Hakimiliki
YouTube imeundwa ili kuhakikisha kuwa kila mchangiaji katika mfumo wetu anaweza kufanikiwa.
Hii inajumuisha kulinda wenye haki na kuwapa watayarishi utulivu ili waangazie utayarishaji wa maudhui asili.
Hakimiliki
YouTube imeundwa ili kuhakikisha kuwa kila mchangiaji katika mfumo wetu anaweza kufanikiwa.
Hii inajumuisha kulinda wenye haki na kuwapa watayarishi utulivu ili waangazie utayarishaji wa maudhui asili.
Tumewekeza mamilioni ya dola katika kubuni Kifurushi cha Kudhibiti Hakimiliki kilichoundwa ili kushughulikia mahitaji ya mfumo wetu wote na tuna kanuni dhahiri zinazohusiana na hakimiliki.
YouTube imeshirikiana moja kwa moja na wenye haki ili kuhakikisha kuwa maudhui yenye hakimiliki katika mfumo wetu yameidhinishwa na tunatoa zana thabiti ili kuruhusu wenye haki kuiarifu YouTube kuhusu madai ya ukiukaji, ambapo tunayaondoa maudhui kwa mujibu wa sheria. Kuna zana tatu kuu za Kifurushi chetu cha Kudhibiti Hakimiliki:
Madai mengi ya hakimiliki na maombi ya kuondoa kwenye YouTube hutokana na teknolojia yetu ya utambuzi wa kiotomatiki.
Tunawezesha wanaopakia maudhui kuripoti maombi ya kuondoa video yasiyo sahihi na kufuatilia mara ambazo watayarishi hupinga uondoaji na madai ya Content ID katika Ripoti yetu ya Uwazi wa Hakimiliki.
Kati ya zaidi ya madai bilioni 1 ya Content ID yaliyotolewa kati ya Julai 2023 and Desemba 2023, madai yasiyozidi asilimia 1 yamepingwa. Zaidi ya asilimia 65 ya madai yaliyopingwa yaliondolewa kwa sababu mlalamikaji aliondoa dai kwa hiari au hakujibu katika kipindi cha siku 30, hali iliyosababisha dai kuondolewa. (Chanzo)