Nenda kwenye maudhui
Wajibu wetu

Je, YouTube husaidia vipi kulinda watoto na vijana kwenye mfumo?

Watoto na vijana leo wanaweza kupata fursa nyingi kwenye YouTube na huja kwenye mfumo huu kupata jumuiya nzuri zinazowakilisha mambo ya kipekee yanayowavutia. Ingawa tunawapatia nafasi na zana za kupanua mawazo yao na kugundua mambo mapya, pia tunaelewa kwamba vijana hawa wanahitaji ulinzi na kuzingatiwa kwa njia ya kipekee kuhusiana na hali yao ya utumiaji na mambo mapya wanayogundua mtandaoni.

Kuimarisha usalama wa vijana

Kanuni za YouTube za Kuwalinda Vijana ni nini?

Kanuni zetu za Kuwalinda Vijana ndio mwongozo tunaofuata katika kazi yetu hapa YouTube na ni muhimu katika juhudi zetu za kuweka mazingira salama na bora zaidi kwa vijana wadogo.

Kwa kipindi cha miaka mingi, tumejitolea kukuza mfumo salama, wa ubora wa juu na unaofaa ambao unaboresha maisha ya watoto na familia kote duniani. Tumeweka nyenzo nyingi katika kubuni mkusanyiko thabiti wa sera na huduma zinazolinda jumuiya yetu yote na kuunganisha watu na vyanzo vya kuaminika, iwe ni kukabiliana na utangazaji wa matatizo ya ulaji na kujitoa uhai au kulinda dhidi ya changamoto hatari.

YouTube Kids na matumizi yanayosimamiwa ya vijana wadogo na vijana ni nini?

YouTube hutoa matumizi kadhaa ili kukidhi mahitaji ya ukuaji wa watoto na vijana pamoja na kuwapa walezi zana, vipengele na usaidizi wa kuchagua matumizi ya mtandaoni yanayofaa familia zao. Huduma na sera zetu zinabadilika kadiri watoto na vijana wanavyoendelea kubadilisha namna wanavyotumia mtandao.

  • YouTube Kids (ya watoto walio na umri usiozidi miaka 12) ni programu tofauti iliyobuniwa kikamilifu ili itumiwe na watoto kwa usalama na urahisi. Ina zana za wazazi na walezi za kuwaongoza watoto wanapoitumia.

  • Matumizi yanayosimamiwa ya vijana wadogo (watoto walio chini ya umri wa miaka 13 au umri unaofaa katika nchi au eneo lao) yanawalenga wazazi wanaoamua kuwa watoto wao wanaweza kutazama maudhui kwenye programu kuu ya YouTube, lakini wangependa kuwa na uwezo wa kubadilisha hali ya utumiaji wa watoto wao. Yanatoa mipangilio mitatu ya maudhui inayokidhi miundo tofauti ya ulezi na tofauti za binafsi katika ukuaji wa mtoto. Kila mpangilio unawezesha ufikiaji wa kiwango kikubwa zaidi wa maudhui kwenye YouTube.

  • Matumizi yanayosimamiwa ya vijana (wa umri wa kati ya miaka 13 hadi 17 katika nchi na maeneo mengi) yanawaruhusu wazazi na vijana kuunganisha akaunti kwa hiari ili kusaidia kuwafahamisha wazazi kuhusu jinsi vijana wao wanavyotumia YouTube na maudhui wanayotayarisha, kuanzisha mazungumzo kati ya wazazi na vijana pamoja na kuwapatia fursa za wakati unaofaa wa kujifunza kuhusu jinsi ya kutayarisha maudhui kwa njia salama kwenye YouTube.

Hatua zipi za usalama wa watoto zinapatikana kwenye programu kuu ya YouTube?

Tunawekeza zaidi kwenye teknolojia na timu zinazosaidia kuwapa watoto na familia ulinzi bora zaidi iwezekanavyo.

Kwenye YouTube, tunawahitaji watumiaji wawe na umri wa miaka 13 (au umri unaoruhusiwa katika nchi waliko) isipokuwa waruhusiwe vinginevyo na mzazi au mlezi. Mwongozo wa Jumuiya yetu hubainisha maudhui ambayo hayaruhusiwi kwenye mfumo na sera mahususi za usalama wa watoto haziruhusu maudhui yanayoweza kusababisha hatari fulani kwa watoto.

Kwenye YouTube Kids, tunajitahidi kubaini maudhui yanayoambatana na umri, yanayotii kanuni zetu za ubora na ambayo ni anuai kiasi cha kutimiza mambo mbalimbali yanayowavutia watoto kote duniani. Hii ni pamoja na sera za maudhui mahususi zilizobuniwa kupitia maoni kutoka kwa wataalamu wa nje wanaoshughulikia masuala ya malezi ya watoto, maudhui ya watoto, mafunzo dijitali na uraia.

Tunaendelea kukuza mfumo wetu ili kuhakikisha kuwa tunabuni mazingira yanayofaa maudhui ya familia kwenye YouTube na kuboresha sera na bidhaa zetu zinazoangazia mchango kutoka kwa wataalamu wa nje na wa ndani panapofaa.

Je, YouTube inakusanya data ya watoto ili kuwaonyesha matangazo?

Tunachukulia data kutoka kwa mtu yeyote anayetazama maudhui yaliyobainishwa kuwa 'yanalenga watoto' kwenye YouTube, kuwa yanatoka kwa mtoto, bila kujali umri wa mtumiaji. Hii inamaanisha kuwa, kwenye video 'zinazolenga watoto', tunapunguza ukusanyaji na matumizi ya data. Kwa sababu hiyo, tunapaswa kuzuia au kuzima baadhi ya vipengele vya bidhaa. Kwa mfano, hatuonyeshi matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwenye maudhui 'yanayolenga watoto', na baadhi ya vipengele havipatikani kwenye video hizi, kama vile maoni na arifa. Watayarishi wote wanatakiwa kubaini iwapo maudhui yao 'yanalenga watoto' au hayawalengi.

Matangazo yaliyowekewa mapendeleo hayaruhusiwi kwenye YouTube Kids na pia kwa wanaotumia hali ya utumiaji inayosimamiwa kwenye YouTube. Hii inamaanisha kuwa matangazo yanayoonekana hulinganishwa na video zinazotazamwa kulingana na maudhui, si mtumiaji mahususi anayetazama.

YouTube inalinda vipi watoto wanaochapisha maudhui kama Watayarishi au wanaoonekana kwenye video za Watayarishi wengine?

Kama ilivyobainishwa kwenye Sheria na Masharti yetu , watoto walio na umri unaofaa wa kutoa idhini wanaweza kutumia YouTube au YouTube Kids (zinapopatikana) ikiruhusiwa na mzazi au mlezi wa kisheria.

Kwenye YouTube Kids na katika hali ya utumiaji inayosimamiwa na mzazi kwenye YouTube, watoto hawawezi kupakia maudhui, kutiririsha moja kwa moja, kusoma au kuandika maoni, au kufikia vipengele vyovyote vinavyohusu miamala ya fedha. Tuna ulinzi wa ziada wa watoto kwenye mitiririko ya moja kwa moja, kama vile kufunga mitiririko inayoangazia watoto ambao hawaonekani kuwa pamoja na mtu mzima.

Tunatoa pia mbinu bora za usalama wa watoto na vidokezo vya wazi kwa Watayarishi walio na watoto katika video zao ili wafahamu wajibu wao kisheria. Mbali na kupata idhini, ni wajibu wao kutii sheria, kanuni na masharti yote yanayotumika wakionyesha watoto katika maudhui yao - ikiwa ni pamoja na vibali vinavyohitajika, malipo au ugavi wa mapato, shule na elimu; na mazingira na saa za kazi.

YouTube huzuia vipi ufikiaji wa maudhui ya watu wazima?

Tumejitolea kuweka hali zinazofaa umri wakati watu wanafungua YouTube. Tunatambua kuwa Watayarishi ndio wana uwezo bora wa kuamua anayepaswa kuona maudhui yao, kwa hivyo tunawapa uwezo wa kuweka masharti ya umri kwenye maudhui yao wenyewe panapofaa. Maudhui yanapowekewa masharti ya umri, lazima watazamaji wanaofungua YouTube waingie katika akaunti yao na lazima umri kwenye akaunti yao uwe miaka 18 au zaidi ili waweza kutazama video. Iwapo hawajafikisha umri huo, wataona onyo na kuelekezwa kwingine ili wapate maudhui yanayofaa kwa umri wa watoto. Mwongozo wa Jumuiya yetu una taratibu kwa wanaopakia kuhusu wakati maudhui yanapaswa kuwekewa masharti ya umri.

Wahakiki wetu huweka mipaka ya umri iwapo wanapohakiki maudhui, wataona video ambayo haifai watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18. Pia tunatumia teknolojia ya mashine kujifunza kutambua maudhui ili kutusaidia kutekeleza kiotomatiki mipaka ya umri panapohitajika. Wanaopakia wanaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi iwapo wanaamini kuwa ulitekelezwa kimakosa.

Ili kuhakikisha kuwa hali za utazamaji hazibadiliki, watazamaji wanaojaribu kufikia video zilizo na masharti ya umri katika tovuti nyingi za wengine wataelekezwa kwenye YouTube ambapo ni lazima waingie katika akaunti na wawe na umri wa zaidi ya miaka 18 ili watazame. Hili husaidia kuhakikisha kuwa, bila kujali mahali ambapo video imegunduliwa, itaweza tu kutazamwa na hadhira inayofaa.

YouTube hulinda vipi watoto ambao huonekana katika hali hatari kwenye video?

Tumekuwa na sera wazi dhidi ya video, orodha za kucheza, vijipicha na maoni kwenye YouTube yanayonyanyasa watoto kingono au kuwadhulumu. Tunatumia mifumo ya mashine kujifunza kujaribu kutambua ukiukaji wa sera hizi na tuna wakaguzi kote duniani ambao huondoa kwa haraka ukiukaji unaotambuliwa na mifumo yetu au unaoripotiwa na watumiaji. Tunafunga mara moja akaunti za wale wanaolenga kunyanyasa watoto kingono au kuwadhulumu na tunaripoti shughuli zisizo halali kwa Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaoyanyaswa (NCMEC), ambacho hushirikiana na mashirika ya dunia ya kutelekeza sheria.

Ingawa baadhi ya maudhui yanayoangazia watoto huenda hayakiuki sera zetu, tunatambua kuwa watoto hao wanaweza kuwa katika hatari ya kudhulumiwa mtandaoni au nje ya mtandao. Hii ndiyo maana tunachukua makini zaidi katika utekelezaji wetu. Mifumo yetu ya mashine kujifunza husaidia kutambua mapema video zinazoweza kuhatarisha watoto na kutekeleza ulinzi wetu kwa haraka, kama vile kuzuia vipengele vya moja kwa moja, kuzima kipengele cha maoni na kupunguza mapendekezo.

Pia tunashirikiana na wadau wa sekta, ikiwa ni pamoja na kampuni za teknolojia na Mashirika Yasiyo ya Serikali kwa kutoa teknolojia yetu inayoongoza ya mashine kujifunza kwa ajili ya kukabili maudhui ya CSAI (Maudhui Yanayoonyesha Unyanyasaji wa Ngono Dhidi ya Watoto) mtandaoni. Teknolojia hii inaturuhusu kutambua Maudhui ambayo yanajulikana, yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAI) katika maudhui mengi mazuri. Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAI) yakipatikana, huripotiwa kwa washirika ili wayaripoti kwa kuwajibika kwa mujibu wa sheria na kanuni za mahali ulipo.

Ifahamu Kamati ya Ushauri ya Vijana na Familia