Nenda kwenye maudhui
Vipengele vya bidhaa

Utafutaji kwenye YouTube

Utafutaji kwenye YouTube

Kwa kuwa kuna zaidi ya saa 500 za maudhui yanayopakiwa kwenye YouTube kila dakika, inaweza kuwa vigumu kupata unachohitaji bila usaidizi wa kupitia video zote. Mfumo wa YouTube wa kupanga matokeo ya utafutaji hufanya hivyo kwa kupitia video nyingi ili kupata matokeo muhimu na yanayofaa zaidi hoja yako ya utafutaji na kuyaonyesha kwa njia inayokusaidia kupata unachotafuta.

Katika timu ya Utafutaji kwenye YouTube, tunavipa kipaumbele vipengele vitatu vikuu ili kukupa matokeo bora zaidi ya utafutaji: ufaafu, ushirikishi na ubora. Vipengele hivi vitatu hupewa umuhimu tofauti kulingana na aina ya utafutaji. Ili kukadiria ufaafu tunaangalia vigezo vingi, kama vile kiasi ambacho mada, lebo, maelezo na maudhui ya video yanalingana na hoja yako ya utafutaji. Ishara za ushirikishi ni njia bora ya kubaini ufaafu. Tunajumuisha ishara za jumla za ushirikishi kutoka kwa watumiaji, yaani tunaweza kuangalia muda wa kutazama video fulani ya hoja fulani ili kubaini iwapo watumiaji wengine wanachukulia kuwa video hiyo inafaa hoja husika. Mwisho, kuhusu ubora, mifumo yetu imebuniwa hivi kwamba inaweza kutambua ishara zinazoweza kubaini chaneli zinazoonyesha utaalamu, weledi na kuaminika kwenye mada husika. YouTube haikubali malipo ili kuweka maudhui katika nafasi bora kwenye matokeo halisi ya utafutaji wala hatushughulikii maudhui yanayomilikiwa na Google kwa mapendeleo zaidi kuliko ya watayarishi wengine.

Mbali na vipengele hivyo vitatu vikuu, tunajitahidi kufanya matokeo ya utafutaji yafae kila mtumiaji na tunaweza pia kuzingatia historia ya mambo uliyotafuta na video ulizotazama, iwapo umeiwasha. Ndiyo maana matokeo yako ya utafutaji yanaweza kuwa tofauti na matokeo ya utafutaji ya mtumiaji mwingine kwa hoja sawa. Picha zilizo hapo chini ni mifano iliyowekwa sambamba inayoonyesha jinsi utafutaji unaofanana wa watumiaji unaweza kutofautiana kulingana na vigezo hivi.

Utafutaji kwenye YouTube Utafutaji kwenye YouTube

Matokeo ya utafutaji yanaweza kuwa tofauti kwa kila mtumiaji. Kwa mfano, kama mtumiaji hutazama video nyingi za matunda na akitafuta "nyanya', tunaweza kupendekeza video zinazoangazia matunda ya nyanya badala ya video za wanawake wakongwe.

YouTube Kids

YouTube Kids ni programu tofauti ambayo ni toleo lililochujwa la YouTube lililo na mkusanyiko mdogo zaidi wa maudhui ikilinganishwa na tovuti na programu kuu ya YouTube. Sera zetu za YouTube Kids zinabainisha aina ya maudhui yanayotimiza masharti ya kuwekwa kwenye YouTube Kids. Lazima maudhui yatii sera hizi ili yaonekane katika YouTube Kids, ikiwa ni pamoja na utafutaji kwenye YouTube Kids. YouTube Kids pia ina kifurushi kamili cha vidhibiti vya wazazi ili wazazi waweze kuweka mapendeleo kwenye hali ya utumiaji ya watoto wao, ikiwa ni pamoja na kuzima au kuwasha utafutaji. Pata maelezo zaidi.

Kwa miaka michache iliyopita, tumekuwa tukijitahidi kutoa bidhaa na kutekeleza sera zinazotusaidia kuzipa familia maudhui yenye ubora wa juu kwenye YouTube Kids. Kwa ushirikiano na wataalamu wa ukuaji wa watoto, tuliweka mkusanyiko wa kanuni za ubora ili zisaidie kuongoza watoto wetu na watayarishi wetu wa maudhui ya familia. Kwenye YouTube Kids, tunabainisha na kujumuisha video na vituo vinavyoambatana na umri na vinatii kanuni hizi za ubora. Soma maelezo zaidi hapa.

Kwa jumla, utaratibu wa kupanga matokeo ya utafutaji kwenye YouTube Kids unafanana na utaratibu wa kupanga matokeo ya utafutaji kwenye YouTube, lakini una vigezo vya ziada vya ubora na usalama wa maudhui. Tumechukua tahadhari kadhaa ili kuhakikisha kuwa familia zinazotafuta maudhui zitapata matokeo yanayofaa hadhira za walio na umri mdogo. Ili kituo au video ijumuishwe katika programu ya YouTube Kids, kwanza ni lazima maudhui yaliyomo yabainishwe na vichujio vya kiotomatiki kuwa yanafaa familia (pamoja na maoni kutoka kwa watumiaji na ukaguzi unaofanywa na binadamu kwa kiasi fulani). Pia tunaendelea kuboresha huduma kulingana na teknolojia mpya, utafiti na maoni ya watumiaji. Ukimruhusu mtoto wako atafute kwenye YouTube Kids, anapotafuta maudhui, matokeo huchujwa kulingana na mipangilio ya maudhui uliyomchagulia. Usipositisha kipengele cha historia ya video ulizotazama, huenda matokeo ya utafutaji pia yakajumuisha video zinazopendekezwa kulingana na video ambazo mtoto wako amezitazama hapo awali na hoja alizozitafuta.

Kumbuka: YouTube hushughulikia maudhui mengi ya aina mbalimbali. Kwa hivyo, hata tunapojitahidi kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa, kuna uwezekano wa mtoto wako kupata maudhui ambayo hungependa ayatazame. Hali hii ikitokea, unaweza kuripoti video husika. Tunatumia maelezo haya kuboresha YouTube Kids kwa ajili ya kila mtu.

Vidhibiti vya kufanya matokeo ya utafutaji yakufae zaidi

Tunakupa zana za kukusaidia kuchangia vigezo tunavyozingatia ili kukupa matokeo bora zaidi ya utafutaji. Ukichagua kusimamisha na kufuta historia ya mambo uliyotafuta na video ulizotazama, matokeo ya utafutaji kwenye YouTube hayatazingatia ishara hizi.

Kukuza vyanzo vya kuaminika

Katika vipengele kama vile muziki au burudani, mara kwa mara tunatumia vigezo vya ufaafu, upya au umaarufu kusaidia mifumo yetu kukuonyesha maudhui bora utakayofurahia. Hata hivyo, katika habari, siasa na maelezo ya kimatibabu au kisayansi, tunafahamu kuwa kuaminika ni muhimu.

Unapotafuta mada zinazohusiana na habari, huenda ukaona sehemu ya Habari Maarufu karibu na sehemu ya juu ya matokeo ya utafutaji, iwapo tuna maudhui yanayofaa kutoka kwa vyanzo vya habari vinavyofuata sera za maudhui ya Google News. Sehemu hii ya Habari Maarufu huonyesha matokeo yanayofaa kutoka vyanzo vya kuaminika, kama vile CNN na Fox News. Rafu ya Habari Maarufu inaweza pia kuonyeshwa kwenye ukurasa wako wa kwanza ukitazama au kutafuta maudhui ya habari. Pata maelezo zaidi kuhusu habari na maelezo ya kuaminika kwenye YouTube.

Katika baadhi ya nchi, ukitafuta kwenye YouTube mada inayohusiana na hali fulani ya afya ya mwili au akili, unaweza kuona rafu iliyo na maudhui ya afya katika matokeo yako ya utafutaji. Rafu hii ya maudhui ya afya itajumuisha video kutoka kwa vyanzo vya kuaminika vya maelezo ya afya vinavyohusiana na mada ya afya uliyotafuta. Vile vile, unapotafuta kwenye YouTube baadhi ya mada zinazohusiana na afya, huenda ukaona kidirisha cha taarifa za afya katika matokeo yako ya utafutaji. Vidirisha hivi vinaonyesha maelezo kama vile dalili, uzuiaji na chaguo za matibabu kutoka kwa vyanzo vya kuaminika vya maelezo ya afya kama vile Shirika la Afya Duniani na taasisi nyingine za matibabu. Pata maelezo zaidi kuhusu maudhui yanayohusiana na afya na jinsi YouTube hubainisha vyanzo vya kuaminika vya maelezo ya afya.

Vidirisha vyetu vya maelezo ya kuhakikisha ukweli hutoa muktadha wa ziada kwa kuangazia makala mengine yanayofaa yaliyohakikishwa ukweli, juu ya matokeo ya utafutaji kwa hoja zinazofaa. Kuna vigezo vingi vya kubaini iwapo kidirisha cha taarifa ya kuhakikisha ukweli kitaonekana kwenye utafutaji wowote ule. Kwa mfano, tunazingatia ubora, ufaafu na upya wa makala ya kuhakikisha ukweli kwenye hoja ya utafutaji. Wakati kuna makala kadhaa ya kuhakikisha ukweli kutoka kwa wachapishaji tofauti, tunaweza kuonyesha makala mengi ya kuhakikisha ukweli, ambayo huonyeshwa kulingana na ufaafu. Pata maelezo zaidi kuhusu vidirisha vingine vya maelezo vinavyotoa muktadha kwenye YouTube.

Kadi Rasmi pia huwarahisishia watumiaji mchakato wa kugundua maudhui kwa kuangazia nyenzo rasmi katika Utafutaji kwenye YouTube. Kadi hizi ni pamoja na video na machapisho rasmi kutoka vituo maarufu, kama vile vya watayarishi maarufu wa YouTube, watu mashuhuri na wasanii maarufu wa muziki. Video na machapisho pia yamejumuishwa kutoka maudhui yanayohusiana na timu za spoti, filamu na TV, muziki na matukio maalum. Kadi hizi hutolewa kiotomatiki na haziwezi kuwekewa mapendeleo.

Lengo letu ni kukupa nyenzo za kukusaidia kuelewa vigezo tunavyozingatia ili kutoa matokeo bora zaidi ya utafutaji kwa watumiaji.