu, ili wanafunzi na wakufunzi waweze kufikia malengo yao pamoja. Kimeundwa kifae wanafunzi, kinaendelea kuzingatia faragha ya wanafunzi na kuwaruhusu wakufunzi kukabidhi video za YouTube huku wakidhibiti ufikiaji wa moja kwa moja wa wanafunzi kwenye mfumo.

Pata maelezo zaidi
1

ya walimu waliofanyiwa utafiti duniani kote wametumia YouTube katika majukumu yao wakiwa walimu.*

1

kati ya walimu waliofanyiwa utafiti duniani kote wanasema YouTube ina aina sahihi ya maudhui ya kuboresha mipangilio ya masomo ya kawaida.*

1

ya walimu waliofanyiwa utafiti duniani kote wanasema maudhui yanayohusiana na kujifunza kwenye YouTube huwasaidia wanafunzi kutumia muda wao mtandaoni kwa njia nzuri.*

*Kulingana na utafiti wa Agosti 2024 uliofanywa na Ipsos katika masoko kumi na moja (Australia, Brazili, Kanada, Ujerumani, Ufaransa, Indonesia, India, Japani, Korea Kusini, Uingereza na Marekani).

Jinsi Ushirika wa YouTube Unavyoboresha Mafunzo

YouTube inashirikiana na wataalamu wa elimu ili kuwapa watumiaji wetu hali za kujifunza zenye matokeo ya hali ya juu. Kupitia juhudi zetu za ushirikiano, tunalenga kuwa na huduma zinazopatikana duniani kote na ndiyo maana tunaendelea kuratibu fursa za ushirikiano zinazopatikana duniani kote. Kwa mfano:

Tunashirikiana na UNESCO ili kuimarisha ufikiaji wa maudhui bora ya elimu katika maeneo yote ya Amerika ya Kusini. Ushirikiano huu unalenga kuanzisha chaneli maalum za YouTube zinazotoa maudhui yaliyoratibiwa yanayolingana na mtaala wa kitaifa wa nchi husika wa Shule za Upili na za Kati. Pia, huwapa walimu nyenzo muhimu na za usaidizi, hivyo kuwawezesha kujumuisha kwa urahisi video hizi zilizoratibiwa kwenye mipangilio yao ya masomo na kuanzisha hali za kujifunza zinazoshirikisha zaidi.

Picha ya Unesco

Kwa ushirikiano na YouTube India, NPTEL inatoa Kozi 100 za Vyeti kwenye YouTube katika masomo mbalimbali iwe ni Uendeshaji wa Roketi, Uchanganuzi wa Kifasihi, Mashine Kujifunza au Saikolojia ya Michezo. Kila kozi imetayarishwa ili kutoa maudhui yaliyopangwa, ikiwa ni pamoja na mihadhara ya video, slaidi na viambatisho vya faili vya ziada, vinavyotoa hali ya kina ya kujifunza.

Picha ya Nptel

Tunashirikiana na Common Sense Media ili kuwapa walimu maudhui yenye ubora wa juu na yanayoshirikisha bila mchakato wa utafutaji unaotumia muda mwingi. Mchakato uliofanikishwa kupitia mikusanyiko ya video zilizoratibiwa za walimu wa shule za kati kuhusu mada zilizobainishwa mapema za Hisabati na Ushauri zinazolingana na utaratibu wa kujifunza wa Common Core Standards, CASEL na Common Sense Media.

Picha ya Common sense media

Tumeshirikiana na Chuo Kikuu cha Jimbo la Arizona (ASU) na Crash Course ili kuunda Study Hall. Ni mbinu mpya inayorahisisha mchakato wa elimu ya chuo kikuu huku ikiunda njia ya bei nafuu na inayoweza kufikiwa ya kupata alama za chuo kikuu.

Picha ya chuo kikuu cha jimbo la Arizona

Gundua zaidi

Ungependa kujifunza ujuzi mpya? Iruhusu YouTube ikusaidie kujifunza jinsi ya kusimba
Njia 3 ambazo Kichezaji cha YouTube cha Elimu kinaboresha Edtech kwa wanaojifunza
Njia mpya ya kupata elimu ya juu inayoanzia kwenye YouTube!
Kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani: Kutambua mchango wa walimu, pamoja na watayarishi wa YouTube