Sera Zetu

Lengo la YouTube ni kumpa kila mtu fursa ya kujieleza na kuonyesha wote matukio ya ulimwengu — uwazi na uhuru wa kujieleza ni kiini cha lengo hili. Mfumo wetu ni sehemu ambapo tunahimiza mitazamo mipana na hatuogopi mijadala na kutofautiana kimawazo.

Jinsi Mwongozo wa Jumuiya na wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji unavyofanya kazi

Sera zetu hutusaidia kudumisha biashara thabiti ambayo watazamaji, watayarishi na watangazaji wanaweza kutegemea ili kuendelea kustawika kwenye YouTube.

Kama ilivyo kwenye mfumo wowote, wakati mwingine huwa tunakosea. Ndiyo maana rufaa ni sehemu muhimu ya michakato yetu. Watayarishi huarifiwa video zao zinapoondolewa kutokana na ukiukaji wa sera au wanaposimamishwa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube na wanaweza kukata rufaa iwapo hawakubaliani na uamuzi wetu.

Mwongozo wetu wa Jumuiya na Mwongozo wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji ndio unaotusaidia kuleta usawa huu.

Mwongozo wa Jumuiya

Maudhui yanayokiuka mwongozo wetu wa jumuiya huripotiwa na mchanganyiko wa wanadamu na utambuzi wa kiotomatiki — mengi hutambuliwa kiotomatiki — na tunajitahidi sana ili kuhakikisha kuwa maudhui yanayokiuka mwongozo hayatazamwi na watu wengi au hata kutotazamwa kabisa, kabla ya kuyaondoa.

Tunaweza kuruhusu maudhui yenye muktadha dhahiri wa kielimu, kihalisia, kisayansi au kisanaa (EDSA).


Mwongozo wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji

Chapa hututegemea tulinde malengo ya biashara zao wanapotangaza katika YouTube.

Ili kusaidia kutimiza lengo hili, tumeweka mwongozo wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji ambao watayarishi waliojiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) wanapaswa kufuata ili kuonyesha Matangazo katika maudhui kwenye chaneli zao na kuchuma mgawo wa mapato.


Jinsi tunavyowasaidia watayarishi

Tangu 2007, tumekuwa tukiwalipa watayarishi wanaotimiza masharti kila mwezi kupitia mfumo wetu wa ugavi wa mapato, Mpango wa Washirika wa YouTube.

Ili mtayarishi atimize masharti ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, ni lazima atimize viwango vya juu zaidi kwa maudhui anayochapisha katika YouTube. Ni lazima watayarishi wafuate Sera za uchumaji wa mapato kwenye YouTube na huwa tunakagua chaneli ya kila anayetuma ombi kabla ya kumruhusu ajiunge na Mpango wa Washirika wa YouTube. Huwa pia tunakomesha uchumaji wa mapato katika video zinazokiuka Mwongozo wetu wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji na kusimamamisha watayarishi kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube kwa ukiukaji unaojirudia. Kwa kutumia mfumo huu, watayarishi wanapata marupurupu ya muda mrefu ili kuimarisha usalama wa YouTube na kufuata sera zetu.

Jinsi tunavyowasaidia watayarishi
Pia tunawapa Watayarishi zana mbalimbali ili kudhibiti maudhui na jumuiya zao:
Kudhibiti Hali za Utumiaji

Mwongozo wa Chaneli huwasaidia watayarishi kuamua maudhui ambayo wangependa kutayarisha kwenye chaneli zao.

Watayarishi wanaweza kuzuilia maoni ambayo huenda hayafai ili yakaguliwe, kuwaficha watu fulani wasione maudhui, kuzuia maneno, kukabidhi haki za kudhibiti na zaidi.


Jinsi ya kuweka mwongozo wa chaneli
Usimamizi wa Chaneli

Tunawapa watayarishi bidhaa mbalimbali zinazowasaidia kuamua jinsi ya kudhibiti chaneli zao.


Jinsi ya kudhibiti machapisho na maoni
Nyenzo za Faragha na Usalama

Faragha na usalama wa watayarishi katika YouTube ni muhimu kwetu na tunatoa zana na nyenzo mbalimbali ili kuwasaidia.


Jinsi ya kutumia zana za faragha na usalama

Jinsi Washirika wa YouTube pamoja na Wataalamu wa Sekta Wanavyokabili Matumizi mabaya

YouTube hairuhusu maudhui yanayokusudiwa kusifu, kutangaza au kusaidia mashirika yenye itikadi kali au ya kihalifu. Tunategemea vigezo vingi — kama vile uteuzi wa serikali na mashirika fulani ya kimataifa — ili kubainisha ni nini kinajumuisha mashirika ya uhalifu au ya kigaidi.

Sisi pia ni wanachama waanzilishi wa Jukwaa la Mtandaoni la Kimataifa la Kukabili Ugaidi (GIFCT), ambapo tunashirikiana na kampuni nyingine za teknolojia kuzuia maudhui ya kigaidi kwenye wavuti — na kutoa mafunzo na nyenzo nyingine kwa kampuni ndogo zilizo na changamoto kama hizo.

Gundua zaidi

Zana mpya za kuwalinda watayarishi na wasanii
Jinsi tunavyowasaidia watayarishi kufumbua maudhui sanisi au yaliyobadilishwa
Kujaribu njia mpya za kuwapa watazamaji maelezo na muktadha zaidi katika video