Mwongozo wa Jumuiya
Mwongozo wa Jumuiya yetu ni mambo tunayoruhusu na ambayo haturuhusu kwenye YouTube. Upo ili tuweze kulinda jumuiya dhidi ya mambo kama vile maudhui hatari, unyanyasaji na ulaghai. Hutumika kwa kila mtu, na kwa aina yote ya maudhui kwenye YouTube - kama vile video, maoni, viungo na vijipicha.
Hakimiliki
Tumebuni nyenzo kadhaa ili kusaidia Watayarishi kuelewa hakimiliki, kulinda maudhui yao yaliyo na hakimiliki na kuepuka kukiuka sheria za hakimiliki.
Sera za uchumaji wa mapato
Mpango wa Washirika wa YouTube huwezesha Watayarishi kupata pesa kupitia vituo vyao. Ili kuwa Mshirika wa YouTube, lazima Watayarishi wafuate sera zetu za uchumaji wa mapato. Sera hizi zinanuiwa kuzawadi Watayarishi ambao wanachangia vyema kwenye jumuiya kupitia maudhui halisi. Watayarisi wanaotimiza masharti ambao wangependa kuchuma mapato kwenye maudhui yao kwa kuonyesha matangazo wanahitaji kufuata Mwongozo wa Maudhui Yanyofaa Watangazaji mbali na Sera zetu pana za Uchumaji wa Mapato.
Uondoaji halali
Kwa sababu YouTube inapatikana kote duniani, tumeweka michakato ya kutii sheria za mahali ulipo.