Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

YouTube imeshughulikia vipi janga la dunia la COVID-19?

Tangu kuzuka kwa COVID-19, YouTube imeendelea kujitolea kusaidia watu kufikia habari za kuaminika za afya kwenye mfumo wetu. Tumeshughulikia COVID-19 kwa kubuni sera, nyenzo na bidhaa ambazo tumewekezea kwa miaka michache iliyoptia ili kutimiza wajibu wetu. Pia tumezindua miradi kote duniani ili kuwasaidia watumiaji kuendelea kujifunza na kuwasiliana tunapozoea dunia inayobadilika.

Kushughulikia COVID-19

YouTube inaunganisha vipi watumiaji na maudhui yanayoaminika huku ikipunguza maelezo ya kupotosha?

Katika miaka michache iliyopita, tumeongeza juhudi zetu za kulinda jumuiya ya YouTube dhidi ya maudhui hatari. Pia, hivi ndivyo tunavyoshughulikia maudhui yanayohusiana na COVID-19 kwenye YouTube. Tunakuza vyanzo vya kuaminika, kuondoa maelezo ya kupotosha na kupunguza kuenea kwa maudhui yanayokaribia kukiuka sera ili jumuiya yetu iweze kupata maelezo muhimu na kwa wakati unaofaa katika kipindi hiki kigumu.

Kukuza vyanzo vya kuaminika

Tunaonyesha vidirisha vya maelezo vinavyounganisha kwa maafisa wa afya wanaofaa duniani kote na karibu nawe kwenye ukurasa wetu wa kwanza na kwenye vidirisha vinavyoonekana kwenye video na utafutaji kuhusu COVID-19. Kwa jumla, vidirisha hivi vimekuwa na zaidi ya maonyesho bilioni 400.

Janga la COVID-19 haliathiri tu afya ya kimwili - linaweza pia kuathiri afya ya akili. Ili kusaidia watu wafikie maelezo ya kuaminika kwa urahisi, katika baadhi ya nchi au maeneo, tumezindua vidirisha vya taarifa za afya kuhusu mfadhaiko na mzongo wa mawazo na kujichunguza kwenye Utafutaji katika YouTube. Tunajitahidi kufanya vidirisha hivi vipatikane katika nchi au maeneo zaidi.

Kama mwendelezo wa juhudi zetu za kukabili maelezo ya kupotosha kuhusu COVID-19, tulisasisha vidirisha vyetu vya taarifa kuhusu COVID-19 ili kujumuisha viungo vya taarifa kuhusu chanjo ya COVID-19. Vidirisha vilivyosasishwa vinaweza kuonekana kwenye matokeo ya utafutaji na kwenye kurasa za kutazama zinazohusiana na COVID-19 au chanjo za COVID-19. Vidirisha vilivyosasishwa vinanuiwa kusaidia watumiaji kupata maelezo mengine ya kuaminika kuhusu chanjo ya COVID-19 na si uamuzi kuhusu usahihi wa video yoyote.

Pia tumechangia hesabu ya matangazo kwa serikali na mashirika yasiyo ya serikali ili kusaidia ujumbe kuhusu COVID-19 uonekane zaidi kwenye YouTube.

Tunasaidia watumiaji kupata taarifa mpya kwa kuwaelekeza kwenye vyanzo vya kuaminika. Katika miezi michache ya kwanza ya COVID-19, YouTube ilikuwa imezindua rafu ya habari ya COVID-19 iliyoonyesha video zinazofaa kutoka vyanzo vya kuaminika vya habari na afya kwenye ukurasa wa kwanza.

Kuondoa maelezo ya kupotosha

Kadri hali ya COVID-19 inavyobadilika, tumeshirikiana kwa karibu na mamlaka za afya katika eneo na duniani ili kuhakikisha kuwa ufafanuzi na utekelezaji wa sera zetu unaweza kuondoa maudhui yenye hatari kubwa au madhara hatari. Sera zetu haziruhusu, kwa mfano, maudhui yanayopinga uwepo wa Virusi vya Korona au yanayohimiza matumizi ya suluhu za nyumbani badala ya matibabu. Haturuhusu pia maudhui ambayo yanapinga umuhimu wa ushauri kutoka mamlaka za afya katika eneo au kote duniani kuhusu umbali wa kutengana, yanayoweza kufanya watu watende kinyume cha mwongozo huo.

Mnamo Oktoba 2020, tulipanua sera yetu kuhusu maelezo ya kupotosha ya matibabu ya COVID-19 ili kuondoa maudhui kuhusu chanjo, yanayokinzana na yanayotoka kwenye mamlaka za afya, kama vile Vituo vya Kudhibiti Ugonjwa au Shirika la Afya Duniani.

Kupunguza kuenea kwa maudhui yanayokaribia kukiuka sera

Maudhui yanayokaribia — lakini hayakiuki — Mwongozo wa Jumuiya yetu ni asilimia moja ya maudhui yanayotazamwa kwenye YouTube nchini Marekani. Mnamo 2019, tulianza kupunguza mapendekezo ya maudhui yanayokaribia kukiuka sera au video zinazoweza kupotosha watumiaji kwa njia hatari. Kazi hii imekuwa ya msingi katika kuhakikisha kuwa tunapunguza kuenea kwa maudhui yanayokaribia kukiuka sera, yanayohusiana na COVID-19 kwenye tovuti yetu.

YouTube imewasaidia watu vipi kuendana na mabadiliko duniani?

Kwa muda mfupi, COVID-19 imebadilisha jinsi watu wanavyoishi. Kuanzia kwa wazazi, walimu, wafanyakazi wa mbali, tunabuni nyenzo ili kusaidia watumiaji kuzoea hali zisizo za kawaida wanapodumisha umbali wa kutengana.

Kusoma kwa mbali

Shule zilipofungwa na familia kujikuta nyumbani. Tulizindua Learn@Home na kuboresha Kituo cha Kujifunza kwenye YouTube ili kusaidia wazazi na walezi kuendeleza masomo ya familia kwa kutumia maudhui na shughuli za ziada za masomo. Kuanzia Khan Academy hadi Edelvives hadi Kok Bisa, nyenzo hizi huonyesha maudhui kuhusu hesabu, sayansi, historia na sanaa kutoka kwenye vituo maarufu vya mafunzo. Kwa sasa, maudhui kwenye tovuti hii yanapatikana katika Kiingereza, Kiitaliano, Kifaransa, Kikorea, Kihispania, Kijerumani na Kijapani.

Kuendelea kuwasiliana

Tumepata njia za kusaidia watumiaji wetu kuendelea kumakinika, kuhamasishwa na kuburudishwa huku wakifuata mwongozo wa afya ya umma. Mnamo Machi 2020, tulizindua Mradi wa #Nami uliohimiza watumiaji kufuata mwongozo wa umbali wa kutengana. Mradi huu uliendelea mwezi wa Machi hadi Aprili 2020 na ulichapishwa kwenye masoko 63 na ulishirikiana na zaidi ya wasanii na watayarishi 700.

Tangu kuanza kujitenga duniani, watu wameenda kwenye YouTube ili kuwasiliana kupitia mitiririko ya moja kwa moja. Ili kusaidia hili, tulibuni na kushiriki Mwongozo wa Kutiririsha Moja kwa Moja and Mwongozo wa Matukio Dijitali na washirika kote duniani ili kuwezesha watayarishi na mashirika zaidi kudumisha mawasiliano ya kielektroniki tunapodumisha umbali.

YouTube inasaidia vipi kuhimiza usaidizi na kurejea kwa shughuli?

Kadri serikali na jumuiya ya kisayansi inavyofanya kazi haraka ili kudhibiti na kukabili athari ya janga, YouTube inachangia nyezo na usaidizi ili kusaidia kuwezesha viongozi wa jumuiya ya sayansi na matibabu kulinda watu na kurejesha hali ya kawaida ya jamii.

Tunatangaza na kusaidia juhudi za kuchangisha pesa zinazoongozwa na watayarishi wa YouTube na wasanii ili kusaidia miradi kadhaa inayohusiana na janga la COVID-19 kwa kuweka fedha za ruzuku kote duniani na kutoa uwezo mpana wa kufikia vipengele vya YouTube kama vile lebo yetu ya mchango na kitufe cha kuchanga.