Uchaguzi

Watumiaji kote duniani huja katika YouTube kupata habari na taarifa kuhusu uchaguzi - iwe ni kupata maelezo yanayoweza kutegemewa kuhusu kupiga kura, wagombeaji na matokeo ya uchaguzi au kuweza kufikia matukio makuu mubashara yanayohusiana na uchaguzi – kama vile mijadala na maonyesho ya matukio ya uchaguzi.

Jinsi YouTube Inavyowaelekeza Watu kwenye Maudhui ya Uchaguzi

Tumejitolea kuwaelekeza watu katika maudhui ya uchaguzi yanayoweza kutegemewa na kuhakikisha kuwa matukio mubashara makuu yanayohusishwa na uchaguzi yanaendelea kupatikana kwa urahisi kwa hadhira pana kwenye mfumo wetu.

Jinsi Sera za YouTube za Uchaguzi Zinavyofanya Kazi

Kwa kuwa mfumo wetu unatumiwa duniani kote, mifumo na sera zetu za uchaguzi hubuniwa na kutekelezwa kwa kuzingatia mtazamo wa jumla - Mwongozo wetu wa Jumuiya hutekelezwa kwenye lugha na mifumo yetu huunganisha wapiga kura katika nchi zote tunakohudumu na habari na taarifa za ubora wa juu kuhusu uchaguzi, ambayo yanawafaa zaidi.

Watumiaji wanapotazama au kutafuta maudhui ya uchaguzi katika YouTube, mfumo wetu wa mapendekezo huonyesha maudhui ya ubora wa juu kwenye matokeo ya utafutaji, ukurasa wa kwanza na kidirisha cha “Tazama Inayofuata”. Kwa hivyo, wapiga kura hupata maudhui ya ubora wa juu kutoka vyanzo mbalimbali vya habari. Pia, ili kupanua ufikiaji wa maudhui mubashara yanayohusiana na uchaguzi, mitiririko mubashara ya matukio makuu yanayohusiana na uchaguzi – kama vile mijadala na maonyesho ya matukio ya uchaguzi –  yanaweza kuonyeshwa katika sehemu ya juu ya ukurasa wa kwanza au ya matokeo ya utafutaji wako unapotafuta video zinazohusiana na matukio mubashara mahususi ya uchaguzi wa kitaifa.

Kuangazia Taarifa za Uraia na Uchaguzi

Kando na vipengele vyetu vya bidhaa vinavyopatikana kila wakati, tunaweza kufanya juhudi zaidi ili kupata taarifa nyakati za matukio muhimu ya kiraia na uchaguzi. Jinsi vipengele hivyo vinavyofanya kazi kwenye bidhaa katika kipindi cha uchaguzi:

Kidirisha cha maelezo ya mgombeaji
Vidirisha vya maelezo ya kupiga kura
Vidirisha vya maelezo ya matokeo ya uchaguzi

Tunaweza pia kuondoa maudhui mahususi kwa kanuni zifuatazo:

1
Kuzuia au kuwakatisha tamaa wapiga kura

Haturuhusu maudhui yanayolenga kupotosha wapiga kura kuhusu wakati, mahali, njia au masharti ya kupiga kura au madai ya uongo yanayoweza kuwafanya watu wakate tamaa zaidi kuhusu kupiga kura.

2
Uigaji

Haturuhusu maudhui yanayolenga kuiga mtu au chaneli, kama vile mgombeaji wa kisiasa au chama chake cha siasa.

3
Masharti ya Kufaa kwa Mgombeaji

Haturuhusu maudhui yanayoendeleza madai ya uongo yanayohusiana na masharti ya kiufundi ya kufaa kwa wagombea viti vya kisiasa na wafanyakazi wa serikali wa sasa waliochaguliwa. Masharti ya kufaa yanayozingatiwa yanalingana na sheria ya kitaifa inayotumika na yanajumuisha umri, uraia au hali muhimu.

4
Uchochezi wa kukatiza

YouTube hairuhusu maudhui yanayowahimiza wengine kukatiza michakato ya kidemokrasia, hii inajumuisha kuzuia au kuingilia utaratibu wa kupiga kura.

5
Maudhui yaliyobadilishwa

YouTube hairuhusu maudhui ambayo yamebadilishwa au kukarabatiwa kwa kutumia teknolojia kwa namna ambayo yanapotosha watumiaji (kwa kawaida kando na klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha) na yanaweza kusababisha madhara mabaya sana.

Tunathibitisha pia kuwa tunapaswa kusawazisha kwa uangalifu maudhui yanayoangazia uchaguzi ili kuhakikisha kuwa tunaruhusu mjadala thabiti wa kisiasa, kwa hivyo wakati mwingine maudhui ambayo huenda yanakiuka sera zetu yanaweza kusalia katika YouTube iwapo yana muktadha wa Kielimu, Hali halisi, Kisayansi au Kisanaa (EDSA).

Katika hali fulani, tunaweza kutoa ruhusa za EDSA za kutofuata kanuni kulingana na maslahi ya umma. Hali hizi zinaweza kujumuisha, kwa mfano, maudhui kama vile wagombea viti vya kisiasa wa kitaifa wakiwa katika kampeni.

Jinsi YouTube Inavyoshughulikia Maudhui ya Uchaguzi Yaliyotayarishwa kwa AI

Kadiri AI inavyoendelea kuwa bora, huenda ikawa vigumu kwa watazamaji kutofautisha kati ya maudhui halisi na sanisi.

Jinsi tunavyoyashughulikia:

  • Pata maelezo zaidi
Ufumbuzi wa Watayarishi
Uwekaji lebo

Jinsi YouTube Inavyodhibiti Utambuzi wa Mapema

Tunajitahidi kuondoa maudhui yanayokiuka sera zetu haraka iwezekanavyo kwa kushughulikia mapema matishio na masuala yanayoibuka kabla yafike au yasambae kwenye mfumo wetu. Timu yetu ya Kituo cha Ufuatiliaji hufuatilia na kutambua mambo mapya ikiwa ni pamoja na tabia mbaya na maudhui yasiyofaa.

Timu ya Usalama na Uaminifu katika YouTube na Kikundi cha Kuchanganua Hatari kwenye Google (TAG) hufanya kazi pamoja ili kutambua shughuli za ushawishi ulioratibiwa katika YouTube na kufunga chaneli na akaunti za wanaoendeleza shughuli hizo — ikiwa ni pamoja na shughuli za udukuzi unaoungwa mkono na serikali kwa lengo la kukatiza michakato ya uchaguzi. Kupitia kikundi cha TAG, tunawatumia washirika wa sekta na vyombo vya sheria taarifa za uchunguzi, mbinu bora na taarifa kuhusu tishio.

Jinsi Utangazaji wa Maudhui ya Siasa kwenye YouTube unavyofanya kazi

Mwongozo wa Jumuiya yetu, Mwongozo wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji na sera za Google Ads hufanya kazi pamoja ili kuhakikisha hali nzuri na salama kwa watumiaji, watayarishi na watangazaji wetu na kusimamia maudhui yanayoonyeshwa katika matangazo kwenye Google — ikiwa ni pamoja na YouTube.

Gundua zaidi

Matukio kabla ya Uchaguzi wa Marekani 2024
Uchaguzi wa Bunge la Umoja wa Ulaya katika YouTube
Jinsi YouTube inavyosaidia uchaguzi wa Bunge la Umoja wa Ulaya 2024
Kusaidia uchaguzi wa Marekani 2024