Kifurushi chetu cha Kudhibiti Hakimiliki huwapa wenye haki udhibiti wa maudhui yao yaliyo na hakimiliki kwenye YouTube. Kifurushi hiki hutumia mchakato wa ulinganishaji wa Content ID, ambao ni teknolojia bora zaidi katika kiwango chake, inayotumiwa kutambua maudhui yanayoweza kuwa yamekiuka haki. Kinajumuisha fomu yetu ya wavuti ya umma ya Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali, inayopatikana kwa mabilioni ya watumiaji wa YouTube; Copyright Match Tool, zana yetu iliyobuniwa mahususi kwa Watayarishi na inayopatikana kwa zaidi ya watayarishi milioni 3; na Content ID, nyenzo yetu ya biashara kwa walio na mahitaji mengi ya kudhibiti hakimiliki, kama vile lebo za muziki, studio za filamu au jamii za kukusanya mirabaha.
Watumiaji wa Content ID na Copyright Match Tool huarifiwa kiotomatiki kuhusu video zilizopakiwa na watumiaji ambazo huenda zina kazi zao za ubunifu: kwenye Content ID, hili hufanywa kupitia faili za marejeleo zilizotolewa na mwenye haki; katika Copyright Match Tool, watumiaji huona video zinazolingana na walizopakia au video waliozoziondoa kupitia maombi sahihi ya kuondolewa kwa video zinazokiuka hakimiliki. Vilevile, watumiaji wa Content ID wanaweza kuchagua mapema mambo ambayo wangependa yafanyike baada ya video hizo kutambuliwa. Kutokana na chaguo tofauti ambazo Content ID huwapa wenye hakimiliki, Content ID si tu suluhisho la kukabili matukio ya kughushi, lakini pia ni zana ya kuzalisha mapato. YouTube imelipa zaidi ya Dola bilioni 9 za Marekani kwa wenye haki kufikia Desemba 2022, kutokana na mapato ya matangazo pekee katika maudhui ambayo wameyadai na kuchuma mapato humo kupitia Content ID.