Mapendekezo

Mfumo wa mapendekezo ya YouTube huwaunganisha mabilioni ya watu kote duniani na maudhui ambayo yanahamasisha, kufunza na kuburudisha kwa njia ya kipekee. Kwa sababu kila mtu ana tabia za kipekee za utazamaji, kazi ya msingi ya mapendekezo ni kutimiza mahitaji ya watumiaji kwa kuwasaidia watu kupata video ambazo wangependa kutazama na zilizo muhimu.

Mapendekezo kwenye YouTube

Katika kiwango cha juu zaidi, mfumo wetu wa mapendekezo umeundwa ili kutarajia na kukidhi mahitaji ya mtumiaji ya kuongeza thamani kupitia utazamaji unaofaa na kuridhisha. Kuelewa mtindo wa utazamaji wa mtumiaji, maudhui anayopenda, maudhui asiyopenda, chaneli anazofuatilia na maoni yake, ikiwa ni pamoja na kutokana na utafiti wa kubainisha kiwango cha kuridhika, hutusaidia kukidhi mahitaji kwa ufanisi zaidi. Kama ilivyo kwenye huduma ya Tafuta, pia, tunazingatia ubora na sifa ya chaneli ili kubaini jinsi, wakati na anayeweza kuonyeshwa maudhui na kutumia wakaguzi wa nje ili kutusaidia kuelewa jinsi mtazamaji wa kawaida anaweza kuchukulia maudhui ili kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata utazamaji wa ubora wa juu.

Pia tunafahamu kuwa si kila mtu angependa kuingia katika akaunti na kuruhusu tufikie maelezo yake kila wakati, kwa hivyo tumeunda vidhibiti vinavyowasaidia watu kuamua kiwango cha data ambacho wangependa ifikiwe. Watumiaji wanaweza kusitisha, kubadilisha au kufuta historia ya video walizotazama pamoja na utafutaji wao kwenye YouTube wakati wowote wanapotaka.

Unaweza kupata mapendekezo katika sehemu mbili kuu kwenye YouTube:

Ukurasa wa Kwanza
Kidirisha cha “Inayofuata”

Jinsi YouTube Inavyoangazia Maelezo ya Ubora wa Juu

Kwa mada ambazo usahihi na ubora wa juu ni muhimu— kama vile za habari, usimamizi wa fedha za binafsi pamoja na maelezo ya afya na sayansi — huwa tunaangazia maudhui ya ubora wa juu kwa kutumia zana mbalimbali. Jinsi inavyoonekana:

Matokeo ya Utafutaji
Tazama Inayofuata
Maelezo ya Afya

Jinsi YouTube Inavyotoa Muktadha wa Ziada

Ili kutoa muktadha wa ziada kuhusu matukio, mada na wachapishaji fulani, tunatumia kidirisha cha maelezo kwenye YouTube, hali hiyo ni kama:

Mada yakini za kihistoria, kisayansi na kiafya
Mada yakini za kihistoria, kisayansi na kiafya

Kwa mada zinazohusiana na taarifa zisizo kweli, tunaweza kukuelekeza katika vyanzo vya wengine ili kukupa muktadha zaidi.

Maudhui sanisi au yaliyobadilishwa
Maudhui sanisi au yaliyobadilishwa

Tunahitaji watayarishi wafumbue maudhui yanayofanana na uhalisia yaliyotayarishwa kwa kutumia maudhui sanisi au yaliyobadilishwa, ikiwa ni pamoja na maudhui yaliyotayarishwa kwa AI Zalishi kisha lebo zitaonekana kwenye video au katika maelezo ya video.

Gundua zaidi

Mfumo wa mapendekezo ya YouTube
Kudhibiti mapendekezo na matokeo ya utafutaji
Kudhibiti data katika YouTube