Faragha
Hapa YouTube na Google, tunaelewa kuwa watu wanapotumia huduma zetu, wanaamini kuwa tutalinda taarifa zao.
Faragha
Hapa YouTube na Google, tunaelewa kuwa watu wanapotumia huduma zetu, wanaamini kuwa tutalinda taarifa zao.
Tunatii kanuni za faragha za Google, hali inayomaanisha kuwa tunaunda bidhaa zenye faragha iliyodhamiriwa na tunazingatia kwa uangalifu data tunayotumia, jinsi tunavyoitumia na kuilinda. Data yoyote tunayokusanya ili kuwekea mapendeleo huduma zetu kwa watumiaji, ikiwa ni pamoja na mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo, matokeo ya utafutaji yanayowasaidia kugundua watayarishi wanaowapenda, maudhui yanayotimiza mahitaji yao na kuonyesha matangazo yanayofaa hudhibitiwa na mtumiaji katika mipangilio yake ya faragha.
Kufanya hivi huwaruhusu watumiaji kuchagua mambo yanayowafaa ili wadhibiti taarifa binafsi ambazo wameruhusu Google ifikie - ikiwa ni pamoja na kukagua, kupakua na kuhamishia data yao kwenye huduma nyingine au kuifuta kabisa wakati wowote wanapotaka. Sera za faragha za Google huwafahamisha watumiaji kuhusu data tunayokusanya, jinsi tunavyoitumia na kwa nini. Na kamwe hatumuuzii mtu yeyote taarifa binafsi za mtumiaji.
Zana zetu za faragha ni rahisi kutumia na huwawezesha watumiaji wetu kuchagua hali ya utumiaji inayowafaa.