Mnamo 2007, YouTube ilikuwa na wazo la kipekee - itakuwaje
watayarishi wakipewa sehemu halisi ya mapato
wanayochangia? Kwa kuwagawia moja kwa moja watayarishi,
wasanii na kampuni za vyombo vya habari zaidi ya nusu ya
mapato ya usajili na ya utangazaji, YouTube ilivunja
vikwazo vilivyokuwepo vya uchumaji wa mapato. Hatua hii
ilimpa mtu yeyote fursa ya kukuza biashara na chapa kwa
kuanza kuchuma mapato kwa kubadilisha kile anachopenda
kuwa kazi bunifu.
Sehemu ya mapato yaliyosalia huwekezwa tena kwenye
YouTube, hali inayohakikisha kuwa watayarishi wanapata kwa
urahisi zana bora za utayarishaji, usambazaji na uchumaji
wa mapato.
Miaka ishirini baadaye, mfumo wa kipekee wa ugavi wa
mapato wa YouTube umesalia kuwa usioweza kulinganishwa na
mingine na umesababisha kuibuka kwa mfumo mpya kabisa wa
biashara bunifu.