Nenda kwenye maudhui
Kanuni na sera

Mwongozo wa Jumuiya

Mwongozo wa Jumuiya

Muhtasari

Mwongozo wa Jumuiya yetu umebuniwa ili kuhakikisha kuwa jumuiya yetu inaendelea kulindwa. Hubainisha kinachoruhusiwa na kisichoruhusiwa kwenye YouTube na hutumika katika aina zote za maudhui kwenye mfumo wetu, ikiwa ni pamoja na video, maoni, viungo na vijipicha.

Utapata orodha kamili ya Mwongozo wa Jumuiya yetu hapa chini:

Tunabuni sera mpya na kusasisha zilizopo kwa njia gani?

Kila mojawapo ya sera zetu hutungwa kwa makini ili iwe yenye msimamo, iwe na maelezo ya kutosha na iweze kutumiwa kwenye maudhui kutoka kote duniani. Hubuniwa kwa ushirikiano na wataalamu wengi wa sera, na wa nje ya sekta, pia Watayarishi wa YouTube. Sera mpya hufanyiwa mabadiliko mengi kabla ya kuchapishwa ili kuhakikisha kuwa timu yetu ya wakaguzi kote duniani inaweza kuzitumia kwa njia sahihi na bila mabadiliko.

Kazi hii ni endelevu na tunakagua sera zetu kila wakati ili kuelewa jinsi tunavyoweza kusawazisha kati ya kulinda jumuiya ya YouTube na kumpa kila mtu fursa ya kujieleza.

YouTube hutambua vipi maudhui yanayokiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu?

Kutokana na mamia ya saa za maudhui mapya yanayopakiwa kwenye YouTube kila dakika, tunatumia mseto wa watu na mashine kujifunza ili kutambua maudhui yenye matatizo kwa haraka. Teknolojia ya mashine kujifunza ni bora katika kutambua mitindo, inayotusaidia kupata maudhui yanayofanana na maudhui mengine ambayo tayari tumeondoa, hata kabla hayajatazamwa.

Pia tunatambua kuwa njia ya haraka zaidi ya kuondoa maudhui ni kukisia matatizo kabla yaibuke. Kituo chetu cha Upelelezi hufuatilia habari, mitandao jamii na ripoti za watumiaji ili kutambua mitindo mipya ya maudhui yasiyofaa na hujitahidi kuhakikisha kuwa timu zetu zimejiandaa kuyashughulikia kabla yawe matatizo makubwa.

Je, kuna njia ambayo jumuiya pana inaweza kuripoti maudhui hatari?

Ingawa tumejitahidi kuendelea kupunguza kuonekana kwa video zinazokiuka sera zetu na tumewapa zaidi ya watu 10,000 jukumu la kutambua, kukagua na kuondoa maudhui yanayokiuka mwongozo wetu, jumuiya ya YouTube pia ina jukumu muhimu katika kuripoti maudhui inayofikiri kuwa hayafai.

  • Ukiona maudhui ambayo unafikiri kuwa yanakiuka Mwongozo wa Jumuiya, unaweza kutumia kipengele chetu cha kuripoti ili kutuma maudhui yakaguliwe.

  • Tulibuni Mpango wa Wapigaripoti wa Kuaminika kwenye YouTube ili kutoa michakato imara ya kuripoti maudhui kwa mashirika yasiyo ya serikali (NGO) yaliyo na utaalamu katika masuala ya sera, taasisi za serikali na watu mahususi walio na viwango vya juu vya kuripoti kwa usahihi. Washirika hupokea mafunzo kuhusu sera za YouTube na wana njia ya moja kwa moja ya kuwasiliana na wataalamu wetu wa Uaminifu na Usalama. Video zinazoripotiwa na Wapigaripoti wa Kuaminika haziondolewi kiotomatiki. Hukaguliwa na wakaguzi sawa na wanaokagua video zinazoripotiwa na mtumiaji mwingine yeyote, lakini tunaweza kuharakisha ukaguzi unaofanywa na timu zetu. NGO pia hupokea mafunzo ya mara kwa mara kuhusu sera za YouTube.

YouTube huchukua hatua gani dhidi ya maudhui yanayokiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu?

Mifumo ya mashine kujifunza hutusaidia kutambua na kuondoa taka kiotomatiki na pia kuondoa nakala zinazopakiwa za maudhui ambayo tayari tumekagua na kubaini kuwa yanakiuka sera zetu. YouTube huchukua hatua kwenye video nyingine zinazoripotiwa baada ya kukaguliwa na wakaguzi waliohitimu. Wanakagua kama maudhui yanakiuka sera zetu na kulinda maudhui yaliyo na lengo la elimu, hali halisi, sayansi au sanaa. Timu za wakaguzi wetu huondoa maudhui yanayokiuka sera zetu na kuweka vikwazo vya umri kwenye maudhui ambayo huenda hayafai hadhira zote.

Maonyo kwa Kukiuka Mwongozo wa Jumuiya

Wakaguzi wetu wakiamua kuwa maudhui yanakiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu, tutaondoa maudhui na kutuma arifa kwa Mtayarishi. Mtayarishi anapokiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu mara ya kwanza, atapokea onyo bila adhabu kwenye kituo. Baada ya onyo moja, tutatoa onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye kituo na akaunti itakuwa na vikwazo vya muda ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kupakia video, kutotiririsha moja kwa moja na kutoonyesha hadithi kwa muda wa wiki moja. Vituo vinavyopokea maonyo matatu ndani ya kipindi cha siku 90 vitafungwa. Vituo ambavyo vinalenga kukiuka sera zetu au vina hali moja ambapo vilitumia mfumo vibaya zaidi, havitapitia mchakato wetu wa maonyo na vitafungwa. Mtayarishi anaweza kukata rufaa dhidi ya maonyo na matukio yote ya kufungwa kwa kituo iwapo anaamini kuwa tulifanya makosa, ili timu zetu zikague upya uamuzi wetu.

Kuweka Vikwazo vya Umri kwenye Maudhui

Wakati mwingine maudhui hayakiuki Mwongozo wa Jumuiya yetu, lakini huenda hayafai watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18. Katika hali hizi, timu yetu ya ukaguzi itaweka vikwazo vya umri kwenye video hiyo ili isionekane kwa watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18, watumiaji walioondoka katika akaunti, au wale ambao wamewasha Hali yeye Mipaka. Watayarishi wanaweza pia kuchagua kuweka masharti ya umri kwenye maudhui yao wenyewe wanapoyapakia iwapo wanafikiri kuwa hayafai hadhira za walio na umri mdogo.