Nenda kwenye maudhui
Athari na hatua tulizopiga

Hatua tulizopiga katika kudhibiti maudhui hatari

Mwongozo wa Jumuiya yetu hubainisha tunachoruhusu na tusichoruhusu kwenye YouTube. Sehemu muhimu ya wajibu wetu ni kutekeleza mwongozo huu na kuondoa maudhui yanayokiuka sera. Tumetoa pointi chache muhimu za data ili kukuonyesha hatua tunazopiga kwenye juhudi zetu za uwajibikaji - iwapo ungependa kupata maelezo zaidi, unaweza kusoma Ripoti yetu ya kina ya Utekelezaji wa Mwongozo wa Jumuiya.

Hatua tulizopiga katika kudhibiti maudhui hatari

Video ambazo zimeondolewa, kulingana na sababu

YouTube inategemea timu zilizo kote duniani kukagua video zilizoripotiwa na kuondoa maudhui yanayokiuka Mwongozo wa Jumuiya; kuwekea video masharti (k.m., kuweka masharti ya umri kwenye maudhui ambayo huenda hayafai hadhira zote); au kuendelea kuonyesha maudhui iwapo hayakiuki mwongozo wetu.

Chati hii inaonyesha idadi ya video zilizoondolewa na YouTube kulingana na sababu ya video kuondolewa. Sababu hizi za kuondoa zinafuata [Mwongozo wa Jumuiya] ya YouTube (https://support.google.com/youtube/answer/9288567). Wakaguzi hutathmini video zilizoripotiwa kwa kulinganisha na sera na Mwongozo wa Jumuiya yetu bila kujali ni kwa nini video iliripotiwa mwanzo.

Aprili 2021 hadi Juni 2021

Video zilizoondolewa, kulingana na chanzo cha kwanza cha utambuzi

Chati hii inaonyesha idadi ya video zilizoondolewa na YouTube, kulingana na chanzo cha kwanza cha utambuzi (kuripotiwa kiotomatiki au utambuzi wa watu). Ripoti kutokana na utambuzi wa watu inaweza kutoka kwa mtumiaji au mwanachama wa Mpango wa Wapigaripoti wa Kuaminika kwenye YouTube. Wanachama wa Mpango wa Wapigaripoti wa Kuaminika wanajumuisha mashirika yasiyo ya serikali na mashirika ya serikali yaliyo bora katika kuarifu YouTube kuhusu maudhui yanayokiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu.

Aprili 2021 hadi Juni 2021

Video zilizoondolewa, kulingana na mara ambazo zimetazamwa

YouTube hujitahidi kuzuia maudhui yanayovunja kanuni zetu yasitazamwe zaidi — au yasitazamwe hata kidogo — kabla yaondolewe. Kuripoti kiotomatiki hutuwezesha kuchukua hatua kwa haraka na kutekeleza kwa usahihi sera zetu. Chati hii inaonyesha asilimia ya uondoaji wa video uliofanyika kabla video hizo zitazamwe, ikilinganishwa na uondoaji uliofanyika baada ya video kutazamwa kidogo.

Aprili 2021 hadi Juni 2021