Wakati tunategemea uwezo wa AI, tungependa kuhakikisha kuwa
tunatumia mbinu sahihi za ulinzi. Sera na bidhaa zetu
zinalenga kulinda na kuwezesha watayarishi wa maudhui katika
enzi ya AI na kudumisha usalama wa jumuiya ya YouTube.
Kama kawaida,
Mwongozo wetu wa Jumuiya
hufafanua kanuni za kufuatwa na maudhui yote — ikiwa ni
pamoja na maudhui yaliyotayarishwa kwa AI — kwenye YouTube.
Pia tuna sera mahususi zinazoelekeza jinsi
tunavyoshughulikia maudhui yaliyotayarishwa kwa AI, ikiwa ni
pamoja na masharti ya ufumbuzi na ya uwekaji lebo.
Ili kusaidia kuwafahamisha watazamaji kuhusu maudhui
wanayotazama, tunawahitaji watayarishi wafumbue ikiwa AI
ilitumika kuhariri au kutayarisha maudhui halisi kwenye
video zao. Lebo za maudhui ya AI yaliyobadilishwa kwa njia
sanisi au kwa uhalisia zinaweza kuonekana kwenye kicheza
video ya Video Fupi au moja kwa moja chini ya video ndefu.
Kwa aina nyingine za maudhui ya AI, lebo itaonekana kwenye
maelezo ya video (k.m., mabadiliko madogo kama vile madoido
ya urembo, wahusika waliohuishwa, n.k.). Ikiwa mtayarishi
hatabainisha kuwa alitumia AI, lakini mifumo yetu itambue,
tunaweza kuweka lebo kiotomatiki. Watayarishi wanaweza
kudhibiti lebo hizi kwenye Studio ya YouTube, lakini
hawawezi kuziondoa ikiwa kuna uwezekano mkubwa kuwa maudhui
hayo yalitayarishwa kwa AI.
Tumesasisha pia viwango vyetu vya faragha vinavyoruhusu
kuomba kuondolewa kwa maudhui yaliyotayarishwa kwa AI au
maudhui mengine sanisi au yaliyobadilishwa ambayo yanaiga
mtu anayeweza kutambulika, ikiwa ni pamoja na uso au sauti
yake kwa kutumia mchakato wetu wa ombi la faragha. Si
maudhui yote yatakayoondolewa kwenye YouTube na tunazingatia
vigezo mbalimbali tunapotathmini maombi haya. Hii inaweza
kujumuisha iwapo maudhui ni ya tashtiti au bezo, iwapo mtu
anayetuma ombi anaweza kutambuliwa kimahususi au iwapo
yanamwangazia kiongozi katika serikali au mtu maarufu, hali
ambayo huenda ikahitaji kutimiza vigezo madhubuti zaidi.