Je, YouTube huuza data ya watazamaji?
Hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote. Tunatumia taarifa tunazokusanya ili kukupa huduma zinazokufaa, ikiwa ni pamoja na kukupa mapendekezo, kuweka mapendeleo kwenye matokeo ya utafutaji na kukuonyesha matangazo yanayokufaa. Ingawa matangazo haya yanatusaidia kufadhili huduma zetu na kuzifanya zipatikane kwa kila mtu bila malipo, hatuuzi taarifa zako binafsi. YouTube kwa muda mrefu imetoa vidhibiti vya faragha ambavyo ni thabiti na muhimu, kama vile Data yako kwenye YouTube, ambavyo hukurahisishia mchakato wa kuelewa na kudhibiti data inayohifadhiwa na jinsi inavyotumiwa kwenye YouTube na Google.
Mwongozo wa Faragha wa YouTube unalenga kulinda usalama na faragha ya watumiaji huku ukisawazisha masilahi ya umma na ustahiki wa habari. Tuko makini kuhusu kulinda watumiaji wetu kwa kushughulikia masuala ya faragha yanayoweza kutokea na mwongozo huu unalenga watumiaji wote duniani. Yaani, ingawa huenda video haikiuki sheria za faragha katika nchi uliko, bado inaweza kukiuka Mwongozo wa Faragha wa YouTube.