Kanuni Zetu za Kuwalinda Vijana

Kanuni zifuatazo ni za msingi katika shughuli za YouTube za kuhakikisha mazingira salama na bora zaidi kwa vijana.

Kupitia kanuni hizi, tunatumai kuchangia kwenye mazungumzo muhimu ya wanaounda sera, familia, watafiti na wataalamu kuhusu kujenga mazingira ya intaneti yanayowafaa vijana.

1

Faragha, usalama wa kimwili, afya ya akili na ustawi wa watoto na vijana unahitaji ulinzi maalum mtandaoni.

Kuwalinda watoto na vijana ni jambo la msingi na linapaswa kuwa kiini cha kazi yetu kila wakati na tungependa kuhakikisha kwamba hali yao ya matumizi kwenye jukwaa letu ni bora na salama zaidi.

Pia tuna wajibu wa msingi wa kuelewa mahitaji ya afya ya akili ya vijana, kuunda mikakati ya kulinda mahitaji hayo na kuwa washirika na watetezi wa ustawi wao.

2

Wazazi na walezi wana jukumu muhimu katika kuweka kanuni za matumizi ya mtandaoni kwa familia zao, hasa kwa watoto wao wenye umri mdogo zaidi.

YouTube huwapa wazazi na walezi njia za kubadilisha wapendwavyo hali ya matumizi ya mtandao kwa familia zao. Huwa tunabuni aina mbalimbali za matumizi ya YouTube, vidhibiti vya wazazi, vipengele na mipangilio ya upeo tofauti wa umri, ili familia ziweze kuweka uwiano unaofaa kati ya usimamizi na uhuru kulingana na makuzi yao, ya mtoto au ya kijana wao.

Na kwa sababu hakuna jibu moja linalofaa kwa wote, YouTube inatoa nyenzo, mwongozo na usaidizi ili kuzisaidia familia kufanya uamuzi unaowafaa watoto wao wadogo, vijana walio na umri mkubwa na kila mtoto aliye kati ya hao.

3

Vijana na watoto wote wanastahili kupata bila kulipia, maudhui yanayoambatana na umri na ya ubora wa juu yanayotimiza mahitaji na mambo yanayowavutia.

Huwa tunaweka maudhui yanayoambatana na umri na yenye ubora wa juu yawe yasiyolipiwa na yanayofikiwa na vijana wote. Kamwe hatuonyeshi matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwa watoto na hatufikiri kuwa wengine wanapaswa kuyaonyesha.

Mfumo wetu wa mapendekezo umebuniwa kutoa hali bora na salama zaidi kwa watumiaji wadogo kwenye YouTube. Hali hii husaidia kuwaunganisha na maudhui ya ubora wa juu — yanayotokana na kanuni bora zilizotengenezwa kwa ushirikiano na wataalamu huru wa makuzi ya watoto na nidhamu dijitali— ambayo yanachochea udadisi, mawazo na ubunifu.

4

Mahitaji ya ukuaji wa watoto ni tofauti sana na ya vijana na yanapaswa kuzingatiwa katika hali zao za matumizi mtandaoni.

Mambo yanayowavutia, mahitaji na uwezo wa kimaendeleo hutofautiana kwa kiasi kikubwa kati ya mtoto wa miaka 8, wa miaka 12 na wa miaka 17.

YouTube hushirikiana na wataalamu wa nje katika maudhui ya watoto, ukuaji wa watoto, mafunzo ya kidijitali na uraia kutoka katika nyanja mbalimbali za taaluma, mashirika yasiyolenga faida na za kimatibabu ili kuunda hali za matumizi zinazoambatana na umri zinazosaidia na kuwalinda vijana katika kila hatua ya maisha yao.

5

Kwa kutumia ulinzi stahiki, teknolojia bunifu zinaweza kuwa za manufaa kwa watoto na vijana.

Mara nyingi vijana wadogo huwa watumiaji wa mapema katika uvumbuzi. Tungependa wawe na hali nzuri wanapotumia zana mpya, hivyo tunafanya kazi kutathmini na kupunguza hatari za teknolojia mpya tangu mwanzo.

Huwa tunashirikiana na wataalamu wa sekta, watafiti na wazazi ili kuhakikisha kuwa familia zinaelewa vyema jinsi teknolojia mpya zinaweza kuwasaidia watumiaji wadogo kujifunza, kutayarisha na kukua na pia kuelewa mipaka ya teknolojia hizo.

Gundua zaidi

Watoto na Vijana
Mwongozo wa mazoea mazuri ya muda wa kutumia kifaa kwa vijana, kutoka YouTube na Shirika la Kisaikolojia la Marekani
YouTube na viongozi wa sekta wanatangaza Mpango wa Nidhamu Dijitali kwa Vijana