Nenda kwenye maudhui
Ahadi Zetu

Tunavyoshughulikia Maudhui Yanayotayarishwa kwa AI

YouTube hushughulikiaje AI zalishi kwa kuwajibika?

AI zalishi tayari imeanza kubadilisha njia ambazo watayarishi wanaweza kutumia kujieleza – iwe ni kuchangia mawazo au kujaribu zana za muziki. Tunafurahi kuwa kwenye mstari wa mbele wa kuongeza ufikiaji wa vipengele hivi ili kumsaidia kila mtu atayarishe maudhui. Katika YouTube, uvumbuzi na uwajibikaji ni vitu viwili vinavyoambatana na tunapotazamia kuona jinsi watayarishi wetu wanavyoendelea kutumia AI katika mfumo wetu, uwajibikaji utaendelea kuwa sehemu ya msingi ya shughuli zetu zote.

Mwongozo wetu wa Jumuiya utaendelea kufafanua kanuni za kufuatwa na maudhui yote kwenye mfumo. Tumekuwa tukiondoa na tutaendelea kuondoa maudhui sanisi au yaliyobadilishwa yanayokiuka sehemu yoyote ya Mwongozo wetu wa Jumuiya, ikiwa ni pamoja na sehemu zinazokataza matamshi ya chuki, maudhui ya kuogofya au ya vurugu na unyanyasaji.

Tunaamini kuwa ni muhimu kwa kila mtu kudumisha mfumo bora wa maelezo kwenye YouTube na tumezindua hali za utumiaji wa bidhaa na sera mpya ili kutimiza wajibu wetu wa kujumuisha AI kwa ujasiri na uwajibikaji.

Hii inajumuisha:

  • Zana za uwazi za maudhui sanisi au yaliyobadilishwa: Zana kwenye Studio ya Watayarishi ili kusaidia watayarishi kuripoti wakati maudhui yao yamebadilishwa au ni sanisi kwa kiwango kikubwa na yanaonekana kuwa halisi, ikiwa ni pamoja na AI zalishi. Watayarishi wanatakiwa kufumbua maudhui haya wakati yanafanana uhalisia, kumaanisha kuwa mtazamaji anaweza kufananisha kwa urahisi kile kinachoonyeshwa na mahali, tukio au mtu halisi. Kulingana na ufumbuzi wa mtayarishi, lebo zitaonekana kwenye maelezo ya video na ikiwa maudhui yanahusiana na mada nyeti kama vile afya, habari, uchaguzi au fedha, pia tutaonyesha lebo kwenye video yenyewe katika dirisha ya kichezaji.

Fedha

Lebo ya kicheza video

Kusalimiana kwa mkono

Lebo ya maelezo ya video

Ingawa tunatarajia watayarishi wafumbue wenyewe wanapotumia maudhui sanisi au yaliyobadilishwa kwenye video zao, huenda pia tukaweka lebo kwenye baadhi ya video katika hali ambazo ufumbuzi huu haujawekwa, hasa wakati maudhui yanajadili maudhui nyeti yaliyotajwa hapo juu.

  • Kutumia teknolojia ya AI zalishi ili kuimarisha udhibiti wa maudhui: AI zalishi tayari inatusaidia kupanua kwa haraka seti ya maelezo ambayo viainishi vyetu vya AI vimefunzwa, hali ambayo inatuwezesha kutambua na kupata maudhui mabaya kwa haraka zaidi. Kasi na usahihi ulioboreshwa wa mifumo yetu pia unatuwezesha kupunguza kiwango cha maudhui hatari kinachowafikia wahakiki wetu wanadamu.

Hizi ni baadhi tu ya hatua za kwanza tunazochukua katika mchakato unaoendelea na tutaendelea kufanya mabadiliko na kuboresha hatua kwa hatua, ili kuhakikisha kwamba tunasawazisha manufaa makubwa ambayo teknolojia hii inatoa na kudumisha usalama wa jumuiya yetu katika wakati huu muhimu.