Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube hupata pesa kwa njia gani?

Chanzo kikuu cha mapato ya YouTube ni utangazaji. Pia, tunapata pesa kutoka kwa biashara zetu za usajili wa kila mwezi kama vile YouTube Premium. Tumebuni pia zana za kusaidia Watayarishi wanaotimiza vigezo kupata pesa kupitia njia nyingine kadhaa kama vile Super Chat, uanachama katika kituo na bidhaa. Katika hali nyingi, Watayarishi na YouTube hugawana mapato yanayozalishwa kutokana na vituo hivi.

Kugawa mapato

YouTube hugawa vipi mapato ya usajili na utangazaji kwa Watayarishi?

Chanzo kikuu cha mapato ya YouTube ni utangazaji, unaowezesha biashara kupata hadhira zinazofaa na kukuza chapa zake.

Watayarishi ambao ni sehemu ya Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) wanaweza kupokea mapato ya utangazaji.

Tunapata pia pesa kutoka kwa biashara zetu za usajili wa kila mwezi kama vile YouTube Premium. Kupitia YouTube Premium, wanachama wanaweza kufurahia video yoyote kwenye YouTube bila matangazo huku wakiendelea kuwasaidia Watayarishi. Kwa sasa, mapato kutoka ada za uanachama wa YouTube Premium husambazwa kwa Watayarishi kulingana na kiasi cha maudhui yao kinachotazamwa na wanachama.

YouTube huhakikisha vipi ufanisi wa Watayarishi huku ikihakikisha kuwa matangazo yanaonyeshwa kwenye maudhui bora?

Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, tumechukua hatua za kuboresha masharti yetu ya uchumaji wa mapato kupitia matangazo ili kuzawadi tu Watayarishi wanaoaminika zaidi wanaotunga maudhui halisi.

Hata hivyo, utangazaji si njia pekee ya Watayarishi kupata pesa kwenye YouTube. Tunasaidia Watayarishi kila wakati kushiriki hadithi zao, kuzidisha uhusiano na mashabiki wao, na kupata pesa zaidi. Katika kipindi cha miaka chache iliyopita, tumebuni na kutoa zana kadhaa ili kusaidia Watayarishi wanaotimiza masharti, walio kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, kupata njia za ziada za kuchuma pesa kama vile Super Chat, uanachama katika kituo, bidhaa na YouTube BrandConnect. Kama ilivyo kwenye utangazaji, Watayarishi na YouTube hugawana mapato kutoka kwenye bidhaa hizi.

Je, YouTube hutuzwa ili kutangaza maudhui yenye utata kwa nia ya kuongeza muda wa kutazama na kuchuma mapato?

Lengo letu kuu ni uwajibikaji - wala si ushirikiano - na kila kitu tunachofanya, sisi huzingatia kigezo hicho. Kwa kawaida watangazaji hawapendi kuhusishwa na maudhui yenye utata au nyeti kwenye YouTube - kama ilivyobainishwa kwenye Mwongozo wetu wa Maudhui Yanayofaa Watangazaji. Maudhui haya, ingawa wakati mwingine yanafaa kuwa kwenye YouTube kulingana na Mwongozo wa Jumuiya yetu, wakati mwingine hayafai watangazaji wetu. Madhara kwa watumiaji na chapa huzidi manufaa mengine yote.