Nenda kwenye maudhui
bango kuu

13 Wanachama Waliopo

2018 Tangu

Kamati ya Ushauri ya Vijana na Familia

YouTube husasisha mara kwa mara hali ya matumizi ya bidhaa na sera zetu za familia kwa kushauriana na wataalamu wa maudhui ya watoto, ukuaji wa watoto, mafunzo ya kidijitali na uraia kutoka katika nyanja mbalimbali za taaluma, mashirika yasiyo ya faida na ya kitabibu. Kamati hii ya ushauri ni mkusanyiko wa wataalamu huru wanaoshauri kuhusu bidhaa, sera na huduma tunazotoa kwa vijana na familia. Kwa pamoja, YouTube na kamati yetu ya ushauri imejikita kukuza mfumo salama, wa ubora wa juu na wenye manufaa unaoboresha maisha ya vijana na familia duniani kote. Gundua ni akina wanaounda jopo letu la wataalamu.

bango kuu

13 Wanachama Waliopo

2018 Tangu

Kutana na Washauri

Gundua tunachofanya kwa ajili ya jumuiya yetu.

Anne Collier

Anne Collier

Mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa shirika la kitaifa lisilo la faida la The Net Safety Collaborative

Mwandishi na mtetezi wa masuala ya vijana Anne Collier ameandika mijadala ya wazi kuhusu vijana na maudhui dijitali tangu mwaka 1997. Yeye ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa shirika la kitaifa lisilo la faida linaloitwa The Net Safety Collaborative (TNSC), ambalo mradi wake mkuu ni huduma za usaidizi kuhusu mitandao ya kijamii mashuleni. Anne alihudumu katika vikosi kazi vitatu vya kitaifa kuhusu usalama wa vijana na Intaneti, ikiwa ni pamoja na kuwa mwenyekiti mwenza wa Kikundi Kazi cha Teknolojia na Usalama wa Mtandaoni cha utawala wa Obama pia katika Kikosi Kazi cha Kiufundi cha Kitaifa Kuhusu Masuala ya Usalama wa Inteneti cha mwaka 2008. Hivi majuzi, alihudumu kwenye Kikosi Kazi cha Taasisi ya Aspen cha mwaka 2013 hadi 2014 kilichohusu Kujifunza na Intaneti.

Allison Briscoe-Smith

Allison Briscoe-Smith

Daktari na mtafiti mwenye utaalamu katika masuala kuhusu Utofauti, Usawa na Ujumuishwaji. Mkuu na mwanzilishi wa Soft River Consultation

Allison Briscoe-Smith ni mwanasaikolojia wa kimatibabu wa watoto aliyeidhinishwa. Ametumia kipindi chote cha kazi yake katika taaluma na uandaaji wa mipango akiangazia zaidi watoto na familia zinazokabiliwa na changamoto za masuala yanayohusiana na haki za kimbari. Yeye ndiye mkuu na mwanzilishi wa Soft River Consultation ambapo huwa anatoa usaidizi, uandaaji wa mitaala, kuwezesha mashirika yanayotaka kuondoa vikwazo vinavyowazuia watu kuhisi kuwa wanastahiki.

Amanda Third

Amanda Third

PhD, Profesa na mwanzilishi wa Mjadala Mtambuka kuhusu Masuala ya Teknolojia na Ustawi nchini Australia katika Chuo Kikuu cha Western Sydney

Profesa Amanda Third (PhD) ni Mtafiti Mwenza katika Taasisi ya Utamaduni na Jamii; Mkurugenzi Msaidizi katika Kituo cha Utafiti cha Vijana na Ustahimilivu katika Chuo Kikuu cha Western Sydney; na Mshiriki wa Kitivo katika Kituo cha Berkman Klein cha Intaneti na Jamii katika Chuo Kikuu cha Harvard (2020-2023). Mtaalamu wa kimataifa katika utafiti shirikishi unaolenga vijana, utafiti wa Amanda unachunguza matumizi ya teknolojia kwa watoto na vijana, ukilenga makundi yaliyotengwa na mbinu zinazozingatia haki. Ameongoza miradi ya utafiti inayolenga watoto kuelewa matumizi yao ya teknolojia katika zama za kidijitali kwenye zaidi ya nchi 70, akifanya kazi na watoto, vijana pamoja na washirika ambao ni makampuni, serikali na mashirika yasiyo ya faida.

Ellen Selkie

Ellen Selkie

Profesa Msaidizi katika Tiba za Vijana Walio katika Umri wa Kubalehe katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison

Dkt. Selkie alitunukiwa shahada yake ya Utabibu na Uzamili katika Afya ya Umma (MPH) kutoka Shule ya Tiba na Afya ya Umma ya Chuo Kikuu cha Wisconsin ambapo kwa sasa yeye ni Profesa Msaidizi katika kitengo cha Matibabu ya Watoto. Kazi yake ya utabibu inahusisha malezi maalum yanayolenga udhibiti wa makuzi ya vijana wadogo walio katika umri wa balehe. Kama mtaalamu wa afya, Dkt. Selkie anatumai atapunguza shughuli hasi za mitandao ya kijamii na kuchochea shughuli chanya za matumizi ya mitandao ya kijamii kwa vijana waliotengwa, hasa vijana walio katika jamii za wachaje kijinsia na utambuisho wa ngono.

Jessica Piotrowski

Jessica Piotrowski

PhD, Profesa, na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Watoto, Vijana na Maudhui katika Chuo Kikuu cha Amsterdam

Dkt. Jessica Taylor Piotrowski ni Profesa katika Shule ya Utafiti ya Mawasiliano ya Amsterdam (ASCoR) katika Chuo Kikuu cha Amsterdam (UvA) ambapo yeye ni Mwenyekiti wa Mpango wa Mawasiliano katika Jamii Ya Kidijitali. Utafiti wa Dkt. Piotrowski unauliza jinsi tofauti za mtu binafsi, kijamii na kitamaduni huathiri uchaguaji wa maudhui kwa watoto, matumizi, na namna wanavyochanganua mambo na athari zinazoweza kutokea, kwa kuzingatia hasa miktadha inayounga mkono matumizi ya maudhui dijitali kwa vijana.

Justin Patchin

Justin Patchin

PhD, Profesa, Mwanzilishi Mwenza na Mkurugenzi Mwenza wa Kituo cha Utafiti wa Uchokozi wa Mtandaoni katika Chuo Kikuu cha Wisconsin, Eau Claire

Profesa wa sheria za jinai katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Eau Claire. Utafiti wa Justin Patchin unachunguza uhusiano uliopo kati ya vijana wadogo na teknolojia, kwa kuzingatia hasa uchokozi wa mtandaoni, utumiaji wa mitandao ya kijamii na utumaji wa ujumbe wa ngono. Yeye husafiri mara kwa mara ili kuwafunza wakufunzi, washauri, maafisa wa kutekeleza sheria, wazazi na vijana kuhusu jinsi ya kuzuia matumizi mabaya ya teknolojia.

Kareem Edouard

Kareem Edouard

Profesa Msaidizi wa Shule ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Drexel

Kareem Edouard ni Profesa Msaidizi wa Teknolojia za Kujifunza katika Shule ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Drexel na mshauri wa maudhui wa The Ole Greens Group. Dkt. Edouard alitunukiwa Ph.D. katika mpango wa Kujifunza Sayansi na Teknolojia katika Shule ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Stanford. Eneo lake la utafiti limejikita kwenye kuelewa uhusiano uliopo kati ya mbari na tamaduni na ushiriki wa wanafunzi wenye asili ya Afrika katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi Sanaa na Hisabati (STEAM). Kazi ya ushauri ya Dkt. Edouard imejikita kwenye ubunifu na utayarishi wa maudhui unaosisitiza kuhusu umuhimu wa utamaduni na ujumuishwaji pamoja na mikakati ya kujifunza.

Mimi Ito

Mimi Ito

Profesa katika masuala ya Makazi, Sayansi ya Kompyuta katika Chuo kikuu cha California, Irvine

Mimi Ito ni mwanaanthropolojia wa kitamaduni wa utamaduni wa kidijitali na mtetezi wa mafunzo yaliyounganishwa ambayo yanazingatia vijana, vitu wanavyopenda, shughuli za kujifanyia na za kijamii. Yeye ndiye mwanzilishi mwenza wa Connected Camps, shirika la faida ambalo hutoa fursa za ubunifu za mtandaoni kwa watoto katika nyanja zote za maisha. Utafiti wa miongo kadhaa kuhusu magwiji, wachezaji, mashabiki, wanaharakati na wasanii umemshawishi Ito kwamba watoto hujifunza vyema zaidi wanapofuatilia mambo wanayovutiwa nayo na watu wanaowahamasisha.

Sameer Hinduja

Sameer Hinduja

PhD, Profesa, Chuo Kikuu cha Atlantic cha Florida; Mkurugenzi Mwenza, Kituo cha Utafiti wa Uchokozi wa Mtandaoni; Mwanzilishi Mwenza na Mhariri Mwenza wa Jarida la Kimataifa la Kudhibiti Uchokozi

Dkt. Sameer Hinduja anatambulika kimataifa kwa kazi yake kubwa kuhusu uchokozi wa mtandaoni na matumizi salama ya mitandao ya kijamii. Ameandika vitabu saba na utafiti wake umetajwa zaidi ya mara 20,000 katika nyanja mbalimbali. Dkt. Hinduja mara kwa mara hutoa ufafanuzi wa kitaalamu kwa vyombo vya habari pia hufunza wanafunzi, wakufunzi, wazazi, wataalamu wa afya ya akili na wanateknolojia njia bora za kukuza matumizi chanya ya teknolojia.

Sarah M. Coyne

Sarah M. Coyne

PhD, Profesa wa Masuala ya Ustawi wa Binadamu, Shule ya Maisha ya Familia, Chuo Kikuu cha Brigham Young

Dkt. Sarah M. Coyne ni Profesa wa masuala ya Ustawi wa Binadamu kwenye Shule ya Maisha ya Familia katika Chuo Kikuu cha Brigham Young. Mara kwa mara, yeye huzungumza na familia na vijana kuhusu utumiaji wa mbinu na majukwaa ya mawasiliano kwa njia bora. Alipokea shahada ya kwanza ya Sayansi ya Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Utah na Shahada yake ya Uzamifu ya Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Central Lancashire jijini Preston, Uingereza. Masuala anayoyatafiti yanahusisha mbinu na majukwaa ya mawasiliano, ugomvi, jinsia, afya ya akili na ukuaji wa watoto. Dkt. Coyne ana zaidi ya machapisho 200 kuhusu mada hizi na nyinginezo. Ana watoto watano na anaishi Utah.

Sun Sun Lim

Sun Sun Lim

Profesa wa Mawasiliano na Teknolojia katika Chuo Kikuu cha Usimamizi cha Singapoo

Sun Sun Lim ni Profesa wa Mawasiliano na Teknolojia katika Chuo Kikuu cha Usimamizi cha Singapoo. Ameandika kwa upana kuhusu matumizi ya vyombo vya habari na familia, ikiwa ni pamoja na kitabu cha Malezi Yaliyopitiliza: Kulea Watoto katika Zama za Kidijitali (Oxford University Press, 2020) na Mawasiliano kwa njia ya Vifaa vya Mkononi na Familia (springer, 2016). Anahudumu katika Baraza la Elimu kwa Vyombo vya Habari na kuanzia mwaka 2018-2020 alikuwa Mbunge Aliyeteuliwa kwenye Bunge la Singapoo ambapo alikuwa akitetea haki dijitali kwa watoto na matumizi yanayofaa ya AI na kushiriki data.

Thiago Tavares

Thiago Tavares

Mwanzilishi na Rais wa SaferNet

Thiago Tavares ni mwanzilishi na rais wa SaferNet, Kituo cha Intaneti Salama ambacho kimedumu kwa miaka 18 nchini Brazili. SaferNet ndiyo shirika la kwanza kabisa lisilo la kiserikali (NGO) nchini Brazili kuanzisha mbinu ya kushirikisha wadau mbalimbali kulinda watoto na kukuza uelewa wa haki za binadamu katika mazingira dijitali. Tangu mwaka 2005 SaferNet imekuwa ikisimamia Nambari ya Simu ya Huduma za Usaidizi ya Kitaifa na Kituo cha Usaidizi na Uhamasishaji Elimu ya Usalama Mtandaoni cha Brazili. Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita kazi zake kuhusu usalama wa watoto, usalama wa kidijitali na udhibiti wa matumizi ya intaneti zimewasilishwa katika zaidi ya nchi 30, yakiwemo matoleo tisa ya UN IGF.

Yalda T. Uhls

Yalda T. Uhls

Mkurugenzi Mwanzilishi wa The Center for Scholars & Storytellers na Profesa Msaidizi wa Chuo Kikuu cha UCLA

Yalda T. Uhls ni mwanasayansi wa utafiti anayetambulika kimataifa aliyeshinda tuzo, profesa msaidizi wa chuo kikuu cha UCLA na mwandishi wa kitabu cha Media Moms & Digital Dads: A Fact not Fear Approach to Parenting in the Digital Age. Yeye ndiye mkurugenzi mwanzilishi wa The Center for Scholars & Storytellers, shirika la utafiti katika chuo cha UCLA, ambalo linashughulikia kuondoa utofauti uliopo kati ya utafiti wa sayansi ya jamii na utayarishaji wa maudhui ili kusaidia uandaaji wa simulizi zenye uhalisia na zinazojumuisha vijana. Ujuzi wa Dkt. Uhls kuhusu jinsi ambavyo maudhui ya vyombo vya habari yanavyotayarishwa na sayansi ya jinsi ambavyo maudhui huathiri watoto hudhihirisha mtazamo wake wa kipekee.

Vielelezo

Gundua jinsi YouTube inavyoshirikiana na wataalamu ili kubuni hali ya utumiaji ya ubora wa juu kwa watazamaji walio na umri mdogo.

Kuunda mapendekezo ya maudhui ili kukidhi mahitaji ya kipekee ya vijana na vijana wadogo

Kulingana na ushirikiano wetu na wataalamu, YouTube imetekeleza kanuni za ulinzi kwa watazamaji vijana na vijana wadogo ili kupunguza mapendekezo yanayorudiwa ya video zinazohusiana na mada fulani.

Pata maelezo zaidi

Jinsi kanuni za ubora wa maudhui ya YouTube zinavyosaidia watayarishi kukuza ubunifu na udadisi wa watoto

Kanuni zetu za ubora ambazo zimeundwa kwa kushirikiana na wataalamu, huwaongoza watayarishi kutayarisha maudhui yanayoboresha, yanayoshirikisha na ya kuvutia kwa ajili ya watoto na familia.

Pata maelezo zaidi